Ushuhuda wa ndoa ya wazazi wangu, baba aliachishwa kazi ghafla miaka 14 iliyopita. Mama amekuwa ndio kila kitu

Hekima94

Member
Joined
Mar 16, 2017
Posts
32
Reaction score
90
Habari wana JF
Leo nawapa ushuhuda wa maisha ya ndoa ya wazazi wangu...

Baba aliachishwa kazi ghafla miaka 14 iliyopita. Mama anafanya biashara ndogondogo amekuwa ndio kila kitu chakula, mavazi, ada za shule na mahitaji mengine...

Wakati baba anaendelea kufatilia kesi yake ya kuachishwa kazi bila sababu na fidia zake ambazo hakuweza kuzipata mpaka tunamzika mwaka jana RIP....

SOMO
Je, wanawake wa sasa hivi wanaweza kuishi na mwanaume asiye na kipato kwa miaka 14 bila hata kusikia ugomvi wa masuala ya kifedha...

Kila nikimuangalia mama huwa najiuliza, wapi naweza kupata aina hii ya wanawake ili niishi kwa amani nikijua kwamba nina jembe ndani. Hata siku nikikosa naweza kurudi nyumbani nikamwambia akanielewa...

Mahusiano siku hizi bila pesa hayaendi kabisaa....

Ndoa zimekuwa kama business partnership....
 
Achana na maneno ya kuambiwa na mama yako wewe chunguza sababu kuu ya kifo cha baba yako halafu urudi tena hapa..
 
Mbona mnatutilia mashaka sana? Show trust to ur wife...ukimuonyesha kumuamini kamwe hatavunja hyo imani...
Acha hizo, hakuna cha trust wala nini! Mwanaume akifulia hakuna amani tena! Kifo nje nje kwa stress sababu kuu ni mwanamke! Mimi niliponea kiduchu kufa kabla sijapindua meza
 
Mzee hana kazi kwa miaka 14, anabaki nyumbani bila kujishughulisha kwa miaka yote hiyo?

Kuna tatizo mahali. Alishindwa hata kufuga kuku aisee ...huko kazini walikuwa na haki ya kumtimua sio siri.
 
Acha hizo, hakuna cha trust wala nini! Mwanaume akifulia hakuna amani tena! Kifo nje nje kwa stress sababu kuu ni mwanamke! Mimi niliponea kiduchu kufa kabla sijapindua meza
Pole kwa yaliyokusibu...hayo ni yako mkuu...
 
Mimi mzee aliachishwa kazi

Alikaa kitaa miaka 4 juu ya mawe Hana ramani.

Bimkubwa alisimamia shoo zote za home.

Hadi mzee akaja pata kazi tena sehemu nyingine. Maisha yakastabilize

Leo wote tumesepa home wako wenyewe tu. Na kazi zao.

Wanawake wa dizaini hii washaisha hawako

Labda umtoe kijijini hasa vijiji vya nyanda za juu kusini huko.
 
Ndoa zimekuwa kama business partnership....
Sio zimekua ndoa za siku hizi ndio hivyo hawa wanawake wanajali sana wallet, Ila kwa UPANDE mwingine yaweza kua huo mtaji wa biashara Baba yako ndio alifanya manuva akampa Mama yako afanye biashara maisha yaende wazazi wana Siri nyingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…