Usichokifahamu kuhusu haki na wajibu wa mtoto

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
280
Reaction score
173
Mtoto ni binadamu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18. Katika suala lolote lile liwe la binafsi, taasisi, kimahakama au vyombo vingine vya maamuzi maslahi ya mtoto yatawekwa mbele kwanza.

Baadhi ya watu katika jamii wamekuwa na uelewa finyu kuhusu haki na wajibu wa mtoto, katika jamii, kwa asilimia kubwa watu wanajua haki ya mtoto ni kupata elimu tu. Lakini kuna haki nyingi ambazo mtoto anastahili kupata zaidi ya ile ya elimu. Tuzitazame haki za mtoto kwa upana wake.

Ubaguzi wowote ule dhidi ya mtoto hauruhusiwi, hii inamaanisha ukimfanyia ubaguzi mtoto yoyote yule na kwa namna yoyote ile ni umevunja hazi ya mtoto.

Mtoto ana haki ya kupata jina. Mtoto yeyote yule anapozaliwa ana haki ya kupatiwa jina. Jina ni moja kati ya utambulisho wa binadamu yeyote yule.

Mtoto ana haki ya kujua utaifa wake.

Mtoto ana haki ya kujua wazazi wake waliomzaa. Hii inamaanisha hata kama mtoto analelewa na mtu mwingine ambae sio mzazi wake bado ana haki ya kuwajua wazazi wake waliomzaa, kumficha mtoto utambulisho wa wazazi wake ni kumnyima moja kati ya haki zake za msingi.

Mtoto ana haki ya kusajiriwa kwenye vyombo vinavyo husika

Mtoto ana haki ya kuishi na wazazi wake au mlezi, na inapoonekana mzazi au mlezi anamtesa au anaweza kumsababishia mtoto madhara yoyote mabaya au kuishi na mzazi au mlezi si kwa maslahi ya mtoto mahakama inaweza kuamuru atolewe kwa mzazi au mlezi huyo.

Mtoto ana haki ya kupata matunzo toka kwa mzazi, au mlezi au mtu yeyote anayeishi naye; Matunzo ambayo mtoto anastahili kuyapata kutoka kwa mzazi au mlezi ni kama vile:
Kupata chakula bora.
Kupata malazi bora.
Kupata mavazi.
Kupata huduma ya afya ikiwamo CHANJO.
Kupata elimu na maelekezo mengine.
Uhuru wa kuamua.
Kucheza na kupumzika.

Kwa mujibu wa sheria hairuhusiwi kwa jinsi yoyote ile mzazi, au mlezi au mtu anayeishi na mtoto kutompatia mtoto haki anazostahili kama ilivyoorodheshwa hapo juu.

Mtoto mwenye ulemavu anastahili huduma ya ziada kuhakikisha anaendelezwa kwa kiwango cha uwezo wake na kuwa aweza kujitegemea.

Mzazi au mlezi anayeishi na mtoto ana majukumu ya kutimiza kwa mtoto anayeishi naye, majukumu ya mzazi au mlezi kwa mtoto ni kama ifuatavyo;
Kuhakikisha anaishi, anathaminiwa, anaheshimiwa, anapata mda wa kupumzika, anakuwa huru, anapata elimu na malazi.
Kumlinda dhidi ya manyanyaso, ubaguzi, vurugu, uonevu, ukatili au kupata madhara kimwili au kisaikolojia.
Kumwelekeza, kumjali, kumsaidia na kutoa matunzo ili kuhakikisha maendeleo na maisha ya mtoto.
Kuhakikisha mtoto anapata malezi bora toka kwa mtu mwingine iwapo yeye mzazi hatakuwepo. Iwapo wazazi wa mtoto hawapo, majukumu ya mzazi yatachukuliwa na mlezi ambaye atapewa majukumu hayo kwa amri ya mahakama au kutokana na mila na desturi.
Mtoto pia ana haki ya kufaidi mali iliyotafutwa na wazazi wake.

Mtoto ana haki ya kutoa maoni, kusikilizwa na kushirikishwa katika maamuzi yanayomuhusu.

Mtoto haruhusiwi kufanyishwa kazi ambayo inaweza kumuathiri kiafya, kielimu, kiakili au kukuwa kimwili au kiakili.

Mtoto anastahili kulindwa dhidi ya mateso na adhabu zinazodhalilisha. Kuenda kinyume na haki na ustawi wa mtoto na mzazi kutotimiza wajibu wake ni kosa la jinai.

Mambo ambayo mtoto haruhusiwi kuyafanya, kushiriki au kushirikishwa ni kama vile;
Kuingia eneo la disko, baa au klabu ya usiku.
Kuuza au kuuziwa vitu kama vile sigara, pombe, madawa ya kulevya au kilevi cha aina yeyote Ile.
Mtoto haruhusiwi kufanya kazi usiku. Yaani kuanzia saa 4 hadi saa 12 asubuhi.
Mtoto hatakiwi kulazimishwa kufanya kazi.
Mtoto ana haki ya kufanya kazi ili mradi kazi ni nyepesi, isiyo ya unyonyaji na kuwa mtoto ana umri si chini ya miaka 14. Kumfanyisha mtoto kazi ya hatari kama vile kuingia baharini, au ziwani, machimboni, kubeba mizigo mizito, viwanda vya kemikali, na sehemu za baa, hoteli na maeneo ya starehe ni kosa kisheria.

Mambo mengine muhimu kuhusu haki za mtoto ni kama vile;
Mtoto aliyemaliza darasa la 7 au aliye na miaka 14 ana haki ya kupata mafunzo ya kazi kwa vitendo. Lazima kuwe na mkataba kati ya anayetoa mafunzo na mzazi, mlezi au ndugu wa mtoto. Mtoa mafunzo atalazimika; kutumia ujuzi wake wote kumfundisha mtoto kwa kujali uwezo wa mtoto, kuwajibika kwa madhara yeyote yatakayo mpata mtoto wakati wa mafunzo, kuhakikisha mazingira salama kwa afya ya mtoto, kumuandaa mtoto kujitegemea baada ya mafunzo na kujali maslahi ya mtoto husika.

Iwapo wazazi wametengana mtoto atakuwa na haki zifuatazo;
Matunzo na elimu ile ile aliyokuwa anaipata kabla wazazi hawajetanga.
Kuishi na mzazi ambae ana uwezo wa kuhakikisha maslahi ya mtoto yanalindwa.
Mtoto ana haki ya kumtembelea na kuishi na mzazi mwingine.
Iwapo mtoto ni chini ya miaka 7 ataishi na mama yake ili mradi kuishi na mama hakutaathiri maisha ya mtoto.

Yafahamu makundi ya watoto yaliyo kwenye mahitaji ya malezi na matunzo

Yatima au aliyetupwa na wazazi wake
Aliyetelekezwa au anayeteswa.
Anayeishi na mzazi au mlezi asiyejali majukumu yake.
Anayeishi katika umaskini.
Anayeishi na mzazi au mlezi ambaye kutokana na kuwa mharifu au mlevi anashindwa kutimiza majukumu yake kwa.mtoto.
Anaye tangatanga kwa kukosa sehemu ya kuishi.
Ombaomba.
Mtoto anaye fuatana na kulelewa na ombaomba.
Mtoto ambaye yuko chini ya matunzo ya mzazi au mlezi maskini.
Mtoto ambaye mda wote anafuatana na waharifu au wanawake wanao jiuza.
Aliye katika hatari ya kusafiriashwa kwenda kuuzwa.
Mtoto anaye jihusisha na uharifu au matendo kinyume na maadili.
Mtoto anaye jihusisha katika uharifu mkubwa.
Mtoto aliyeko katika mazingira hatarishi.
Na Mtoto anaye lelewa na mlemavu ambaye hana uwezo wa kutoa matunzo kwa mtoto.

Ufahamu wajibu wa mtoto.

Mtoto ana wajibu wa kuweka mahusiano mazuri katika familia.
Mtoto pia ana wajibu wa kuwaheshimu wazazi, walezi, na watu wote wanao mzidi umri na kuwasaidia wanapohitaji msaada.
Mtoto ana wajibu wa kulitumikia taifa na jamii kwa kutumia uwezo alio nao na kutokana na umri wake.
Mtoto pia ana wajibu wa kulinda na kuendekeza mshikamano wa taifa na jamii.
Mtoto ana wajibu wa kulinda na kuendeleza mila na desturi za jamii na taifa kwa ujumla.

MTOTO NI TAIFA LA KESHO, MTOTO YEYOTE ANA HAKI YA MAISHA BORA KWA USTAWI WA TAIFA LA KESHO.
 
Mtoto ni binadamu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18. Katika suala lolote lile liwe la binafsi, taasisi, kimahakama au vyombo vingine vya maamuzi maslahi ya mtoto yatawekwa mbele kwanza.

Baadhi ya watu katika jamii wamekuwa na uelewa finyu kuhusu haki na wajibu wa mtoto, katika jamii, kwa asilimia kubwa watu wanajua haki ya mtoto ni kupata elimu tu. Lakini kuna haki nyingi ambazo mtoto anastahili kupata zaidi ya ile ya elimu. Tuzitazame haki za mtoto kwa upana wake.

Ubaguzi wowote ule dhidi ya mtoto hauruhusiwi, hii inamaanisha ukimfanyia ubaguzi mtoto yoyote yule na kwa namna yoyote ile ni umevunja hazi ya mtoto.

Mtoto ana haki ya kupata jina. Mtoto yeyote yule anapozaliwa ana haki ya kupatiwa jina. Jina ni moja kati ya utambulisho wa binadamu yeyote yule.

Mtoto ana haki ya kujua utaifa wake.

Mtoto ana haki ya kujua wazazi wake waliomzaa. Hii inamaanisha hata kama mtoto analelewa na mtu mwingine ambae sio mzazi wake bado ana haki ya kuwajua wazazi wake waliomzaa, kumficha mtoto utambulisho wa wazazi wake ni kumnyima moja kati ya haki zake za msingi.

Mtoto ana haki ya kusajiriwa kwenye vyombo vinavyo husika

Mtoto ana haki ya kuishi na wazazi wake au mlezi, na inapoonekana mzazi au mlezi anamtesa au anaweza kumsababishia mtoto madhara yoyote mabaya au kuishi na mzazi au mlezi si kwa maslahi ya mtoto mahakama inaweza kuamuru atolewe kwa mzazi au mlezi huyo.

Mtoto ana haki ya kupata matunzo toka kwa mzazi, au mlezi au mtu yeyote anayeishi naye; Matunzo ambayo mtoto anastahili kuyapata kutoka kwa mzazi au mlezi ni kama vile:

Kwa mujibu wa sheria hairuhusiwi kwa jinsi yoyote ile mzazi, au mlezi au mtu anayeishi na mtoto kutompatia mtoto haki anazostahili kama ilivyoorodheshwa hapo juu.

Mtoto mwenye ulemavu anastahili huduma ya ziada kuhakikisha anaendelezwa kwa kiwango cha uwezo wake na kuwa aweza kujitegemea.

Mzazi au mlezi anayeishi na mtoto ana majukumu ya kutimiza kwa mtoto anayeishi naye, majukumu ya mzazi au mlezi kwa mtoto ni kama ifuatavyo;

Mtoto pia ana haki ya kufaidi mali iliyotafutwa na wazazi wake.

Mtoto ana haki ya kutoa maoni, kusikilizwa na kushirikishwa katika maamuzi yanayomuhusu.

Mtoto haruhusiwi kufanyishwa kazi ambayo inaweza kumuathiri kiafya, kielimu, kiakili au kukuwa kimwili au kiakili.

Mtoto anastahili kulindwa dhidi ya mateso na adhabu zinazodhalilisha. Kuenda kinyume na haki na ustawi wa mtoto na mzazi kutotimiza wajibu wake ni kosa la jinai.

Mambo ambayo mtoto haruhusiwi kuyafanya, kushiriki au kushirikishwa ni kama vile;
Kuingia eneo la disko, baa au klabu ya usiku.
Kuuza au kuuziwa vitu kama vile sigara, pombe, madawa ya kulevya au kilevi cha aina yeyote Ile.
Mtoto haruhusiwi kufanya kazi usiku. Yaani kuanzia saa 4 hadi saa 12 asubuhi.
Mtoto hatakiwi kulazimishwa kufanya kazi.
Mtoto ana haki ya kufanya kazi ili mradi kazi ni nyepesi, isiyo ya unyonyaji na kuwa mtoto ana umri si chini ya miaka 14. Kumfanyisha mtoto kazi ya hatari kama vile kuingia baharini, au ziwani, machimboni, kubeba mizigo mizito, viwanda vya kemikali, na sehemu za baa, hoteli na maeneo ya starehe ni kosa kisheria.

Mambo mengine muhimu kuhusu haki za mtoto ni kama vile;
Mtoto aliyemaliza darasa la 7 au aliye na miaka 14 ana haki ya kupata mafunzo ya kazi kwa vitendo. Lazima kuwe na mkataba kati ya anayetoa mafunzo na mzazi, mlezi au ndugu wa mtoto. Mtoa mafunzo atalazimika; kutumia ujuzi wake wote kumfundisha mtoto kwa kujali uwezo wa mtoto, kuwajibika kwa madhara yeyote yatakayo mpata mtoto wakati wa mafunzo, kuhakikisha mazingira salama kwa afya ya mtoto, kumuandaa mtoto kujitegemea baada ya mafunzo na kujali maslahi ya mtoto husika.

Iwapo wazazi wametengana mtoto atakuwa na haki zifuatazo;
Matunzo na elimu ile ile aliyokuwa anaipata kabla wazazi hawajetanga.
Kuishi na mzazi ambae ana uwezo wa kuhakikisha maslahi ya mtoto yanalindwa.
Mtoto ana haki ya kumtembelea na kuishi na mzazi mwingine.
Iwapo mtoto ni chini ya miaka 7 ataishi na mama yake ili mradi kuishi na mama hakutaathiri maisha ya mtoto.

Yafahamu makundi ya watoto yaliyo kwenye mahitaji ya malezi na matunzo

Na Mtoto anaye lelewa na mlemavu ambaye hana uwezo wa kutoa matunzo kwa mtoto.

Ufahamu wajibu wa mtoto.

Mtoto ana wajibu wa kuweka mahusiano mazuri katika familia.
Mtoto pia ana wajibu wa kuwaheshimu wazazi, walezi, na watu wote wanao mzidi umri na kuwasaidia wanapohitaji msaada.
Mtoto ana wajibu wa kulitumikia taifa na jamii kwa kutumia uwezo alio nao na kutokana na umri wake.
Mtoto pia ana wajibu wa kulinda na kuendekeza mshikamano wa taifa na jamii.
Mtoto ana wajibu wa kulinda na kuendeleza mila na desturi za jamii na taifa kwa ujumla.

MTOTO NI TAIFA LA KESHO, MTOTO YEYOTE ANA HAKI YA MAISHA BORA KWA USTAWI WA TAIFA LA KESHO.
Asanteee sana kutumbukusha. Wazazi wengi sada hivi tupo busy na majukumu ya kutafuta pesa tunasahau malezi. Hivyo tubalance vyote ili kujenga ustawi bora wa watoto wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
vp mtoto akishindwa timiza wajibu wake (hapo chini]) ana andelea nufaika na haki izo
 
Back
Top Bottom