Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Hizi mada ziliwahi kuletwa kwa mtindo tofauti huku zingine zikiwa na mlengwa wa kidini.Nilitaka kuona maoni yako kuhusu hili mkuu.
Ili aendelee kuzungusha uchhi magheto mbalimbali hapa tzKuna Rafiki ang wa kike anampango wa kwenda dubai, badhani nitampa taarifa ya vitisho ili aghairishe
IQ yako ndogo sanaMbona wewe hujaenda?
Kuna upuuzi mwingi tu kaandika Mleta mada na wala sio post ya kwanza kuleta humu na wenzake.
Waarabu WANGESE NASA!!Utangulizi: Je, Unatamani Kwenda Dubai Kufanya Kazi? Fikiri Tena!
Kila siku kwenye mitandao ya kijamii kuna video na picha za maisha ya kifahari Dubai — magari ya kifahari, majengo marefu, maduka ya thamani, na warembo waliopendeza kwenye fukwe. Ndiyo maana maelfu ya vijana kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, India, Ufilipino, Bangladesh na kwingineko hupakia mabegi yao na kuanza safari ya kuifuata “ndoto ya Kiarabu.”
Lakini ukweli mchungu unaofichwa na picha hizo za Instagram ni huu: wengi wanaoenda Dubai wanajipeleka utumwani kwa hiari yao, wakitumbukia kwenye mateso yasiyoelezeka huku wakiwa na matumaini ya maisha bora.
1. Dubai: Jumba la Mchanga Lililojengwa Kwa Mateso ya Maskini
Dubai si mji wa historia wala utamaduni uliojengwa kwa miaka mingi kama miji mikuu ya Afrika, Asia au Ulaya. Ni jangwa lililogeuzwa jiji la kifahari kwa kutumia pesa za mafuta na jasho la wahamiaji masikini.
Miaka ya 1950, Dubai ilikuwa bandari ndogo isiyojulikana. Leo hii, ndani ya muda wa chini ya kizazi kimoja, imejengwa kwa kasi ya kutisha – lakini si Waarabu walioujenga, bali Wahindi, Wafilipino, Wabangladeshi, na hata baadhi ya Waafrika.
Hawa wahamiaji, waliovutwa na ahadi za mishahara mizuri, hujikuta wamefungwa katika mnyororo wa kijasusi, manyanyaso, na hali mbaya ya kazi isiyo na haki wala utu.
2. Hali Halisi: Wanyama Wanaishi Vizuri Kuliko Wafanyakazi Wahamiaji
Wengi wa wafanyakazi wa kawaida — hasa wahudumu, wasafishaji, madereva na mafundi — hukumbana na mambo yafuatayo mara tu wanapofika:
- Pasipoti kunyang’anywa: Ili kuwadhibiti, mabosi wengi huwachukulia wafanyakazi wao pasipoti ili wasiweze kutoroka.
- Mishahara midogo na kuchelewa kulipwa: Mtu anayeahidiwa dola 500 kwa mwezi anaweza kulipwa dola 150, ikiwa atalipwa kabisa.
- Malazi ya aibu: Wanaishi kwenye vyumba vya msongamano mkubwa, watu 10 hadi 20 kwenye chumba kimoja, bila hewa wala faragha.
- Kazi masaa 12-18 kwa siku bila likizo: Hii ni kinyume kabisa na haki za binadamu.
- Unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia: Kutukanwa, kupigwa, na hata kutishiwa maisha ni jambo la kawaida.
3. Je, Huu Sio Utumwa wa Kisasa?
Watanzania wengi wanaoenda huko, hasa kupitia mawakala wa ajira, huambiwa watafanya kazi ya ofisini au nyumba za kifahari. Lakini wanapofika, wanajikuta wamefungwa katika kazi za mateso.
Wanawake wengi waliodhani wanaenda kuwa “housemaids” huishia kufanywa vibarua wa kazi zote — wengine hufanyiwa unyama na kudhalilishwa, huku sauti zao hazisikiki.
Baadhi yao hujaribu kutoroka, lakini hukamatwa na kurudishwa kama wahalifu. Wengine huchagua kujitoa uhai kutokana na mateso wanayoyapata. Hii haijaripotiwi sana kwenye vyombo vya habari — lakini ni ukweli unaojulikana na mashirika ya haki za binadamu duniani kote.
4. “Fursa” au Mtego? Watanzania, Jifunzeni kwa Waliohangaika
Wengi huamini kuwa maisha yoyote ya kuteseka nje ya nchi ni bora kuliko maisha ya nyumbani. Huu ni uongo wa kisasa.
Je, unajiuliza kwa nini baadhi ya watu wanauza mashamba na kuchukua mikopo ili waende “kuhangaika” huko? Kwa sababu wanaamini waliyoyaona kwenye TikTok na Instagram ni maisha halisi.
Lakini ukweli ni kwamba Dubai imejengwa kwa ajili ya matajiri wachache, na imewekwa kama mtego kwa masikini wanaotafuta maisha bora. Bila maarifa ya kutosha, mtanzania wa kawaida anaweza kufikiri anaenda kwenye pepo la ajira, kumbe anaingia kuzimu ya mateso ya kifedha, kijamii, na kisaikolojia.
5. Kwa Nini Waarabu Wanapenda Watumwa Wa Kujileta?
Wenyeji wa mataifa haya si wajinga — wanajua kuwa maisha ya kifahari wanayoishi yanalindwa na ukimya wa wale wanaoteseka chini ya miguu yao.
- Wanajua watu wanapenda pesa, hivyo wanatoa ahadi za mishahara mizuri.
- Wanajua watu wana njaa, hivyo hawatasema chochote hata wakiteswa.
- Wanajua serikali za nchi maskini hazina uwezo wala nia ya kuwatetea raia wao.
Kwao, kila Mtanzania anayeingia Dubai kupitia “mwakala wa ajira” ni mtumwa mpya wa karne hii.
6. Onyo Kali kwa Watanzania: Acha Kufukuzia Ndoto kwa Upofu
Kabla hujachukua mkopo au kuuza kiwanja ili kuenda kufanya kazi huko, tafakari:
- Je, uko tayari kunyanyaswa, kulala kwenye dari la chuma bila hewa, na kupigwa bila msaada?
- Je, uko tayari kufungwa pasipoti yako na kushindwa kurudi nyumbani hata ukitaka?
- Je, uko tayari kutumika kama mashine ya kazi, kisha kutupwa baada ya miaka miwili ukiwa mgonjwa na uliyechoka?
Hitimisho: Ukombozi wa Kifikra Lazima Uanze Sasa
Watanzania, tusidanganywe na maghorofa ya Burj Khalifa au magari ya dhahabu. Huko ni jela ya kifahari kwa masikini wa dunia.
Ajira halisi ni ile yenye heshima, haki, na utu. Kama nchi, tukikubali kuwa kila fursa kutoka nje ni fursa njema, basi tutakuwa kizazi cha watumwa wa kisasa — wenye pasipoti lakini bila uhuru.
Onyo letu kwa vijana wa Tanzania ni hili:
Usiache kuamka kila asubuhi huku nyumbani kujitafuta kwa jasho lako mwenyewe, ili uende kufanyiwa kazi kama mbwa kwenye jangwa la watu wasiojua huruma.
Nyumba ya kifahari isiyo na roho haiwezi kuwa makazi salama ya binadamu. Tafakari kabla ya kusafiri.
MkuKuna upuuzi mwingi tu kaandika Mleta mada na wala sio post ya kwanza kuleta humu na wenzake.
1. Dubai haijaundwa na mafuta na wala sio mji wa karibuni, Dubai creek ipo mamia ya miaka na imeundwa na Wahindi, Wairan na wa kazi wa hapo, kuna Nyuzi kibao na picha kibao, na hata sasa hivi Dubai haitegemei mafuta, At most ilipata mikopo ya mafuta kujiendeleza zaidi ila definetely haijatokana na mafuta.
View attachment 3353353
2. Watu wengi wanaoijua Dubai na UAE ina watanzania wengi vyeo vikubwa vikubwa kwenye majeshi na Polisi, Hapa Tanga nipo na wastaafu wa Jeshi lao ambao ni watanzania kila siku Tunapiga Stori hata ukicheki online utaona jeshi lao na kwanini nchi zao zinataniwa ni za UN
View attachment 3353360
3. Watanzania wengi wana Tegemea Biashara zao kuchukulia mizigo dubai, na wameanza miaka zaidi ya 40 sasa, long story Short UAE ni nchi ya tatu kwa Watanzania kuimport Bidhaa baada ya China na India na Ni Nchi ya pili ambayo Watanzania wanauza vitu. Tuna Import 1.4B usd na Tuna Export 1.6B usd kwao.
4. Hata wafanyakazi wa ndani ambao wengi wa naongelea toka Africa Hawawi preferred kule, sababu wengi wanaoishi Dubai ni watu wenye hela nyingi kuanzia wazawa ambao wapo Takriban milioni 1-2 Millionaire na Billionaires, hakuna mtu ambaye anaingiza mamia ya mamilioni kwa mwezi ata chukua mtu amlee mwanae ambaye hana hata elimu ya Chakula, hajui hata chakula hichi kina vitamin gani, Ndio maana wafilipino wengi wamechukua hizo nafasi.
Pia ukifuata sheria zote ukiwa na vyeti na serikali ya Dubai na ya kwako ikijua upo wapi ngumu sana kupatwa na tatizo. Wengi wanaoteswa ni wale wanatumia madalali na wanafanya kazi bila vibali.
5. Mishahara ya Dubai ni mikubwa as long as una qualification, na pia Kwa wanaojiajiri ni tax heaven, ndio maana mamilionea kote Duniani wanakimbilia hapo, Urusi walivyoekewa Vikwazo Ma oligarch wao walikimbilia Dubai, mpaka sasa Dubai ndio Headquarter za Telegram,
View attachment 3353366
Dubai/UAE ni top destination ya Millionaire Duniani.
Si tu Millionaire hata wanasiasa wote wanakimbilia huko, ngumu kukuta mwanasiasa mkubwa Africa hana nyumba Dubai.
So mleta mada ni wale wale wenye mentality za masikini anaefikiri kila mtu kaishia la saba anabeba begi lake anaenda Dubai, wakati watu wanaifanya biashara dubai za Matrilioni miaka na miaka toka Tanzania.
Mkuu ahsante pekee haitoshi kwa ufafanuzi mzuri Mungu akubariki.Kuna upuuzi mwingi tu kaandika Mleta mada na wala sio post ya kwanza kuleta humu na wenzake.
1. Dubai haijaundwa na mafuta na wala sio mji wa karibuni, Dubai creek ipo mamia ya miaka na imeundwa na Wahindi, Wairan na wa kazi wa hapo, kuna Nyuzi kibao na picha kibao, na hata sasa hivi Dubai haitegemei mafuta, At most ilipata mikopo ya mafuta kujiendeleza zaidi ila definetely haijatokana na mafuta.
View attachment 3353353
2. Watu wengi wanaoijua Dubai na UAE ina watanzania wengi vyeo vikubwa vikubwa kwenye majeshi na Polisi, Hapa Tanga nipo na wastaafu wa Jeshi lao ambao ni watanzania kila siku Tunapiga Stori hata ukicheki online utaona jeshi lao na kwanini nchi zao zinataniwa ni za UN
View attachment 3353360
3. Watanzania wengi wana Tegemea Biashara zao kuchukulia mizigo dubai, na wameanza miaka zaidi ya 40 sasa, long story Short UAE ni nchi ya tatu kwa Watanzania kuimport Bidhaa baada ya China na India na Ni Nchi ya pili ambayo Watanzania wanauza vitu. Tuna Import 1.4B usd na Tuna Export 1.6B usd kwao.
4. Hata wafanyakazi wa ndani ambao wengi wa naongelea toka Africa Hawawi preferred kule, sababu wengi wanaoishi Dubai ni watu wenye hela nyingi kuanzia wazawa ambao wapo Takriban milioni 1-2 Millionaire na Billionaires, hakuna mtu ambaye anaingiza mamia ya mamilioni kwa mwezi ata chukua mtu amlee mwanae ambaye hana hata elimu ya Chakula, hajui hata chakula hichi kina vitamin gani, Ndio maana wafilipino wengi wamechukua hizo nafasi.
Pia ukifuata sheria zote ukiwa na vyeti na serikali ya Dubai na ya kwako ikijua upo wapi ngumu sana kupatwa na tatizo. Wengi wanaoteswa ni wale wanatumia madalali na wanafanya kazi bila vibali.
5. Mishahara ya Dubai ni mikubwa as long as una qualification, na pia Kwa wanaojiajiri ni tax heaven, ndio maana mamilionea kote Duniani wanakimbilia hapo, Urusi walivyoekewa Vikwazo Ma oligarch wao walikimbilia Dubai, mpaka sasa Dubai ndio Headquarter za Telegram,
View attachment 3353366
Dubai/UAE ni top destination ya Millionaire Duniani.
Si tu Millionaire hata wanasiasa wote wanakimbilia huko, ngumu kukuta mwanasiasa mkubwa Africa hana nyumba Dubai.
So mleta mada ni wale wale wenye mentality za masikini anaefikiri kila mtu kaishia la saba anabeba begi lake anaenda Dubai, wakati watu wanafanya biashara dubai za Matrilioni miaka na miaka toka Tanzania.
Dubai maisha hayatafutwi hivyo kwamba unaenda tu ni mji ghali sana,Mku
Mkuu ahsante pekee haitoshi kwa ufafanuzi mzuri Mungu akubariki.
Naomba ushauri Mimi ni shahada ya maendeleo ya jamii, kwasasa ni afisa usafirishaji
Unanishauri niuze bodaboda yangu niende kutafuta maisha Dubai?? Naomba ushauri wako mkuu
Mkuu nashukuru sana kwa huu muongozo, Mimi tayari Nina maagent ambao ni wa uhakika kuhusu KAZI, so naondoka huku tayari nina mkataba wa KAZI.Dubai maisha hayatafutwi hivyo kwamba unaenda tu ni mji ghali sana,
Issue za usafirishaji zinalipa kule kwa hio Experience yako.
Namna ya kufika
1. Uwe na mtu kule unaemfahamu na sio hawa madalali akuvute ama akupe connection.
2. Omba kazi direct kwenye makampuni na kampuni ndio ikutolee visa na ku kulipia nauli.
3. Tumia nafasi za kazi zinazotolewa na Serikali.
Mfano kama hizi Ajira mpya za Qatar walizotangaza serikali naona Kuna foundation kama ya mkapa ndio inasimamia angalia humo mara kwa mara
Usiuze Asset zako na kuenda sehemu ambayo hujui ukifika unafanya nini.
Kwanini agent asikutolee yeye Viza na nauli? Ushauri wangu mkuu usiuze mpaka uwe na uhakika ume sign mkataba wa kazi unaanza.Mkuu nashukuru sana kwa huu muongozo, Mimi tayari Nina maagent ambao ni wa uhakika kuhusu KAZI, so naondoka huku tayari nina mkataba wa KAZI.
Ni Sahihi kuuza hiyo asset? Lengo langu sio kuishia Dubai lengo langu ni kwenda nchi kama Sweden Finland nk
Je kwa mantiki iyo nipo Sahihi kuuza asset yangu na kwenda kufanya kazi yoyote ili nitimize malengo yangu??
Yaani uuze ardhi na Mali nyingine nchi Yako mwenyewe ili ukawe houseboy UAE au Sweden ?Mkuu nashukuru sana kwa huu muongozo, Mimi tayari Nina maagent ambao ni wa uhakika kuhusu KAZI, so naondoka huku tayari nina mkataba wa KAZI.
Ni Sahihi kuuza hiyo asset? Lengo langu sio kuishia Dubai lengo langu ni kwenda nchi kama Sweden Finland nk
Je kwa mantiki iyo nipo Sahihi kuuza asset yangu na kwenda kufanya kazi yoyote ili nitimize malengo yangu??
Ndio mkuu kama huko Kuna masilahi Zaidi ya huku naenda tu Haina shida tutaangalia fursa na future planYaani uuze ardhi na Mali nyingine nchi Yako mwenyewe ili ukawe houseboy UAE au Sweden ?
Sio kwa kuuza mali mkuuNdio mkuu kama huko Kuna masilahi Zaidi ya huku naenda tu Haina shida tutaangalia fursa na future plan
Wala haihitaji unabii, watumwa wa waarabu wako hata hapa Africa.Uzi utageuka mabishano ya kidini, mimi sio nabii lakini🤔
Pole, mpaka leo hujajuwa tafsiri ya utumwa ni nini kweli?Karibu UAE chief
Toa tafsiri ya utumwa?