#COVID19 Ushuhuda wangu kuhusu janga la COVID-19

Ilikuchukua muda gani kupona? Ninapitia hii hali tangu Jumatatu wiki iliyopita.
 
Ilikuchukua muda gani kupona? Ninapitia hii hali tangu Jumatatu wiki iliyopita.
Hadi harufu irudi inaweza kuchukua angalau wiki mbili, la muhimu ni kupiga nyungu angalau mara tatu kwa siku....kidogo tu kama robo kikombe cha chai, unaweza pia kutumia hizi dawa za vidonge vya mafua au zile za maji.....kama unaenda job inaweza kuwa shida kidogo, mimi kipindi hicho ndo nilikuwa nimeanza likizo, sikuwa na mikiki mikiki ya kwenda job........
 
Asante sana mkuu
 
Nyungu niliyotumia ina mchanganyiko ufuatao; vitunguu swaumu angalau 4, kitunguu maji 1, tangawizi vipande 4 ukubwa wa dole gumba, pilipili unaweza kutumia hata zile za njano wanaziita mwendikasi 4, limao 2. Saga huo mchanganyiko kwenye blender, halafu chemsha upate angalau lita 1. Ukipoa unachuja na chujio tayari unapata nyungu yako, na unaweza kuhifadhi kwenye friji ukawa unatumia kidogo kidogo.....
 
Hivi mnajua complication zinaletwa na corona? Ungekuwa unajua usingerahisha mambo namna hii. Ni hivi: Mtu anaweza kutumia ''tiba'' uliandika na akapona. Lakini ukweli ni kuwa siyo hiyo ''dawa'' imemponya bali hata kama asingetumia angepona. Hii ni kwa sababu wengi ya wanaougua korona hupona hata bila dawa.
 
Tatizo kubwa la Tanzania ni kuwa hawakutoa mwongozo kuhusu kukabiliana na corona. Wewe ulipougua ulitakiwa kwenda hospital upimwe, na kama una corona na hauumwi sana urudi nyumbani mpaka utakapopona. Wataam wanasema kama uliugua na kupona basi unakuwa umebaki na kinga na hata chanjo kuna muda unaweza kukaa bila kuchanja. Hata cheti cha kuonyesha ulishaugua na ukapona kinatambulika kama cheti cha mtu aliyechanja nchi nyingi.
 
Nakuhakikishia siyo nyungu iliyokuponyesha. Hata ungekukaa bila nyungu ungepona. Corona ni ugonjwa ambao ukikukalia vibaya, una complication mbaya sana kwenye viungo vingine vya mwili.
 
Nakuhakikishia siyo nyungu iliyokuponyesha. Hata ungekukaa bila nyungu ungepona. Corona ni ugonjwa ambao ukikukalia vibaya, una complication mbaya sana kwenye viungo vingine vya mwili.
Point yako hasa ni nini?
 
Nakuhakikishia siyo nyungu iliyokuponyesha. Hata ungekukaa bila nyungu ungepona. Corona ni ugonjwa ambao ukikukalia vibaya, una complication mbaya sana kwenye viungo vingine vya mwili.
Pathogenesis ya korona, namna inavyoweza ku-induce immunity na resistance ni mambo ambayo hayajaeleweka kwa uwazi sana.....mwanzoni ilifikiriwa kwamba korona is primarily a respiratory disease, lakini baadaye ikaja kugundulika kwamba inaweza kuathiri mifumo mingine, a multi-systemic disease.
 
Ndiyo maana nasema nyungu ni ujinga kama ujinga mwingine tu
 
Mtu anatoa ushuhuda wa nyungu mwingine anapinga nyungu. Kundi linalopinga nyungu mnaweza kuwa hatarini kuliko wanaopiga nyungu na hawajachanjwa
 
Daah, hongera Sana mkuu kwa kupona na kutushirikisha sote, Tuzidi kupambana na kuchukua tahadhari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…