SUASO
JF-Expert Member
- Oct 19, 2017
- 770
- 1,192
Habari ndugu zangu wana Tanganyika na Zanzibar!
Poleni kwa magumu tunayopitia, pia hongereni kwa zawadi ya uhai!
Najua humu JF familia kubwa tunaweza shirikishana Mambo mengi, leo naomba tushirikishane kuhusu Corona.
Wapo waliougua na kufariki( R.I.P), wapo waliougua na kupona, wapo waliouguza ndugu, jamaa, rafiki wakafariki Lakini wapo waliouguza na mgonjwa akapona,
Kwa phase zote 3, wimbi la 1, 2 Hadi hili la 3.
Naomba tujaribu kushirikishana uhalisia, ushuhuda wa corona ktk muktadha niliojaribu kuelezea hapo juu.
Kwangu Mimi ninao ushuhuda 2.
MOSI! Katika wimbi la kwanza tulimpoteza jirani yetu, yule Mzee ni mstaafu wa Serikali, alikuwa anaafya njema tu, alikuwa anapenda kujumuika jioni kwenye Bar fulani kupata kinywaji na kucheza Draft, corona ilivyoanza mzee akasitisha kuhudhulia Bar
Lakini baada ya muda km siku 3 akaanza kuhisi kuumwa, ikaamua aondoke kwenda Dom, kufika huko Hali ikawa mbaya zaidi, kalazwa na kupewa mtungi wa gesi.
Kabla ya kifo siku moja alikuwa vizuri kidogo na aliweza kuongea na simu, Lakini Hali ikabadilika ghafla na kupelekea kifo,
Ilikuwa majonzi Sana.
PILI!! Hii Ni wimbi hili la tatu, wiki hii ktk kundi letu la WhatsApp kuna memba moja akatuambia tumuombee maana changamoto ya upumuaji imemkabili.
Tukachukulia kawaida, jana imetoka taarifa yule memba umauti umemkuta,
Hakika Ni huzuni Sana, kifo kipo lakini kifo chakuona unakielekea kinauma zaidi.
Naomba tushirikishane/ ku-share matukio au ushuhuda kuhusu corona Kama umeugua au umeuguza vipi Hali ilikuaje?
Kupitia ushuhuda wako tunaweza saidia wengine pia, corona IPO ndugu zangu, na watu wanakufa!
Karibuni sana wakuu!

- Ulianza/ alianza kujisiakiaje Hadi kujua Ni corona?
- Changamoto zipi ulipitia Hadi kuanza kupata nafuu?
- Je, ulipata matibabu gani?
- Kama ulikuwa hospital vipi Hali kwa Wagonjwa wenzio?
- Je, ilikuchukua muda gani kupona na kurudi ktk Hali ya kawaida?