#COVID19 Ushuhuda wa Mchungaji Godwin Chilewa kuhusu COVID-19: Je, tunamficha nani, kwanini na kwa Faida gani?

#COVID19 Ushuhuda wa Mchungaji Godwin Chilewa kuhusu COVID-19: Je, tunamficha nani, kwanini na kwa Faida gani?

Mimi binafsi nilougua hii kitu. Hata uzi wangu upo humu na nilieleza jinsi nilivyokuwa nikijifukiza kwa siku mara 3 ila hali ndyo ilikuwa inazidi kuwa ngumu.

Nilikuja kupewa ushauru na sista angu ambaye ni nesi marekani kuwa nitumie dawa za kupunguza maumivu na aspilini junior. Na nijitahidi kupunguza kulala maana ukilala ndyo unazidi kuwa week na covid ndyo inachukua point kukushambulia.

So nikawa natumia izo dawa kila baada ya masaa 4 najisikia mwili upo safi natembea tembea bila kulala. Siku mbili tu nikawa kama nimepona.

Mke wangu naye akaugua hakupiga nyungi akatumia dawa za maumivu na kufanya mazoezi hata haikumchukua muda akarecover haraka sana.
 
Unaongelea wanamichezo ambao ni vijana. Popote duniani covid haisumbui vijana. Inapita na wazee. Na ukiipata kama mzee hutakiwi kupiga mazoezi sana. Unaweza kufa sababu ya oxygen intake inapokuwa altered unapopiga mazoezi.
 
Yaani mkuu hata kama hawakuandaliwa mtu kuandika negative...ukweli ni kwamba wanaripua tu kutoa majibu....wageni ni wengi sana unadhani wanao huo muda wa kuwa accurate.....
Mambo ya kina Elizabeth Ann, kikubwa kukusanya hizo$100..

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Ukweli ni kuwa Rais Magufuli anawaua Watanzania.

Alipewa fedha nyingi ili kupambana na Civid 19. Viongozi wengi wa Africa, wenye akili, wakiwemo viongozi wa Kenya, walitumia fedha hizo kununua vifaa tiba. Lakini Rais wa kwetu akapeleka fedha hiyo kwenye uchaguzi. Leo hospitali zetu hazina vifaa vya kisasa wala madawa ya kupambana na Covid 19. Na kwa vile hakuna fedha, wananchi wananendelea kudanganywa watumie huo uchafu wa nyungu, eti ndiyo tiba.

Pamoja na kwamba, amekwishaharibu, ni vema asiendelee kuharibu. Asimamishe kupeleka fedha kwenye miradi ya SGR na bwawa, kama dharula, tuagize vifaa kuokoa maisha ya watu wetu ambao sasa wanakufa kwa mamia kila siku. Tunaiwaandika humu ni sample tu lakini wengi wasio na majina makubwa wanateketea kimya kimya!
 
Pole ndugu yetu.kwenye haya mambo ya kusema uongo dhidi ya covid_ 19 hata Mimi nimeyashuhudia.kwa kifupi ni kuwa kwenye issue ya Corona,Tanzania na watanzania tumekosa leadership,kukosa kwetu leadership ukichanganya na umasikini tulionao plus ujinga wa mtanzania,inakuwa msiba mzito kwa taifa hili.tutakufa sana
 
Akuna wa kunichanganya kwasasa,nikijihisi ovyo napiga nyungu.
Wataalam wanasema mazoezi ni sehemu ya kuweka mwili sawa.ukiacha kucheza soka nafanya pia mazoezi ya gym.

Wapinga nyungu na dawa za asili wa mitandaoni wanazuga tu ila wanatumia vizuri tena kwa vipimo sahihi.watakao achwa kwenye mataa ni wafata mkumbo.
 
Minahitaji msaada kidogo wa kujua kutoka kwa huyu mtumishi wa Mungu. Hivi aliyefeli hapa ni huyu mtumishi wa Mungu aliyetumwa na Mungu au Mungu mwenyewe kafeli. Kwa sababu huko nyuma wazee wetu Mungu wao alizuia magonjwa nyemelezi na yaliondoka huyu Mungu wa kisasa wa kanisani inakuwaje? Maana juzi kati sisi mzee wangu ambaye ni mchungaji yeye alitutangazia kanisani kuwa tuwasikilize wataalamu wa afya na wizara ya afya, Mimi kwa uelewa wangu niliona mzee anaweza sababisha sadaka ikapelekwa kwa wataalamu wa afya na tukafa na nja nyumbani.
 
KWANZA, sioni jipya ambalo halijulikani na sidhani kama kweli wewe unaishi Marekani.
PILI, mojawapo ya maelekezo ya kupambana na CORONA ni kutofanya safari kama hakuna ulazima- wewe nawe siyo mwangalifu kwa kitendo chako cha kusafiri wakati huu.
 
Pole ndugu yetu.kwenye haya mambo ya kusema uongo dhidi ya covid_ 19 hata Mimi nimeyashuhudia.kwa kifupi ni kuwa kwenye issue ya Corona,Tanzania na watanzania tumekosa leadership,kukosa kwetu leadership ukichanganya na umasikini tulionao plus ujinga wa mtanzania,inakuwa msiba mzito kwa taifa hili.tutakufa sana
Umeongea point kubwa
1. Poor leadership
2. Umasikini wetu
3. Ujinga wa watu wetu
 
KWANZA, sioni jipya ambalo halijulikani na sidhani kama kweli wewe unaishi Marekani.
PILI, mojawapo ya maelekezo ya kupambana na CORONA ni kutofanya safari kama hakuna ulazima- wewe nawe siyo mwangalifu kwa kitendo chako cha kusafiri wakati huu.
Unataka jipya la zamani umeshalisolve?
 
Asante kwa kutufumbua macho. Wewe ni mzalendo wa kweli unayejali maisha ya watanzania wenzio. Ukweli utatuweka huru!
Mungu akubariki sana.
 
Usimhusishe Mungu na mambo ya kijinga. Unadhani Mungu yuko Tanzania tu kwingine hayuko? Unadhani sisi tu ndio tunajua kuomba?

Korona ipo. Kila mwenye akili anajua hivyo! Tunatakiwa kuchukua hatua na serikali inatakiwa kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom