#COVID19 Ushuhuda wa Mchungaji Godwin Chilewa kuhusu COVID-19: Je, tunamficha nani, kwanini na kwa Faida gani?

#COVID19 Ushuhuda wa Mchungaji Godwin Chilewa kuhusu COVID-19: Je, tunamficha nani, kwanini na kwa Faida gani?

Sasa wanavyo tuhamasisha tujifukize lengo lao nini haswa? Kama hata hiyo ina madhara mbona watanzania tutaisha kwa mtindo huo

Hawataki kujishughulisha na matatizo yenu, wanakupeni shortcut ili mpate hope kuwa kuna kitu kinafanyika na ili pia waweze kujivua lawama!
 
Umeandika maandishi mengi kutaka kufanya kama yana maana kwani ulipita nchi ngapi au hiyo ndege ilitoka direct Tz!
 
Asante mleta mada someni ni muhimu.
1. Corona ni gonjwa serious, tumuombe Mungu atunusuru.
2. Kila mmoja achukue wajibu binafsi kujilinda na kuwakinga wengine.
3. Kwa kuwa ni garama kubwa tutumie kila tiba asili iliyothibitika,lishe nk.
4. Serikali itimize wajibu wake wa msingi kuwa na mpango dhabiti na sio kukwepa wajibu.
 
Acha kupotray ujinga wako mkuu,

Hoja ya msingi ya makala hii ni hukosefu wa uwajibikaji wa serikali katika kulishughulikia hii changamoto ya ugonjwa wa COVID-19.

Weka mihemuko pembeni and be reasonable utaona jinsi afya za watanzania zimewekwa rehani ili kufanyiwa majaribio.

Kwa nini iwe hivyo wakati tunazo mamlaka zilizokabidhiwa jukumu la kusimamia, na kuratibu utoaji wa huduma za afya kwa msingi wa kisayansi?
 
Binafsi nlipoanza kupata such symptoms nilikimbilia kutumia tuba asilia pamoja na hizo za kufukiza nyungu. Lkn hazijasaidia na zilinipelekea shida ya upumuaji kwa vile wadudu waliendelea kushambulia kifua na mapafu.
Niliporudi kwa doctor aliniambia niache kujifukiza mara moja ni hatari kwa pumzi.
halafu ukapona baada ya kunywa pilton.
 
Asante Sana Rev Godwin Chilewa, kwa kuelezea umma wa Watanzania ukweli juu ya madhara ya Covid-19 na uongo wa viongozi wetu chini ya Rais John Magufuli, ambaye ndo muanzilishi wa uongo huu.

Kwa mujibu wa watalamu toka Marekani Rev Chilewa, amesema dhahiri ya kuwa Mgonjwa wa COVID-19 anahitaji Oxygen na sio mvuke. Bahati nzuri Kwake alitibiwa huko na kama angebaki Dar huyu naye tunge mpoteza.

Hivi JPM anaamua kudanganya ili lengo lake iwe Nini? na atapata faida gani watanzania wakiendelea kufa kwa maelfu kama ilivyo sasa wakati yeye na wasaidizi wake washapata chanjo toka CHINA?

Be Blessed we have along journey to go !
 
Jamaa wana plana nzuri sana ya kutibu korona. Na plana lama hiyo hutolewa na wizara ya afya. Hapa kwetu Gwajima asiishie tu kuonyesha anapiga nyungu na kunywa pilipili. Waandae muongozo kwa wataalamu wa afya wa jinsi ya kutibu hii kitu.
 
Whatever it is.......yawezekana nyungu na tangawizu vinafanya kazi kweli au havifanyi kazi.....na yawezekana chanjo za mzungu hazifanyi kazi kweli au zinafanya kazi au zina madhara flani sawa....

Ila mi kwangu tatizo Ni jinsi Serikali inavokataa haya maswala ya sayansi kwa kiburi Tena hadharani.....!!!!
Na Sasa WHO ime exclude Tanzania na Burundi kwnye mpango huo was chanjo ya Covid....!!!

That may not be problem..
Lakini hili swala linanipeleka mbali kuwaza hivi hiki kiburi tulichokionesha mpaka mataifa pamoja na WHO kutuacha tujiendeshe tunavoona Sanaa, je siku ikija kutokea serious disease ingine kabisa tofauti na hii hapa Bongo tutawaomba WHO kutupa msaada tukiwa na sura za aina ipi......!!!!

Kuna njia nyingi za kukataa matibabu na sio kosa kisheria lakini sisi tumeyakataa matibabu kwa kiburi na kejeli nyingi Sana.

Let's see
 
Back
Top Bottom