Usiache kununua ardhi. Niliyojifunza Goba sikufanya makosa Madale

Usiache kununua ardhi. Niliyojifunza Goba sikufanya makosa Madale

2003 Nilipelekwa kibaha kuoneshwa ardhi pale picha ya ndege. Nikafika eneo husika ni robo kilometer kufika lami
Ile ardhi ilikuwa ekari moja na nusu kasoro.. Yule mzee alitaka 1M tena kwa instalments
Kwenye draw ya gari nilikuwa na na kama 1.2 haina kazi. Yule mzee akanisihi sana nisipaache pale mahali na kama nina laki 2 nimpe kwanza
Kuna kasauti kakaniambia moyoni achana naye huyo anakupanga kwani utakuja kuishi lini huku kwa ujinga wa ujana nikakasikiliza kale kasauti
Nikamwambia mzee Leo sina hela ila nakupa hii 20,000 ya usumbufu.. Akaipokea kisha akasema asante lakini ukiweza ongeza 80,000 itimie laki nikuwekee hii ardhi utanukumbuka. Nikagoma
Tukaondoka na mtu niliyekuja naye kufika Kibaha container bar tukapiga ugali samaki wa nguvu
Tukaondoka mpaka Mbezi kufika pale tukaanza kupiga maji.. Tukaondoka kwenye saa 9 mchana
Kufika saa 11 jioni tuko Mama land bar External .. Bata likaendelea
Saa tatu usiku tukanyanyua kuelekea Moshi Bar Goms! Hiyo haikuwa na come back
Siku iliyofuata kuangalia balance nina kama laki7 na ushee
Mwaka 2016 nikapata kazi Kibaha na kuamua sasa kujiwekeza baada ya ujinga kunitoka, nikasema niende kwa yule mzee
Kufika pale nikakuta palishauzwa na kukatwa viwanja vya 20 kwa 20
Kilikuwa kimebaki kimoja tu bondeni na bei ilikuwa million 3 haipungui hata mia😂
Mlandizi pale njia ile unatokea bagamoyo nimeshuhudia m2 ilinunua eneo 2008, sahivi lile eneo estimations zake linakarbia m300 na ushee maana pembeni majirani wameuza kwa wachina na wawekezaji wengine wamejenga viwandaa....unachosema wala sio uongo kaka mshana.....haya maeneo ya kimkakati sanaa na hivi njia ya bandari ya bagamoyo ndio hii hii ni LULU mno hii ardhi kwakwelii💪🏿
 
Nilipita pande hizo niliona lami inajengwa, nikasema Msumi itakuwa ya moto, na hiyo lami itapitia Mbopo eneo ambalo watu walilichukulia poa sana then lami itakuja kuungwa pale Madale mwisho

Ina maana sasa hivi ardhi ya Mbopo nayo inaenda kupanda thamani
kuna lami inajengwa kigamboni manispaa kuanzia mwasonga kwenda tundwi songani hadi buyuni hii ikikamilika viwanja havitashikika kwa bei.
 
Miaka ya 2005-2008 nilikuwa napita sana barabara ya Goba-Makongo Juu hadi Chuo. Kipindi hicho lile daraja la Goba kwenda Makongo Juu halijajengwa.

Plus ujana ulikuwa bado mwingi nikapuuzia tu eneo hilo. Itoshe tu kusema yalikuwa mapori, viwanja hata kuanzia 1mln kushuka chini ulikuwa unapata vikubwa tu. Goba kalikuwa kakijiji leo nikipita huwa naumia sana.

Ni kweli hata leo unaweza kupata maeneo hapo Goba lakini kwa gharama kubwa sana. Eneo ambalo hasa nyumba zilikuwa zimejengwa ni Makongo juu na wengi inaonekana walipachukulia poa sana Goba ila baada ya barabara ya lami tu kupita na madaraja kujengwa daaah maeneo yakawa hayashikiki.

Kuanzia miaka ya 2010s nilipoanza ujenzi Salasala nikawa napitapita sana njia ya Madale kukiwa pori kipindi hicho barabara ya vumbi wakati wa masika hupiti na gari hilo tope. Hapo ndipo nikasema sifanyi tena makosa ya Goba, nikajichanganya na madalali na wenyeji nikapata viwanja vikubwa hapo Madale kukiwa bado pori.

Sasa hivi lami imepita Madale, leo ukifika Madale viwanja vimepanda bei sana na inaenda kuwa kama Goba. Ukweli ni kwamba mpaka leo sijaheal kwa yaliyonikuta Goba.

Hapo Dar na Pwani usiseme sehemu mbali, mbali kutokea wapi? Na sio tu Dar na Pwani popote pale nunua ardhi ili mradi inafaa kwa makazi au kilimo.

Usiseme hakujachangamka nunua tu, wewe ni miongoni mwa watakaopachangamsha. Twenzetu Mabwepande.
​
Mabwepande kias gan
 
Back
Top Bottom