mzamifu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2010
- 6,400
- 3,853
Tunaihujumu dunia kwa haya. Kama kweli nyungu inaponya basi tuweke bayana tafiti ya kisayansi jinsi ilivyo na tuisadie dunia kupona. Kwa nini hii ni pekee kwa Tanzania. Mbona tunajimwambafy hivi.Unajenga immunity kwa gharama ya watu wasio na hatia? Je kujenga immunity ndo kunatufanya tuseme uongo kuhusu Corona? Kujenga immunity ndo kunatufanya tusitunze data sahihi ili kutuwezesha kufanya tadhimini kesho kujua Kama njia tuliyochukua was good or no ukilinganisha na njia walizo chagua wengine?
Huu mtindo wa Kinjekitile unaaminika vipi. Au tuseme Tanzania ni mteule wa Mungu kama ilivyosemwa kwa Israeli.
Ikiwa watu watateswa na ugonjwa huu kwa sababu ya misimamo yetu basi na tuwe tayari kuwajibika. Na kama kwa msimamo huu tunaleta uponyaji basi sifa zije kwetu.