Ushuhuda wangu kuhusu RADI (my own testimonial)Nimeshuhudia RADI! Mara mbili, Ni kweli RADI ni kuku kabisa! Tena jogoo anaevutia haswa!

Kwamba mlibeba radi ,[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama sio kigoma huko basi rukwa au katavi

Huko Kuna radi hadi za jero za kununua.

Kuna kipindi cha mambo mseto radio one enzi zile Charles Hilary akikiendesha aliwa tupa stori ya mwewe kubebwa ngombe wa kilo 300 huko kati[emoji1787]
Ilikua 2004 kipindi hicho niko nasoma Kantalamba Sec. School
 
Mkuu kuna radi mbili ile ya asili ambayo shughuri yake tunaijua na hii ya wanchi kutengeneza ambayo mtengenezaji anaweza kuipa muonekano wowote anaotaka ata akitaka iwe na muonee wa binadamu anaweza tu sasa wewe umeona hii ya binadamu
 
Vitu vya asili vinasiri sana. Jogoo au ndege kutoa umeme mkubwa na ngurumo kubwa. Inashangaza sana.
Wacha niendelee kujifunza
 
Sayansi inaamini ni umeme wa asili,. na wewe unaamimi ni kuku mwekundu tena jogoo anayevutia.??
 
Duh "LY" yaani Last Year umetisha!!!
Nilitaka nimuulize,,,YAANI last year alikuwa darasa la Saba....?so Yuko form one kwa Sasa...ok ngoja nijadili mada....RADI HATA KULE KWETU SUMBAWANGA INAKUJA KWA MTINDO WA MANYUNYU MEPESI MEPESI IKIAMBATANA NA NGURUMO RASHARASHA..ILA KAMA HAIKUHUSU HAINAGA SHOBO NAWE
 
Nyinyi ndio mnaishushq hadhi jf,unajua fika unasimumilia/unashuhudia uonge na still unafanya hivyo,hivi jf mmeifanya fb?,eti tukakamata Radi
 
Simulizi ya kuku kuhusishwa na radi ni mara ya pili naisikia kwako, toka niliposimuliwa hivyo miaka mingi iliyopita.
 
Story hii aliwahi kunihadithia bibi, akasema miaka yao wakiwa wadogo radi zilikua zinapiga Sana kuliko sasa hiv, na muda mfupi kabla ya Radi kupiga walikua wanaona jogoo na baada ya radi anapotea. Nilimuuliza mbona siku hiz hatumuoni jogoo akasema hajui Ila miaka yao waliona mengi ya ajabu na yameenda yanapungua kila mwaka
 
Option 1: tuamini tu maneno yako sababu umeona

Option 2: huenda una hallucination na unaona vitu ambavyo havipo...

Nadhani option 2 ni more plausible

Kwahiyo unataka kusema kuwa yeye, marafiki zake, bibi yake pamoja na wanakijiji wengine walikuwa wana hallucinate kwa pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…