Usiamini unamjua mtu kupitia mtandaoni kama haujawahi kukutana naye uso kwa uso

Usiamini unamjua mtu kupitia mtandaoni kama haujawahi kukutana naye uso kwa uso

Unataka kutuambiaje sie ambao kwa namna moja au nyingine tunakula tam za mitandaoni, tunadatishwa na comments, ucheshi then tunatengeneza taswira zetu. Kinachofata sasa ni kuonana machinjioni na kuwekana. Its so simple.
 
Nakumbuka kuna grp moja la whatsapp huku na huku kuna Kidada kikaanza kuniletea dharau sana.. mie nikamwambia tu kuna siku isiyo na jina tutakutana..

Akacheeka sana na maneno ya shombo.. basi ikaisha hivyo.

Yule Mtu, nafkiri mpk anazama chini ya hii ardhi hatokuja kudharau hata kichaa aliye jalalani.

nifupishe tu story kwa kumaliza hivi.

Usimdharau mtu usiyemjua/Mfahamu.
Hata kama unamjua/kumfahamu usimdharau pia. Utakuja kushangaa na kujiona fala sana.
 
Kama mtu haujawahi kukutana nae uso kwa uso usijiaminishe kwamba unamjua. Wewe unamjua kwa namna ambayo ametaka wewe umjue na asilimia nyingi huyo unayemjua ni mtu ambaye ni wa kisadikika hayupo (Fictional character).

Unamjua kupitia mtandaoni na picha unazo amekutumia lakini ukitaka kuonana naye kwa mazuri anaingia mitini?

Unaanzisha mahusiano na mtu mtandaoni ila ikifika hatua ya kuonana hatokei? Ukimtumia nauli pia haji?

Mtu anayesadikika atakujaje?😂😂. Unataka kukutana na mtu ambaye hayupo? Mtu wa kwenye maandishi? Mtapigwa sana.

Hupaswi kuamini unamjua mtu kwa namna ambayo amekuambia yeye ni nani, hata kama amekutumia picha. Haupaswi pia kuamini hata hizo picha ni za kwake.

Hupaswi kuamini mtu mnayejuana tu mtandaoni ni jinsia fulani. Hata kama amejitambulisha kwa jinsia hiyo haupaswi kuamini kwamba ndio jinsia yake kama haujawahi kukutana naye uso kwa uso. Inawezekana anayejinadi ni mwanamke na wewe umempenda sio mwanamke kweli na vice versa.

Sasa mtandao kama Jamiiforums watu wanatumia majina ya uongo, Profile za uongo lengo likiwa moja tu, Asijulikane yeye ni nani ili awe huru kuchangia. Na wewe unaamini kwamba yale mtu aliyoyaandika kuhusu yeye ni kweli 100%. Huyu huyu mtu anasema hajawahi kukutana na mtu nje ya jamiiforums na hataki na wewe unaamini kila anachokiandika.

Unaona mtu kashare picha zake kwenye ile thread ya Mshana Jr , na wewe unaamini yule aliyeweka hiyo picha ndio yeye kwenye picha. Hapo unaamini umeshamjua. Basi unakuta mtu anadondokea hiyo picha unacheka tu maana unakuta ni picha ya li black Amerca huko imeibwa insta. Na ikikandiwa unacheka tu namna mtu anakandia picha ya mtu aliye nigeria huko akijua anamuumiza aliyeiweka.

Unakuta mtu anajiamini kutukana watu, kudhalilisha watu, kutukana mamlaka za juu halafu anaweka picha na wewe unaamini ni yakwake. Unaamini ana jeuri ya kuweka picha hata kama kaziba sura. (hivi ukutane na picha ya mke wako au mume wako, mfanyakazi mwenzako au ndugu yako au mtu unayemjua vizuri imekatwa sura tu utashindwa kumjua huyu ni fulani).

Mitandaoni kila kitu ni feki. Mtu mwenye nia ya kutokujulikana hawezi kutoa taarifa zake za kweli. Kila kitu lazima aki twist ili ushindwe ku connect dots. Yeye anabadilika kutokana na upepo unavyoenda.

Akikwambia anafanya kazi A sio kweli. Akikwambia Kaoa/kuolewa unakuta sio kweli hata kwa wazazi hajatoka. Akikwambia ana gari unakuta sio kweli hata kuendesha gari hajui, Akikwambia ana nyumba ni kwamba hata bei ya mfuko wa cement haijui. Akiweka picha unakuta sio yake kachukua kwenye pages za watu huko.

Halafu unakuta kuna watu wanagombana na kuoneana wivu na wanachukiana na kupendana mitandaoni kwa kutumia hizi hizi characters za watu wa kusadikika. Kuna maisha ya kweli mitaani acheni kubabaishwa na watu wa kusadikika.
Palina kumbe ww ni wa kufikirika
 
Back
Top Bottom