Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Naomba kujua ulisoma chuo gani?? au kipo mkoa gani, Ushuuda wako uwafikie wale wa kula tunda kimasihara
 
Mabaaria wa kula tunda kimasihara hii inawahusu siwaoni uku kabisa..mnaitajika viti vya mbele uku vipo wazi. yani Kiukweli mimi last time kupima ilikuwa 19/november 18 ila dah kuna rafu mbili nilizicheza af sielewi kbsa yani siku ya kupma tn itakuwaje. Ila Hongera dada Kwa ujasiri ulonao
 
ngoja waje na kuna yule aliyetuma nauli waje wapitie hapa
 
Duh!! Pole saa mpendwa, sina cha kukwambia sababu natumai ushaambiwa saana, wala sina cha kukushauri sababu ushapata ushauri wa kutosha, pia sina sababu ya kukupa maneno ya kukutia moyo sababu kwa maelezo yako na kitendo cha kuandika huu uzi hapa tayari hii hali ushaipokea na wew unajionea kitu cha kawaida, kikubwa tu nakushukuru kwa kushare nasi hapa hii habari, yaweza kuwa matumaini kwa wale wasiokuwa na matumaini waliokata tamaa kwenye janga kama hili ama kwenye misanga tofauti tofauti, ni funzo pia kwetu soote.
Natamani ungekuwa mshikaji wangu kwenye maisha ya kawaida nje na jf.

Nakushukuru na ubarikiwe
Kila la kheri bibie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…