ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Jana limenitokea tukio la kusingiziwa utapeli, ilikuwa hivi:
Nilikuwa bar fulani mchana wa saa 10 karibu na ofisi kwetu napumzika, sasa nikaishiwa hela nikamwambia muhudumu naenda kuchukua 10000 nimeiacha ofisini me nikaondoka. Nikafika ofisini baada ya kama dakika 6 nipo kwa nje anakuja dogo muuza mayai ananiulizia wewe ndo ndege nikamjibu ndio, akauliza nimetapeliwa na mtu anafanana na wewe karibu na bar uliyokuwa unakunywa ameniambia nimpe 7000 anaingia ghetto kwake akirudi na 10000 atakula mayai ya 3000 na alikuwa amevaa shati la ki draft kama wewe.akaenda bar akaambiwa ndege ametoka sasa hivi akaelekezwa ofisini kwetu aje aone kama ni mimi.
Nilistajaabu sana nikahamaki una uhakika ni mimi nimekuibia? Dogo hana uhakika point yake ni kwamba mwizi wake ni mrefu na mweupe kama mimi na anaongea kichaga kama mimi. Kama masihara wakajaa bodaboda na watu wa mtaani kwetu na wakanigeuka mimi wakidai nimpe 7000 yake dogo ili nimalize huo mzozo na ukicheki mfukoni nina 10000 iliyobaki.
Nilibisha sana kwa kuwa mimi, sihusiki. Watu wakajaa ikawa aibu maana ni mazingira karibu na ofisi mambo yakawa mengi tukarudi mpaka bar kuuliza mpaka njia niliyopita watu kibao kama 15 hivi wananifuata baada ya mzozo mkubwa ushahidi ukaonekana kuwa sihusiki.
Nimewaza kumbe wako watu wanachomwa moto kwa kusingiziwa, usijichukulie sheria mkononi kama huna uhakika hujaibiwa acha wampige wao, we usimguse mtuhumiwa achana nae.