Unyakuo imeandikwa ndani ya BIBLIA,
Tapeli ni wewe unayepunguza maandiko na kukataa kitu kilichoandikwa ndani ya BIBLIA.
Biblia ipi hiyo?
Mnapotosha maandiko ndio maana kina mwamposa wanawauzieni maji na mafuta,andazi na keki kwa 10,000 eti yana upako
Huu utapeli eti Kwamba kutakuwa na unyakuo wa siri, watu wa Mungu wataondoshwa duniani pasipo watu wengine kuona na hivyo kuwaepusha watakatifu wa Mungu na ile tabu inayoujia ulimwengu kama ilivyotabiriwa katika maandiko matakatifu.
kwa mujibu wa fundisho hili watakatifu wa Mungu hawatapitia mateso.
Inafundishwa kwamba mpinga Kristo (mnyama aliyetabiriwa katika Ufunuo 13) ataibuka katika siku za mwisho na atatawala kwa miaka 7. Kutakuwa na miaka mitatu na nusu ya mateso kwa wakazi wa dunia, ambapo Israeli watapewa nafasi nyingine ya kumkubali Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao. Warumi 11:26. Wakati hayo yakitokea kanisa la Mungu litakuwa limetoweshwa duniani na hvyo mateso hayo ni kwa ajili ya kuwafanya Israeli wamkubali Yesu na kuokolewa.
Matapeli wanatumia andiko hili katika kufundisha hayo ni Mathayo 24: 40-41. “Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.”
Mambo mengi yaliyopo katika fundisho hili hayana ushahidi katika maandiko matakatifu;
1. Hakuna mahali katika Biblia inaelezwa kuwa mpinga Kristo atatawala kwa muda wa miaka 7, bali tunaona akitawala kwa muda wa miezi 42 au miaka 1260. Danieli 7:25, Ufunuo 11:3, 12:6.
2. Taabu inayozungumzwa katika Biblia, Mathayo 24:22, Marko 13:20. Tena ni kwa sababu ya wateule wa Mungu ndiyo maana hata siku za taabu zitafupishwa. Sasa ikiwa kanisa la Mungu litakuwa limenyakuliwa, kwa maana kwamba halipo duniani, ni akina nani hao ambao kwa ajili yao siku za taabu zitafupishwa, kwamba pasipo hivyo asingaliokolewa mtu hata mmoja?
3. Israeli walipomkataa Mungu hadhi yao ya kuwa taifa teule la Mungu ilikoma. Na kuanzia hapo sisi wote tunahesabika kuwa watoto wa Ibrahimu kwa Imani. Warumi 4:16. Maangamizi ya mji wa Yerusalemu mwaka 70 BK kupitia majeshi ya Rumi ilikuwa ni ishara kuwa Israeli siyo tena taifa teule la Mungu. Baada ya kumpiga mawe Stefano, wanafunzi walitawanyika na milango ikawa wazi kwa mataifa kupata habari njema za wokovu ambazo Israeli walizikataa na kuwaua wajumbe wake. Lakini hii haimaanishi kuwa wamefungiwa kumwamini Kristo, la. Ni kwamba ile nafasi maalumu kama taifa teule haipo tena na hakuna tofauti kati ya myahudi na mtu wa mataifa.
4. Biblia inasema kuwa walio hai hawatawatangulia waliokufa katika kumwona Kristo, na kuja kwa kristo kutakuwa mara moja na ataonekana kila mahali kama ambavyo radi huonekana pande zote. Maelezo Zaidi juu ya mtiririko wa matukio ya kurudi kwa Yesu mara ya pili yatakuwa katika somo maalumu.
Kanuni moja ya kweli ni kwamba neno la Mungu halijipingi, kwa maana limevuviwa na Roho mtakatifu. 2 Timotheo 3:16. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na watu mbalimbali lakini wote waliongozwa na Roho mmoja hivyo sharti kuwe na kukubaliana miongoni mwao. Ikiwa utaona kwamba Biblia inajipinga basi fahamu Dhahiri kuwa hujaelewa vizuri nini hasa Biblia inasema juu ya hilo jambo.
Kanuni nyingine ambayo ni nyongeza juu ya hiyo ni kwamba andiko lazima litafsiriwe katika nuru ya maandiko mengine. “Kwa sababu hiyo neno la Bwana kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa.” Isaya 28:13. Japo fungu moja peke yake laweza kuwa msingi wa fundisho na kujitosheleza, lakini ni vema kuchukua huku kidogo na huku kidogo, kanuni juu ya kanuni na amri juu ya amri, na kwa kupitia hivyo tutaweza kuwa na msingi imara wa nini hasa Biblia inafundisha pasipo kuyumbishwa na kila upepo wa mafundisho. Waebrania 13:9.
Katika sura ya 24 ya kitabu cha Mathayo kuanzia fungu la 36 hadi 44, “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.
43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.” Yesu alikuwa akielezea hali ya dunia itakavyokuwa wakati wa kuja kwa mwana wa Adamu. Alielezea hili kwa kutumia uzoefu wa kipindi cha Nuhu. Tuangalie mambo kadhaa katika haya mafungu ambayo yatatusaidia kuelewa kile ambacho Biblia inafundisha;
1. Wakati wa Nuhu watu waliochukuliwa na gharika ndiyo waliopotea au kuangamia. Wakati Nuhu anaingia katika safina watu walikuwa katika pilika pilika za maisha ya kila siku wasijue hatari iliyo mbele yao na gharika ilivyokuja ikawachukua (ikawatwaa) wote asipone hata mmoja. Hivyo wale waliosalia, yaani Nuhu pamoja na familia yake ndiyo waliookolewa.
2. Biblia haisemi kuwa wanaotwaliwa wanaenda mbinguni kama wengi wanavyodai. Na hata tukisema kwamba waliotwaliwa wanaenda mbinguni na tukalichukuwa fungu kama lilivyo (literal meaning) basi inaonyesha kwamba nusu ya ulimwengu itaenda mbinguni na nusu nyingine itaangamia jambo ambalo siyo kweli. Ni Dhahiri kuwa katika hayo mafungu Yesu hakuzungumzia habari ya kuchukuliwa kwenda mbinguni.
3. Katika hayo mafungu ni wazi kuwa Yesu alikuwa anazungumzia habari ya hukumu ya Mungu juu ya wanadamu. “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” Danieli 7:9-10. Danieli alionyeshwa hukumu iliyokuwa ikiendelea mbinguni wakati Yesu hajaja duniani. Hivi sasa tunavyoishi kuna hukumu inaendelea mbinguni, kila jambo tunalolifanya, liwe jema au baya, linawekwa katika vitabu na kuletwa hukumuni. Yesu atakapokuja duniani atakuja kuwalipa watu ujira wao kulingana na matendo yao. Mathayo 16:27.
4. Tukidumu katika kielelezo cha Nuhu, kwamba waliochukuliwa na gharika ndiyo walioangamia, basi ni wazi kuwa waliotwaliwa pia ndiyo walioangamia. Neno kutwaliwa hapa linaonyesha kuchukua kwa nguvu. Hivyo wakati watu wakiwa katika mambo yao wakistarehe, wakinywa na kula, wakioa na kuolewa, wasijue kuwa kuna hukumu inaendelea ndipo mwisho wao unaamuliwa aidha kwa uzima wa milele au kwa uangamivu wa milele. Hivyo tunaweza kusema hukumu ya Mungu iliwachukua (iliwatwaa).
5. Yesu alitumia kielelezo cha watu wawili ili kuonyesha pande mbili zitakazokuwepo kama matokeo ya hukumu ambazo ni uzima wa milele au mauti ya milele, hakuna upande utakaokuwa katikati. Watu wawili hawakuwakilisha idadi wala uwiano kati ya watakaookolewa na watakaoangamizwa.
Tumekwisha kuona muktadha wa kile Yesu alichokuwa anazungumzia katika hayo mafungu. Jambo la msingi ambalo tunapaswa kushikilia ni kwamba; tunaishi wakati wa hukumu kama ambavyo tumeona katika kitabu cha Danieli, hukumu ya upelelezi. Vitabu vinafunuliwa na kumbukumbu zinaletwa. Jambo la msingi ambalo tunaweza kulifanya wakati huu ni kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu na kudumu katika kufanya yaliyo mapenzi ya Mungu