Ushuhuda: Wanaochomwa moto kwa kuiba siyo kweli wote ni wezi

Ushuhuda: Wanaochomwa moto kwa kuiba siyo kweli wote ni wezi

Duuuh,kuna watu makatili sana
Sure!! Mfano kisa kimoja ktk hivyo viwili nilivyoshuhudia kilitokea Chuoni, Mshkaji alikua ni Mwalimu wa Secondary iliyopo karibu na chuo, akawa anamuhudumia demu fresh tu, akampa PC yake ili demu a file vitu vyake vizuri, kumbe demu anamshkaji mwengine wanasoma wote, Teacher akagundua akaona isiwe taabu ajikatae kivyake, sasa alipofuata PC yake hostel kwa demu ndo kisanga kikamkuta! Demu akamuitia Mwizi maana Teacher alimkuta na hako kajamaa kake, Dem ili kuzuga akaamua amuitie mwizi tu!

Wananchi nao wakawa hawana cha kujiuliza, yaani jamaa alikufa akiwa kavaa shati, suruali ya kitambaa na moka zake, dizain kama alitoroka Job kidogo akachukue PC ndo yakamkuta, ilikua saa nne asubuhi.
 
Duh aiseee inatisha.

Imenikumbusha ule mkasa wa dada wa chuo mabibo hosteli kumuitia Mpenzi wake ukunga wa mwizi na kurestishwa in peace.

Pole sana
Dawa akikuitia mwizi kaa hapo hapo. Usiondoke. Halafu wakifika pale wale watu anza kutoa vielelezo kuwa unajuana na huyu mtu na ulifikajefikaje hapo mlipo.

Mwisho wa siku msikilizwe nyote ukweli utajulikana. Hakikisha unamalizana nae kwa gharama kubwa upande wake ili iwe fundisho kwake na kwa wenzake wenye tabia kama yake.
 
Sure!! Mfano kisa kimoja ktk hivyo viwili nilivyoshuhudia kilitokea Chuoni, Mshkaji alikua ni Mwalimu wa Secondary iliyopo karibu na chuo, akawa anamuhudumia demu fresh tu, akampa PC yake ili demu a file vitu vyake vizuri, kumbe demu anamshkaji mwengine wanasoma wote, Teacher akagundua akaona isiwe taabu ajikatae kivyake, sasa alipofuata PC yake hostel kwa demu ndo kisanga kikamkuta! Demu akamuitia Mwizi maana Teacher alimkuta na hako kajamaa kake, Dem ili kuzuga akaamua amuitie mwizi tu!

Wananchi nao wakawa hawana cha kujiuliza, yaani jamaa alikufa akiwa kavaa shati, suruali ya kitambaa na moka zake, dizain kama alitoroka Job kidogo akachukue PC ndo yakamkuta, ilikua saa nne asubuhi.
Huyu jamaa alikua yule wa SAUT?
 
Pole sana mkuu
Pole sana mkuu,

Mwaka 2016 kuna dogo alimnunulia Godoro mpenzi wake, sasa siku moja dogo kampigia simu huyo babe wake huyo akawa hapatikani, licha ya kupiga Mara kadhaa hali ikawa ile ile, dogo akaona isiwe kesi, akatimba kwa mpenzi bila taarifa, ndipo alipomkuta bonge la bwana miraba minne, ambapo hangeweza hata kuanzisha ugomvi.

Njemba ikaondoka ikamwacha yeye dogo na demu wake,kama kupatana wapatane au waachane njemba haikutaka kujua,

Dogo akaona kuliko kuendelea na demu Malaya na mchafu, bora achukue godoro lake,
Akaingia inside akachomoa mattress yake tano kwa sita inches nane, akatoka nalo nje, ndipo ukawa mwisho wa maisha yake baada ya kupigiwa kelele moja tu.,

Mwiziiiiiiiiiio ananibia godoroooo,

Raia walikotoka na hasira zao, na ukizingatia dogo kakutwa na ushahidi, Godoro Dodoma ipo mgongoni?

Hili tukio lilinitesa kwa muda mrefu sana kulingana na nilivyomjua yule dogo, tuliheshimiana, aliniita Faza , alinikubali na nilimkubali kinomanoma, yaani Kuna wale madogo hata ukimtuma kitu hakatai kutokana na mnavyoheshimiana, nililia sana, ama kweli Dunia haina huruma.
 
Kwann haukufahamisha familia yake ili huyo binti afikishwe mahakani. Maana hawa mabinti wa siku hizi wanajifanya akili zipo fyatu sana sasa bila kuwaadabisha wanakuwa wanajiona ni werevu. Sasa inabidi wapatikane wachache wa kuwatolea mfano.
 
Mkuu baada ya kifo Cha dogo na majirani kadhaa kueleza kuwa huyo ni mpenzi wake wa siku nyingi raia walitaka kumpiga yule Binti lakini uwepo wa polisi ukamuokoa , na yupo gerezani hadi hii leo
 
Dawa akikuitia mwizi kaa hapo hapo. Usiondoke. Halafu wakifika pale wale watu anza kutoa vielelezo kuwa unajuana na huyu mtu na ulifikajefikaje hapo mlipo.

Mwisho wa siku msikilizwe nyote ukweli utajulikana. Hakikisha unamalizana nae kwa gharama kubwa upande wake ili iwe fundisho kwake na kwa wenzake wenye tabia kama yake.
Hata ukikaa Kuna watu wakifika hawaulizi, omba MUNGU tu
 
Mkuu, Hilo zogo la raia unafikiri utasikilizwa?
 
Pamoja na yote, wakuu nashauri vitu viwili, cha kwanza tuangalie namna tunajiweka weka. Yani mavazi yetu, mtindo wa nywele mpaka maongezi. Na pili tujiamini vya kutosha, hata linapotokea tatizo na raia wanaangalia reaction yako baada ya kuitwa mwizi.

Sisemi ambao wanajiweka kiheshima na kujiamini hawapigwi kwa kelele za mwizi, bali asilimia kubwa ya wanaouwawa ukiwaona hata wewe unapata wasiwasi, unakuta mtu amenyoa kihuni, amevaa manguo yamechanika kwamba ndio fasheni na kibaya zaidi hajiamini, akiitiwa mwizi anakimbia akidhani atawazidi spidi raia 500 wenye ushirikiano.

Hata mtoa mada naamini kwa sehemu kubwa hivi viwili ndivyo vimemuokoa, angekuwa amevaa hovyo hovyo na hajiamini hata muda wa kumsikiliza watu wasingempa, wangeshamaliza kazi.
 
Kuna kisa kimoja kinafanania na hii ya kuitia mwizi ila yenyewe haikuwa kubambikia wizi bali kubakwa.

Kuna jamaa yangu alinipigia simu tukutane maeneo ya sanene. So nikaenda na tulipanga tukutane na tutumie gari yake. Tumefika kuna kapub kapo mitaa hiyo tukapoa kidogo nikawa simuelewi nikimwambia tuondoke naona yupo yupo kama kuna kitu anasubiria.

Kumbe kuna mhudumu pale amepanga kumvua nikaja jua baadae baada ya kumuuliza. So akasema ratiba imebadilika ilikuwa twende kitambaa cheupe ila ngoja kwanza tumpeleke binti kwake kisha tutarejea kwenda kitambaa.

Tulivuta muda kidogo pale hadi ikatimia saa tano yule binti akatoka tukaingia kwenye gari ya mshikaji haooo tukaanza safari. Anakaa huku wanaita malamba mawili karibia na standi ya mbezi. Basi tukampeleka.

Tulipofika gari tukaipaki sehemu sio mbali na anapoishi mimi nikamwambia jamaa wacha nibakie kwenye gari nakusikilizia.

Wakaenda kule ilipita kama nusu saa hivi me nikihisi jamaa huko atakuwa alifanikiwa kutifua. Kumbe sivyo bwana. Kule ndani kulikuwa na mzozo. Walipofika binti alimuonyesha jamaa kuwa yupo vema kuruka nae. Wakashikana shikana and at some point, bint akaanza mwambia jamaa alale tu asisepe jamaa akamwambia hataweza maana mwanamke wake atahoji alipokuwa na yeye huwa halali nje ya kwake.

Binti akaanza kama kufosi hivi. Akawa amebadilika sasa sijui ni pombe zile. Akawa anataka jamaa azime simu halafu abakie asisepe akawa kama ameonyesha hali ya wivu ghafla kama nyumba ndogo kwamba kwann ashindwe kulala kwake.

Huku na kule demu akamkunja jamaa akamwambia hapa huondoki. Jamaa akaona huyu vipi bange nini. Akataka kitoka demu akamwambia hapa hamna kuondoka ama sivyo nakupigia kelele za kunibaka, jamaa akabakia kuduwaa akaanza kushikana nae kuvutana. Demu anaanza kulia akajichania nguo aliyovaa akaanza kupiga kelele kama mtu ambaye anabakwa. Sasa mtu unabakwa vipi na mtu ambaye hajatoa hata nguo, halafu kwako na mliingia wote na mlikaa kwa zaidi ya nusu saa?!

Basi jamaa akamshika akamsukumia nje. Muda wote huu mimi sina habari nakuja stushwa na mlio wa kitu kama jiwe la udongo limetupwa kwenye ubavu wa gari. Nikashtuka na kugeuka namuona mshikaji anarumbana na yule dada kama watu waliofumaniana sasa wanazinguana. Nikashuka kutazama nini kinaendelea demu anarusha mawe akilenga gari. Mimi nikaanza kumbwekea ili kumtuliza asilete wazimu wake.

Jamaa kuna jiwe lilirushwa likapiga kwenye bampa ya nyuma ikabidi tumfuate yule demu alitoka nduki akirudi alipotoka. Sasa maneno aliyokuwa anatamka ndio nikasema hawa mabinti wengi wao akili hazipo sawa. Akakimbilia kwake akaingia straight bafuni akiita watu as if anabakwa. Wakatokea majirani pale kufika ikawa story ya nini kinaendelea. Yule jamaa yangu akahadithia kila kitu demu anajifanya analilia bafuni hataki kutoka.

Baada ya kubananishwa na kuambiwa watu wapo hapa nje njoo hakuna wa kukushambulia demu anagoma kutoka anaona aibu. Mimi nikawaambia huyu ana bahati sisi tumeamua isiwe kesi hapa tungemalizana nae kwa kuita polisi akafunguliwe mashitaka. Majirani wakatusii sana tumpotezee. Tukaondoka kwa kusikiliza maneno ya busara ya majirani.

So haya mambo yapo kuna watu wanajikutaka akili zimefyatuka na kuamua kuwabambikia watu msala wakiwa hawana ushahidi kamili.
 
Hata ukikaa Kuna watu wakifika hawaulizi, omba MUNGU tu
Ukikimbia unajenga mazingira ya utata kuaminiwa bora ubakie hapo hapo halafu uombe kusikilizwa kwasababu watu wanakwenda kufanya kosa kubwa sana hakuna anayekujua hapo na wala wewe haumjui mtu yoyote kutoa huyu anaekuitia mwizi.
 
Mkuu, Hilo zogo la raia unafikiri utasikilizwa?
Sasa hapo kuna mazingira ambayo yatashawishi raia kutokukusikiliza. Mfano umekimbia kipande umeenda kukamatiwa huko mbeleni. Au mtu kaanza kukuitia mwizi wewe unakimbia sababu unataka kuokoa maisha yako. Raia wakikukamata hawatakuwa na muda wa kukuhoji wataenda straight kukupa kichapo.

The best option ni kusimama na kuomba kusikilizana na uombe muende mlipotoka na kuhakikisha kuwa hapo hakuna wizi wala uhalifu bali kuna mtu ameamua kukukomesha. Kwenye mazingira ya haki ukweli huwa unaonekana wazi. Na mtu aliyepanga kukufanyia ubaya huwa anafeli akiambiwa afunguke wewe utasema ukweli wako yeye itabidi story yake atunge ili kutengeneza ukweli batili ambao utaumbuliwa na maswali ya msingi.
 
Back
Top Bottom