Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Kuna huu


 
Ahsante sana priscallia, uzi wako utawaamsha wengi waliokuwa kwenye dimbwi la usingizi wa ngono zembe. Binafsi, nakuombea sana kwa Mungu kwa kuwa na upendo wa dhati kuwakknga vijana wenzangu dhidi ya maambukizi ya VVU.

Pamoja na hayo, mimi binafs nimewahi kuwa na mahusiano na msichana humu JF ila bahati nzuri tulilima na ikaonekana wote ni negative mpaka tunaachana nilipima tena pamoja naye tulikuwa negative.

Na mpaka sasa Mungu amenikinga (maana binafs napenda kula peku peku na sio mtumiaji wa kinga vyema) lakini mpaka sasa nipo negative.
Na hitimisha kwa kusema, VIJANA WENZANGU UKIMWI UPO NA CONDOM ZINAZUIA MAAMBUKIZI YA VVU.
 
Sipati picha mabaharia waliopita na wewe na wanaona huu uzi wako kwenye hali gani sasa

Hali mbaya sana, kuna mwingine tayari ameshajianika huko. Tafuta uzi anaosema “anajutia kusoma uzi wa muathirika”
 
Hongera sana kwa ushujaa wako Priscallia

Ahsante pia kwa kutukumbusha mara nyingi wanaume tunadanganywa na maumbo yenu na kuendeshwa na hisia/tamaa za mwili.
 
hata sijui ini comment nini ila huu uzi umenifanya nipime leo
kumbe haya mambo yapo ee.
ice_2019-11-29-11-28-47-383.jpeg
 
Kondom hajawahi kuwa rafiki wakudumu. Utamtumia mara 1 au 2 na kuachana nae kabisa.

Kwangu mimi naona bora nikanunue demu baa au kwenye danguro nitachukua tahadhali za kutosha kuliko mademu wa mtaani tunaoamini ni watilivu.
 
safari moja miaka ya 2009/10 hivi nikiwa katika safari ya kikazi nikitokea mikoa ya kusini kuelekea mkoa mmoja wa kaskazini niliweka kituo dar es salaam muda wa kurejea zangu kusini baada ya kukamilisha shughuli zangu.

baada ya kukosa kiajabu ajabu totoz la kunipoza kaskazini sasa dar ikawa ni lazima nipozwe, nilipata nyama choma mbuzi na castle lager kadhaa sasa pale pub nilipata totoz na hapo siku ya pili alfajiri ilikuwa nianze safari nikitokea pale stand ubungo kuelekea mkoani.
kwa uchu niliokuwa nao nilihakikisha hanipotei, nilimdhibiti vema na nikamnunulia vinywaji na chakula.

muda wa kufunga pub nikatoka nae haraka haraka hadi guest house nilipofikia, zana nilikuwa nazo lakini nafikiri zile pombe.
Round ya kwanza ilienda fresh, sasa round ya pili nikahisi raha zimeongezeka nikamaliza sasa ndio nashtuka kondom ilipasuka... dah

niliingiwa na hofu kubwa sana, sikulala hadi asubuhi na mapema nikadamka na kumpa pesa yake.
kwa kweli nilisafiri nikiwa na mawazo tele ukizingatia nilikuwa bado single.
hii hofu ilichangiwa na ukweli kwamba ilikuwa mara ya pili kondom kupasuka nikiwa mitungi na sikuacha namaliza. hii mara ya pili nili'conclude ninao.

baada ya kuishi kwa muda hofu na mashaka tele nikaamua kupima. sasa nilivyokuja kupima na kubaini sina maambukizi ooooh God. nilibadilika sana, hadi sasa nimebadili life style nina familia na watoto wawili.

kwa ufupi sana lkn unapokuwa na mashaka na hali yako kiafya ni vema ukapime
 
Back
Top Bottom