Ushuhuda: Wanaochomwa moto kwa kuiba siyo kweli wote ni wezi

True ni nadra sana watu waanze kukurukia na kukupiga kama mazingira hayaruhusu kufanya hivyo. Na ni muhimu pia kuwa makini na mazingira ya kwenda kuna sehemu unaenda hata usalama wako mwenyewe unaona upo matatani sasa ukiitiwa mwizi na hakuna mtu anayekujua huko si ni rahisi kupatwa na shida.
 
Speaking from experience, chance ya kusikilizwa ni 10% out of 100%.

Yaani ushakua tagged ni mwizi then usikilizwe? wakati jamaa wanazozana huyu mwizi au sio mwizi anatokea jamaa ambaye hata hajui mjadala umefikia wapi anakupiga na shoka la kichwa, unapotua chini unasindikizwa na tofali, Mara mtu kakutia mpini wa jembe kichwani! hapo kutakua na kikao tena?
 
Ungemuachia tu hiyo Msimbazi aka Ngada FC dogo ajinome.
 
Dah yaani leo ningefika kwako ningekuta turubai? Wallah ningewahi mochwari ya Mwananyamala kukuhifadhi vema! Pole sana
 
Hiyo cha mtoto unampa demu lift añafika anapokwenda unasimama ashuke anakwambia mlipe pesa zake kwa uchi aliyokuuzia usiku kucha, hapo ndio utajuwa maharage ni mboga au kitoweo, halafu RAIA wamejaa pembeni wanawazoom tu.
 
Tena Sasa nimegundua hivi vishikaji vya kuvinunilia smart, wengi ni vinafki na waongo waongo sana na ndiyo hai kutwa vinashinda bar huku mfukoni havina kitu!
 
Hiyo cha mtoto unampa demu lift añafika anapokwenda unasimama ashuke anakwambia mlipe pesa zake kwa uchi aliyokuuzia usiku kucha, hapo ndio utajuwa maharage ni mboga au kitoweo, halafu RAIA wamejaa pembeni wanawazoom tu.
Alafu wanapenda uwashushe karibu na boda boda naunapomshusha lazima Kuna boda anamjua utajuta!
Yaaan kwa dar kumuamini mtu usiyefahamiana naye ni risk sana.
 
Muda mwingine hao madogo wao ndio wezi.. Na wanajua kabisa kuepusha zogo na kwa usalama wako utatoa hela yaishe.

15 years old si ndio panya road hao.

Pole sana chief.
 
Nini kifanyike kupata suluhu ya hili tatizo?
Wahusika wanaojichukuliwa sheria mkononi wakamatwe na wafungwe maisha na Habari ziwafikie wote wenye tabia hiyo

Unakuta muuwaji yeye mwenyewe mwizi
Asilimia kubwa ya watu huko ni waizi halafu wanajifanya wema
Mwema unaua
 
Punguza ulevi mkuu...toka umepata hiyo ajira umekuwa chapombe sana...naona unasahau ulipotoka
 
Wanaochoma moto watuhumiwa wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kujichukulia maamuzi kuchoma watuhumiwa bila kuwafikisha mahakamani. Hao nao ni wahalifu washughulikiwe kisheria
Tatizo serikali yenyewe ndio hio wanaona kuwa jambazi lingine limeuwawa kumbe wengi wanasingiziwa
Unakuta mtu kaiba karanga au kuku wanamchoma moto
 
Kaka unawajua wanawake? Huo muda wa kuongea kwa amani hautakuwepo. Yaani kila utakapotaka kuongea ukweli, na yeye ili kufunika madhambi yake anakuwa anapiga keleke kama kachanganyikiwa "mwiziii"

Wengi wanakufa kwa staili hiyo kwa sababu nafasi ya kujitetea inaingiliwa na mwanamke.
 
Pole sana Mkuu, bora wewe kisa chako ni cha mazingira ya maisha ya kawaida! Nimeshuhudia kwa macho yangu mawili hivi watu wawili wakifa kwa kupigwa na kuchomwa moto kwa kuitiwa wezi na wapenzi wao baada ya kuzinguana..
Unachokisema ni kweli kabisaa, kijichi huku wiki iliopita saa moja saa mbili jamaa mmoja braza men baunsa baunsa kaitiwa mwizi, watu fasta makofi yakaanza Bahati akatokea mtu kuanza kuhoji kaiba nn?? kimyaa ndo jamaa anajitetea ana mgogoro na demu wake Ss huyoo mdada kampigia kelele ya mwizi, ajabu Ss Kumbe yule mdada yupo hapo hapo kwenye kundi la kumshambulia jamaa, mdada kuulizwa anauma uma midomo tuu, jamaa kwa hasira akiwa analia alimtwanga huyoo demu wake kisha akapandishwa bodaboda aondoke eneo lilee
Umati ukabaki na yule maluuuni bi dada
 
Kigogo Cha wote natembea nakutana na mtiti wa watu wanatokea kama kichochoroni ikabidi nihamaki!


Ghafla namuona jamaa kakabwa shingo nyuma Kuna mtiti wa watu wakimsindikiza huku akila mimbata na mitama Hadi kwenye nyumba Fulani hivi.


Kumbe yule jamaa ni muuza sandals Sasa yule machinga katika harakati zake Kuna dada kwenye Moja ya nyumba alimuita akihitaji kuona au kununua sandals yule dada baada ya kuangalia sandals na kushindwana yule machinga ikabidi aondoke Sasa yule dada kwa mawenge ikabidi ajisachi simu yake haioni hapohapo akaanza kumpigia kelele za mwizi yule machinga ndipo watu walipoanza kumkimbiza na kumkamata bahati nzuri Kuna wenye busara walisema twendeni nae kwa aliyeibiwa tupate uhakika lkn huku akisindikizwa na mambata


Kufika kwenye Ile nyumba simu inapigwa inakutwa ipo ukumbini daah na ilikuwa chipuchupu achomwe moto Dogo wa watu machinga ..aliishia kulia na kulalamika tu
 
Asee hii ya kutaka kumpiga mtu kisa eti mwizi au vipi Kuna siku nimeshuhudia ubabe wa kutisha sana.
Bwana wee Kuna bodaboda mmoja pale mabibo sokoni alimgonga dogo mmja kwa pikipiki mitaa ya kupita pale NIT . Baada ya kukimbia Kuna watu walimuona wakamsevu kichwani.. ah mbona tunamjua Yule! Anapaki mabibo sokoni. Basi wakatoka humo watu mamia wanamsaka jamaa. Ghafla wanamuona . Wana mawe, wengine visu na mitarimbo wakataka kumdandia wapige waue. Ghafla akatokea jamaa mmoja mbavu hivi akawambiaje ujue .. dogo njoo Hapa ole wake arushe mtu hata jiwe hapa. Huyo dogo aliyegongwa tutashughulikia tatizo lake.
Ghafla watu wakasambaratika. Nilishangaa ujue..
Mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…