Leo ni siku ya Tano, tangu nimeamua kuacha Kupiga Punyeto.
Najua kuna namna na wengine wanapitia katika hali hii na hawapendi kupiga Punyeto, Napenda kukutaarifu kuwa inawezekana Mi nimedhamiria na kila siku katika hii Thread (Uzi) nitakuwa nawashirikisha hatua ninazopitia katika kuacha kwangu.
Ukiwa na ushauri ukiandika hapa itasaidia na wengine ambao wamedhamiria kuacha kupiga Punyeto au Kujichua. Si kila mtu anaweza kuweka wazi msimamo wake ila wengi wanatamani kujifunza jinsi ya Kuacha hivyo karibu tushirkishe na amini katika kusaidiana
Namshukuru Mungu nimedhamiria, nimekusudia Na Mungu ananiwezesha na Akili imeshasema noo Punyeto Tena.