Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unajua kitu kinaitwa Power of Suggestion ?Kwahiyo unataka kusema kuwa yeye, marafiki zake, bibi yake pamoja na wanakijiji wengine walikuwa wana hallucinate kwa pamoja.
Option 1: tuamini tu maneno yako sababu umeona
Option 2: huenda una hallucination na unaona vitu ambavyo havipo...
Nadhani option 2 ni more plausible
🤣🤣 mimi pia kwa masimulizi ya watu waliopata kuona wanasema huonekana kuku mwekundu kabla ya radi kupiga.Naam,
Kumekuweko na speculation nyingi kuhusu RADI. Nyingi zikihusisha radi katika makundi mawili, ambayo ni radi kisayansi,kama umeme asilia na Radi kiimani. Wengi wakiihusisha na ushirikina.
Binafsi ziko katika upande wowote Kati ya hizo pande mbili hapo juu, bali naeleza kile nilichopata kukishuhudia mara mbili kwa macho yangu mawili, utotoni( adolescent age) na ukubwani kidogo nikiwa najitambua.
Nikiwa na yapata miaka kadhaa, tukiwa porini tunachunga ng'ombe tukiwa rika vijana wadogo watatu tuliona jogoo mzuri pembezoni na maeneo tuliyopo, alikuwa anaevutia tulimnyatia na tukamkamata jogoo alikuwa na kila kitu chekundu kuanzia mdomo,manyoya hadi miguu tukamfikisha nyumbani huku manyunyu ya mvua yakiendelea kuongezeka, tukamfungia jogoo jikoni na wengine wakiirudisha mifugo zizini.
Tukiwa tumefurahi na tukiendelea na michezo kwani kitoweo kimepatikana, tukamwambia bibi kuwa tumeokota kuku machungani na tumemfungia yumo jikoni. Bibi kwenda kuangalia! Lahaula! Alianza kupiga kelele za yowe kwa majirani, unajua umbali uliopo baina ya mji na mji. Aliendelea huku analia na kukimbiza huku na kule huku mvua ikiendelea kunyesha.
Baadhi ya watu waliendelea kujaa, na kutahamaki tukasikia ngurumo kubwa na miale ya radi iliipiga ile nyumba ambayo ndio huko tulipomfungia yule kuku. Wote tuliinama kwa yoga na baada ya mvua kukatika tukagundua kuwa yule kuku hakuwemo tena na alipotea ghafla baada ya Radi ile kutoweka, na haikuleta madhara makubwa sana.
Tukio la pili;-)
Nikiwa likizo last year Std Vii kama ilivyo kawaida nilimtembelea bibi na babu(R.I.P), katika mizunguko yetu ya hapa na pale, tulitenbelea mtoni kuogelea na kupiga stori mbili tatu na washkaji wa kunijibu, maana tulikuwa hatusomi pamoja tena,mimi nilikuwa nikija huku kwa ajili ya likizo tu.
Tukiwa tunaendelea kuogelea kea mbali kidogo niliona tukio kama lile lililotutokea miaka kadhaa nyuma na kufanya tupokee kichapo toka kwa babu, niliona jogoo wa dizaini ile ile! Mwekundu Tii! Akiwa pembeni ya mto akizamisha kichwa makini na kutoa mara kwa mara huku akipigapiga mabawa.
Mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio kwa woga hofu! Kwani nilihisi kinachokaribia kutokea na pembeni kulikuwako na vijana wadogo wanachunga.
Kwa hofu tulikuwa tukimuangalia yule jogoo anaevutia sana na wenzangu wote tukiwa tumetoka mtoni tuko pembeni,ghafla ulisikika muungurumo na mitetemo kikubwa+ miale kadhaa ya mianga(Radi) na pale pale ng'ombe watatu walipigwa na Radi pale pale na kufa!.on the spot!.
Haya nimeyashudia mwenyewe kwa macho yangu,nikiwa na akili timamu!
Sayansi inaamini ni umeme wa asilia, lakini napata ukakasi nikiunganisha nilichokishudia kwa macho,na sayansi ya kufundishwa. Ktka radi napata kuuona uhusika wa hivi vitu, MUNGU yupo(imani) maana nimeona kitu kwa macho halisi, na kikapotea.
Maswali ni mengi najiulizaga, yule jogoo kea nini hupotea! Baada ya Radi!? Anaeenda wapi!? Na kea nini sayansi inakataa ukweli kwamba Radi ni kuku!?
Hio Radi ilikuwa mwendo / kasi gani ? Slow Motion ?juu tulikuwa tumeket tuna kula vitu kunakamvua mvua kunamti tuu mkubwa ghafla radi hyo hapo inazunguka juyamti kama umeme.kulikuwa na masai akachomoka akashika majani makavu akapiga magoti akaanza kuongea ewe radi sisi atuna ubaya tunakunywa tu naomba uondoke .namaneno siyakumbuk ghafla radi hyo ikaenda kuangukia mbali kidogo tukaona moshi tu ..hapo sisi tumelala chini badae tunamuliza masai anasema nikawaida tu ashazoea huko kwao
Amna mkuu...niile radi ya mngurumo inaanza kama transforme inavoungua ndipo ibast..kama fataki xo ilikuwa inazunguka hapo juu kwamngurumo kabla masai hajaikemea ndoika lipukia sehem nyengineHio Radi ilikuwa mwendo / kasi gani ? Slow Motion ?
Sababu kinachoonekana ni waves ambazo ni light na Sauti (Sound) sasa kasi ya hivyo vitu mkuu kweli unapata muda wa kupiga magoti na kupiga nayo story...
Au labda haikuwa moja zilikuwa na washikaji zao ili aliyoipigia magoti sio ile iliyopiga pengine....
Tuishi humuMkuu kuna radi mbili ile ya asili ambayo shughuri yake tunaijua na hii ya wanchi kutengeneza ambayo mtengenezaji anaweza kuipa muonekano wowote anaotaka ata akitaka iwe na muonee wa binadamu anaweza tu sasa wewe umeona hii ya binadamu
Mimi wilaya ya roryaulipo shuhudia miujiza ni wapi huko? wilaya gani?
Hiyo hallucination ndio wawe nayo kijiji kizima.?Option 1: tuamini tu maneno yako sababu umeona
Option 2: huenda una hallucination na unaona vitu ambavyo havipo...
Nadhani option 2 ni more plausible
Kikubwa ni hallucinationOption 1: tuamini tu maneno yako sababu umeona
Option 2: huenda una hallucination na unaona vitu ambavyo havipo...
Nadhani option 2 ni more plausible
Science inatafsiri uumbaji kwa level za kibinadamu.The beyond universe hiyo. Ulimwengu mbadala ambao huitaji kuwa na macho yanayo qualify kuushuhudia.
Ila pia isikufanye upinge science procedure ambayo inasema radi ni umeme km ulivyo umeme mwingine na hutokea baada ya charges zilioko mawinguni kusuguana na radi hiyo ikipiga kitu sifa ya kwanza lazima ikiunguze kabisa maana ni moto mkubwa sana.