Pamoja na yote, wakuu nashauri vitu viwili, cha kwanza tuangalie namna tunajiweka weka. Yani mavazi yetu, mtindo wa nywele mpaka maongezi. Na pili tujiamini vya kutosha, hata linapotokea tatizo na raia wanaangalia reaction yako baada ya kuitwa mwizi.
Sisemi ambao wanajiweka kiheshima na kujiamini hawapigwi kwa kelele za mwizi, bali asilimia kubwa ya wanaouwawa ukiwaona hata wewe unapata wasiwasi, unakuta mtu amenyoa kihuni, amevaa manguo yamechanika kwamba ndio fasheni na kibaya zaidi hajiamini, akiitiwa mwizi anakimbia akidhani atawazidi spidi raia 500 wenye ushirikiano.
Hata mtoa mada naamini kwa sehemu kubwa hivi viwili ndivyo vimemuokoa, angekuwa amevaa hovyo hovyo na hajiamini hata muda wa kumsikiliza watu wasingempa, wangeshamaliza kazi.