Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Nimekwisha msamehe mkuu, na tunawasiliana nae vizuri tu na maisha yanasinga
Sasa kwanini hamkukaa mkafanya maisha pamoja?labda sijakuelewa main post naona umesema kitu kama mkewe alifariki au ni babu mtu mzima sana?

But vyovyote ilivyo nakupa pole sana kwa changamoto hii kubwa uliyokutana nayo ukiwa bado bint m'bichi kabisa.
 
Umejibu vizuri sana,ila iko kitaalamu zaidi na umefupisha sana maelezo yako as if unamjibu mtu ambaye ni professional kwenye hiyo fani ya utabibu...
Nikweli mkuu mimi si mzuri sana kwenye uandishi ila ataambulia kitu
 
Yaani mtu kakuambukiza kisha kakutafutia kazi ndiyo unamuona anakupenda sana? Mpenzi haupo serious.
 
Pole sana kijana! Uwe na moyo mkuu na wala usijali kwa kuwa kuumwa siyo kufa leo.Acha ngono kabisa,usiruhusu mawazo na ujitunze vizuri.Fahamu kinachoua watu haraka baada ya kupata tatizo hilo ni hofu,mawazo na kukata tamaa. La mwisho mrudie Mungu,mwambie akusamehe kwa uovu uliofanya harafu jikabdhi kwake.
Utaishi maisha mazuri sawa sawa na mtu ambaye hana tatizo hilo.
 
Asante, muwe makini tu huko uraiani kumechafuka sana na hali ya uchumi ilivyo mbaya maambukizi yataongezeka sana. Mjitahidi kama hamuwezi kuwa na mpenzi mmoja basi jitahidini mtumie mipira jamani
..............Sure!!!

Juzi nilisoma mahali Tanzania kwa siku moja kuna maambukizi mapya 200,just imagine kwa rate hiyo baada ya miaka mitano tutakuwa taifa la namna gani?

Inasikitisha sana.
 
Naona kumekucha. Yote kwa yote iwe kweli ama La.

Niseme tu huu uzi iwe chachu ya watu hasa members wa humu kukumbuka kwamba ukimwi upo sio watu wanatong*zana tu na siku ya kwanza kuonana breki ya kwanza wanakutana mahotelini na kwenye malodge kwenda kukwich*kwich* yaani hamna kupima na hata kutumia kinga hamna.

Ukimwi haupimwi kwa macho, upo na unaua na hasa sisi vijana yatupasa kuwa makini mnoo sababu kila unayemuona kwa nje kanawiri.
 
Priscallia, Napenda kufaham mtoa mada,mech hzo had inapelekea kuambukizwa kwa michubuko huwa zikoje,je ni kali sana zile za had kinawaka moto au za kawaida tuu
 
Back
Top Bottom