Ushuhuda: Wanaochomwa moto kwa kuiba siyo kweli wote ni wezi

Ushuhuda: Wanaochomwa moto kwa kuiba siyo kweli wote ni wezi

Jana limenitokea tukio la kusingiziwa utapeli, ilikuwa hivi:

Nilikuwa bar fulani mchana wa saa 10 karibu na ofisi kwetu napumzika, sasa nikaishiwa hela nikamwambia muhudumu naenda kuchukua 10000 nimeiacha ofisini me nikaondoka. Nikafika ofisini baada ya kama dakika 6 nipo kwa nje anakuja dogo muuza mayai ananiulizia wewe ndo ndege nikamjibu ndio, akauliza nimetapeliwa na mtu anafanana na wewe karibu na bar uliyokuwa unakunywa ameniambia nimpe 7000 anaingia ghetto kwake akirudi na 10000 atakula mayai ya 3000 na alikuwa amevaa shati la ki draft kama wewe.akaenda bar akaambiwa ndege ametoka sasa hivi akaelekezwa ofisini kwetu aje aone kama ni mimi.

Nilistajaabu sana nikahamaki una uhakika ni mimi nimekuibia? Dogo hana uhakika point yake ni kwamba mwizi wake ni mrefu na mweupe kama mimi na anaongea kichaga kama mimi. Kama masihara wakajaa bodaboda na watu wa mtaani kwetu na wakanigeuka mimi wakidai nimpe 7000 yake dogo ili nimalize huo mzozo na ukicheki mfukoni nina 10000 iliyobaki.

Nilibisha sana kwa kuwa mimi, sihusiki. Watu wakajaa ikawa aibu maana ni mazingira karibu na ofisi mambo yakawa mengi tukarudi mpaka bar kuuliza mpaka njia niliyopita watu kibao kama 15 hivi wananifuata baada ya mzozo mkubwa ushahidi ukaonekana kuwa sihusiki.

Nimewaza kumbe wako watu wanachomwa moto kwa kusingiziwa, usijichukulie sheria mkononi kama huna uhakika hujaibiwa acha wampige wao, we usimguse mtuhumiwa achana nae.
Ndege john masahibu yanakuandama tangu ulivyokuwaga Lumumba buku 7 2013, 14 and 15 ulikuwa unatushambuliaha sana bavicha humu. Machozi tuliyokuwa tunalia ukimshambulia mzee wetu kipenzi Lowassa yalitiririka mfano wa mto umbwe. Omba msamaha na uungame lazima utuombe msamaha lasivyo lasna
 
Pole sana mkuu,

Mwaka 2016 kuna dogo alimnunulia Godoro mpenzi wake, sasa siku moja dogo kampigia simu huyo babe wake huyo akawa hapatikani, licha ya kupiga Mara kadhaa hali ikawa ile ile, dogo akaona isiwe kesi, akatimba kwa mpenzi bila taarifa, ndipo alipomkuta bonge la bwana miraba minne, ambapo hangeweza hata kuanzisha ugomvi.

Njemba ikaondoka ikamwacha yeye dogo na demu wake,kama kupatana wapatane au waachane njemba haikutaka kujua,

Dogo akaona kuliko kuendelea na demu Malaya na mchafu, bora achukue godoro lake,
Akaingia inside akachomoa mattress yake tano kwa sita inches nane, akatoka nalo nje, ndipo ukawa mwisho wa maisha yake baada ya kupigiwa kelele moja tu.,

Mwiziiiiiiiiiio ananibia godoroooo,

Raia walikotoka na hasira zao, na ukizingatia dogo kakutwa na ushahidi, Godoro Dodoma ipo mgongoni?

Hili tukio lilinitesa kwa muda mrefu sana kulingana na nilivyomjua yule dogo, tuliheshimiana, aliniita Faza , alinikubali na nilimkubali kinomanoma, yaani Kuna wale madogo hata ukimtuma kitu hakatai kutokana na mnavyoheshimiana, nililia sana, ama kweli Dunia haina huruma.
ifike hatua iwe ni jino kwa jino,yaani mi ni bora nivunje chungu
 
Hiyo cha mtoto unampa demu lift añafika anapokwenda unasimama ashuke anakwambia mlipe pesa zake kwa uchi aliyokuuzia usiku kucha, hapo ndio utajuwa maharage ni mboga au kitoweo, halafu RAIA wamejaa pembeni wanawazoom tu.

sitoi lift hata kidogo. Maeneo ya mwenge kipindi cha nyuma kuna afisa fulani roho yake nzuri ilikuja kumtokea ili ilibidi kumpa milioni kipindi hiko.tena kavizia sehemu ya kumchafua aliposhushwa
 
Asee hii ya kutaka kumpiga mtu kisa eti mwizi au vipi Kuna siku nimeshuhudia ubabe wa kutisha sana.
Bwana wee Kuna bodaboda mmoja pale mabibo sokoni alimgonga dogo mmja kwa pikipiki mitaa ya kupita pale NIT . Baada ya kukimbia Kuna watu walimuona wakamsevu kichwani.. ah mbona tunamjua Yule! Anapaki mabibo sokoni. Basi wakatoka humo watu mamia wanamsaka jamaa. Ghafla wanamuona . Wana mawe, wengine visu na mitarimbo wakataka kumdandia wapige waue. Ghafla akatokea jamaa mmoja mbavu hivi akawambiaje ujue .. dogo njoo Hapa ole wake arushe mtu hata jiwe hapa. Huyo dogo aliyegongwa tutashughulikia tatizo lake.
Ghafla watu wakasambaratika. Nilishangaa ujue..
Mwisho.

Mitaa ya mabibo,tandale,manzese,mburahati na magomeni kuna mwenyeketi wa wahuni. kama unafahamiana nao ni rahisi kukuokoa
 
Pole sana mkuu,

Mwaka 2016 kuna dogo alimnunulia Godoro mpenzi wake, sasa siku moja dogo kampigia simu huyo babe wake huyo akawa hapatikani, licha ya kupiga Mara kadhaa hali ikawa ile ile, dogo akaona isiwe kesi, akatimba kwa mpenzi bila taarifa, ndipo alipomkuta bonge la bwana miraba minne, ambapo hangeweza hata kuanzisha ugomvi.

Njemba ikaondoka ikamwacha yeye dogo na demu wake,kama kupatana wapatane au waachane njemba haikutaka kujua,

Dogo akaona kuliko kuendelea na demu Malaya na mchafu, bora achukue godoro lake,
Akaingia inside akachomoa mattress yake tano kwa sita inches nane, akatoka nalo nje, ndipo ukawa mwisho wa maisha yake baada ya kupigiwa kelele moja tu.,

Mwiziiiiiiiiiio ananibia godoroooo,

Raia walikotoka na hasira zao, na ukizingatia dogo kakutwa na ushahidi, Godoro Dodoma ipo mgongoni?

Hili tukio lilinitesa kwa muda mrefu sana kulingana na nilivyomjua yule dogo, tuliheshimiana, aliniita Faza , alinikubali na nilimkubali kinomanoma, yaani Kuna wale madogo hata ukimtuma kitu hakatai kutokana na mnavyoheshimiana, nililia sana, ama kweli Dunia haina huruma.
Mtu akimfanyia hivi ndgu yangu na mimi namuua.
Siwezi kumuacha hai.
 
Hao wanaopiga wezi mpaka kuwachoma moto ni hasira za kuibiwa au ni hulka yao kupenda kuua watu ama kuona watu wakiteseka na kipigo walichowapa!?
 
Back
Top Bottom