Usiache kununua ardhi. Niliyojifunza Goba sikufanya makosa Madale

Ardhi inapanda thamani kila siku.
Kiwanja nilichonunua million 10 kwa masikitiko leo kuna mtu anakitaka ana million 150

Kingine lilikuwa shamba mkoani nilinunua barabarani million 5. Mwaka jana napigiwa sehemu kuna mtu anakitaka ajenge parking na petrol station ana million 80.
Uza sasa si ndo uwekezaji umejibu au hautaki kuuza?
 
Miaka ya 2005-2008 nilikuwa napita sana barabara ya Goba-Makongo Juu hadi Chuo. Kipindi hicho lile daraja la Goba kwenda Makongo Juu halijajengwa.

Plus ujana ulikuwa bado mwingi nikapuuzia tu eneo hilo. Itoshe tu kusema yalikuwa mapori, viwanja hata kuanzia 1mln kushuka chini ulikuwa unapata vikubwa tu. Goba kalikuwa kakijiji leo nikipita huwa naumia sana.

Ni kweli hata leo unaweza kupata maeneo hapo Goba lakini kwa gharama kubwa sana. Eneo ambalo hasa nyumba zilikuwa zimejengwa ni Makongo juu na wengi inaonekana walipachukulia poa sana Goba ila baada ya barabara ya lami tu kupita na madaraja kujengwa daaah maeneo yakawa hayashikiki.

Kuanzia miaka ya 2010s nilipoanza ujenzi Salasala nikawa napitapita sana njia ya Madale kukiwa pori kipindi hicho barabara ya vumbi wakati wa masika hupiti na gari hilo tope. Hapo ndipo nikasema sifanyi tena makosa ya Goba, nikajichanganya na madalali na wenyeji nikapata viwanja vikubwa hapo Madale kukiwa bado pori.

Sasa hivi lami imepita Madale, leo ukifika Madale viwanja vimepanda bei sana na inaenda kuwa kama Goba. Ukweli ni kwamba mpaka leo sijaheal kwa yaliyonikuta Goba.

Hapo Dar na Pwani usiseme sehemu mbali, mbali kutokea wapi? Na sio tu Dar na Pwani popote pale nunua ardhi ili mradi inafaa kwa makazi au kilimo.

Usiseme hakujachangamka nunua tu, wewe ni miongoni mwa watakaopachangamsha. Twenzetu Mabwepande.
​
Kweli mkuu!Ardhi ni biashara isiyoshuka bei , Labda kama Ina majanga asili kama, Volcano,Mafuriko nk.
 
2003 Nilipelekwa kibaha kuoneshwa ardhi pale picha ya ndege. Nikafika eneo husika ni robo kilometer kufika lami
Ile ardhi ilikuwa ekari moja na nusu kasoro.. Yule mzee alitaka 1M tena kwa instalments
Kwenye draw ya gari nilikuwa na na kama 1.2 haina kazi. Yule mzee akanisihi sana nisipaache pale mahali na kama nina laki 2 nimpe kwanza
Kuna kasauti kakaniambia moyoni achana naye huyo anakupanga kwani utakuja kuishi lini huku kwa ujinga wa ujana nikakasikiliza kale kasauti
Nikamwambia mzee Leo sina hela ila nakupa hii 20,000 ya usumbufu.. Akaipokea kisha akasema asante lakini ukiweza ongeza 80,000 itimie laki nikuwekee hii ardhi utanukumbuka. Nikagoma
Tukaondoka na mtu niliyekuja naye kufika Kibaha container bar tukapiga ugali samaki wa nguvu
Tukaondoka mpaka Mbezi kufika pale tukaanza kupiga maji.. Tukaondoka kwenye saa 9 mchana
Kufika saa 11 jioni tuko Mama land bar External .. Bata likaendelea
Saa tatu usiku tukanyanyua kuelekea Moshi Bar Goms! Hiyo haikuwa na come back
Siku iliyofuata kuangalia balance nina kama laki7 na ushee
Mwaka 2016 nikapata kazi Kibaha na kuamua sasa kujiwekeza baada ya ujinga kunitoka, nikasema niende kwa yule mzee
Kufika pale nikakuta palishauzwa na kukatwa viwanja vya 20 kwa 20
Kilikuwa kimebaki kimoja tu bondeni na bei ilikuwa million 3 haipungui hata mia😂
Tuna la kujifunza!
 
Bro umeongea Ukwel mtupu.

Shida vijana ambao wanatakiwa kuwekeza (20's - 30's) bado wako Sinza , kinondoni kijitonyama na hawawez kujua haya.
Wanawaza Mamillion meng. Na kuyapata ndio mtihani.

Maeneo kama Mabwepande, mbopo, msumi, makabe, Kibamba na kule kibwegere . Ukiwa na 6 Mill unapata kiwanja kikubwa wastan wa 20*20.

Kwahiyo Ukiwa na 10+ Mill unapata kaeneo kakubwa tu kutosha kujenga nyumba.

Kijana wakat unasubiria Mill 100 za kununua kiwanja prime areas. Hebu anza na kuwekeza na kiwanja sehem za mbali.
You never know. Unaweza usipate hizo hela ukazeekea nyumba za kupanga.
Hii ni kweli? Mbona nimetafuta sana maeneo hayo nakutana na bei kali?
 
Miaka ya 2005-2008 nilikuwa napita sana barabara ya Goba-Makongo Juu hadi Chuo. Kipindi hicho lile daraja la Goba kwenda Makongo Juu halijajengwa.

Plus ujana ulikuwa bado mwingi nikapuuzia tu eneo hilo. Itoshe tu kusema yalikuwa mapori, viwanja hata kuanzia 1mln kushuka chini ulikuwa unapata vikubwa tu. Goba kalikuwa kakijiji leo nikipita huwa naumia sana.

Ni kweli hata leo unaweza kupata maeneo hapo Goba lakini kwa gharama kubwa sana. Eneo ambalo hasa nyumba zilikuwa zimejengwa ni Makongo juu na wengi inaonekana walipachukulia poa sana Goba ila baada ya barabara ya lami tu kupita na madaraja kujengwa daaah maeneo yakawa hayashikiki.

Kuanzia miaka ya 2010s nilipoanza ujenzi Salasala nikawa napitapita sana njia ya Madale kukiwa pori kipindi hicho barabara ya vumbi wakati wa masika hupiti na gari hilo tope. Hapo ndipo nikasema sifanyi tena makosa ya Goba, nikajichanganya na madalali na wenyeji nikapata viwanja vikubwa hapo Madale kukiwa bado pori.

Sasa hivi lami imepita Madale, leo ukifika Madale viwanja vimepanda bei sana na inaenda kuwa kama Goba. Ukweli ni kwamba mpaka leo sijaheal kwa yaliyonikuta Goba.

Hapo Dar na Pwani usiseme sehemu mbali, mbali kutokea wapi? Na sio tu Dar na Pwani popote pale nunua ardhi ili mradi inafaa kwa makazi au kilimo.

Usiseme hakujachangamka nunua tu, wewe ni miongoni mwa watakaopachangamsha. Twenzetu Mabwepande.
mie nipo kusini ya Dar, nimechimba kisima cha 4m, maji safii, umeme upo. Maisha yañaenda
 
Tatizo ni serikali rushwa na mipango kimo cha mbilikimo
2003 Nilipelekwa kibaha kuoneshwa ardhi pale picha ya ndege. Nikafika eneo husika ni robo kilometer kufika lami
Ile ardhi ilikuwa ekari moja na nusu kasoro.. Yule mzee alitaka 1M tena kwa instalments
Kwenye draw ya gari nilikuwa na na kama 1.2 haina kazi. Yule mzee akanisihi sana nisipaache pale mahali na kama nina laki 2 nimpe kwanza
Kuna kasauti kakaniambia moyoni achana naye huyo anakupanga kwani utakuja kuishi lini huku kwa ujinga wa ujana nikakasikiliza kale kasauti
Nikamwambia mzee Leo sina hela ila nakupa hii 20,000 ya usumbufu.. Akaipokea kisha akasema asante lakini ukiweza ongeza 80,000 itimie laki nikuwekee hii ardhi utanukumbuka. Nikagoma
Tukaondoka na mtu niliyekuja naye kufika Kibaha container bar tukapiga ugali samaki wa nguvu
Tukaondoka mpaka Mbezi kufika pale tukaanza kupiga maji.. Tukaondoka kwenye saa 9 mchana
Kufika saa 11 jioni tuko Mama land bar External .. Bata likaendelea
Saa tatu usiku tukanyanyua kuelekea Moshi Bar Goms! Hiyo haikuwa na come back
Siku iliyofuata kuangalia balance nina kama laki7 na ushee
Mwaka 2016 nikapata kazi Kibaha na kuamua sasa kujiwekeza baada ya ujinga kunitoka, nikasema niende kwa yule mzee
Kufika pale nikakuta palishauzwa na kukatwa viwanja vya 20 kwa 20
Kilikuwa kimebaki kimoja tu bondeni na bei ilikuwa million 3 haipungui hata mia😂
Broo umeongea kwa uchungu sana
 
Hata mia haitokii😂😂😂
 
Miaka ya 2005-2008 nilikuwa napita sana barabara ya Goba-Makongo Juu hadi Chuo. Kipindi hicho lile daraja la Goba kwenda Makongo Juu halijajengwa.

Plus ujana ulikuwa bado mwingi nikapuuzia tu eneo hilo. Itoshe tu kusema yalikuwa mapori, viwanja hata kuanzia 1mln kushuka chini ulikuwa unapata vikubwa tu. Goba kalikuwa kakijiji leo nikipita huwa naumia sana.

Ni kweli hata leo unaweza kupata maeneo hapo Goba lakini kwa gharama kubwa sana. Eneo ambalo hasa nyumba zilikuwa zimejengwa ni Makongo juu na wengi inaonekana walipachukulia poa sana Goba ila baada ya barabara ya lami tu kupita na madaraja kujengwa daaah maeneo yakawa hayashikiki.

Kuanzia miaka ya 2010s nilipoanza ujenzi Salasala nikawa napitapita sana njia ya Madale kukiwa pori kipindi hicho barabara ya vumbi wakati wa masika hupiti na gari hilo tope. Hapo ndipo nikasema sifanyi tena makosa ya Goba, nikajichanganya na madalali na wenyeji nikapata viwanja vikubwa hapo Madale kukiwa bado pori.

Sasa hivi lami imepita Madale, leo ukifika Madale viwanja vimepanda bei sana na inaenda kuwa kama Goba. Ukweli ni kwamba mpaka leo sijaheal kwa yaliyonikuta Goba.

Hapo Dar na Pwani usiseme sehemu mbali, mbali kutokea wapi? Na sio tu Dar na Pwani popote pale nunua ardhi ili mradi inafaa kwa makazi au kilimo.

Usiseme hakujachangamka nunua tu, wewe ni miongoni mwa watakaopachangamsha. Twenzetu Mabwepande.
​
Mkuu hayo pia yalinikuta wakati naishi Boko. Maeneo ya Mabwepande nilikuwa nayaona porini japo nilibahatika kunasa kaeneo kadogo. Nikajifunza kutokana na Makosa.... Hivi sasa najitesea zangu tu mitaa ya Mapinga.
 
Hilo ndilo la msingi kujifunza kutokana na makosa. Nakuelewa sana unaposema Mapinga umecheza kaka
 
Kweli mkuu. Waliokuwa wananicheka nakimbilia maporini ndio haohao wanataka niwauzie kasehemu... Nami bado sijawazia hilo. Nasubiria bei iendelee kupaa ili Mungu akijaalia nifaidi uzee wangu kitajiri...
 
Back
Top Bottom