Usidanganyike kuwa Mahusiano ni "kusikilizana" utaachwa. Ukweli ni lazima mmoja amsikilize mwenzake ndio mtadumu

Usidanganyike kuwa Mahusiano ni "kusikilizana" utaachwa. Ukweli ni lazima mmoja amsikilize mwenzake ndio mtadumu

Mmh thubutu ukiona hivo mmoja anajitutumua lakini anafuata maagizo kimyakimya
Kuna best angu mmoja yeye na mmewe ni kama familia ya kambale.... yani wote wana ndevu, wakianza kuzichapa sasa, ni mawe wanarushiana kama hawajuani, baada ya wiki wanauguza majeraha, wakipona penzi lipo pale pale.

Wakianza kutukanana kwenye simu, dakika zinaisha anaagiza tena vocha anajiunga wanaendelezaa baada ya wiki ananunua p2 kuzuia mimba ya huyo mme.

Mahusiano yana mambo na hayafanani!!!!
Narudi pale pale inategemea...
 
Siongezi neno wala kupunguza.

Mahusiano ya kusikilizana huwa nikuongopeana. Ukweli wa mahusiano yanayodumu ni yale mmoja lazima amsikilize mwingine.

Mfumo wa mahusiano ulivyo ni wa HEAD and TAIL! (Kichwa na mkia)

Treni hata kama ina vichwa viwili lakini shuruti kimoja lazima kiwe mkia ndo kuwepo na mwendo.

Ndivyo ilivyo kwenye mahusiano hasa ukileta harakati kwenye mapenzi hutoboi.

"HIVYO NDIVYO YANASEMA MAHUSIANO"
Bila kusikilizana hamtaweza kwenda pamoja. Na ni ngumu katika mahusiano ukawa juu muda wote au kiongozi muda wote, kuna muda utahitaji msaada wa mwenzako akuongeze.

Kila m'moja ana eneo lake la ubora.....
 
Ukae kwa kutulia
Kama mmoja atamsikiliza mwenzake basi kutakuwa na nguvu ya ukandamizaji hapo , mfano mimi niwe na girl frnd harafu niwe namuamlia kwa kila kitu yeye ni wakunisikiliza tu unadhani si kutakuwa na mambo mengine namkandamiza
 
Mwamuzi ni nani?
 
Mahusiano ayataki dipromasia ukileta dipromasia utaleta uzi wa kulalamika tu humu mara wife amenipiga kibao!!!! Unaanzaje kupigwa kibao!!!!
 
Back
Top Bottom