Usidhani shetani ni mdogo kama unavyofikiri

Shetani hakuondoka alimchapa kichapo kitakatifu msalabani na ukawa mwisho wa Yesu kuishi,
 
Shetani hakuondoka alimchapa kichapo kitakatifu msalabani na ukawa mwisho wa Yesu kuishi,
We bhana wee; wapi tena umeyasoma hayo? Hebu soma Mathayo 4: 11 ..Basi Ibilisi akamwacha .....
Pia soma Luka 4:13 Ibilisi alipokwisha mjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda.
Sasa wewe unayatoa wapi hayo? Hayo ni ya kwako mzee.
Karibu tena tusome pamoja mkuu.
Tena nikukumbushe kwamba Yesu yu hai mzima sasa na hata milele.
 
Wale waliomsulubisha walikua wachamungu? Jiulize hilo swali,
 
Wale waliomsulubisha walikua wachamungu? Jiulize hilo swali,
Siwezi kujiuliza hilo swali kwani haliunganiki na hiki tunachobishania hapa. Waliomsulubisha Yesu ni maaskari na ukizingatia Askari yeyote ni lazima (kwa mujibu wa Taratibu za kazi yake) Aitii mamlaka iliyopo.

Askari wale hawakuwa na ugomvi wowote dhidi ya Yesu. Wao alitimiza wajibu wao. Lakini kwamba eti walikuwa wacha-Mungu hilo halinihusu.

Anayejua ni nani mchaMungu na ni nani siyo mchaMungu ni Mungu peke yake. Je, wewe unafikiri kazi ya Uaskari siyo kazi halali kama kazi nyingine?
 
Wale askari walitumwa na wapinga Kristo, kwa hiyo wapinga Kristo walishinda
 
Yesu Kristo ndiye aliyeumba vyote akiwepo shetani leo hii atakuwaje na nguvu kuliko Yesu?
Yesu aliumba vyote? Ila kuna watu ni wajinga sana.

Unakuta mtu kasoma ana PHD yake anaenda kupigia goti lile sanamu la muigizaji daah!! Hua nashangaa sana.
 
Kwahiyo:-
Shetani alitoka wapi? Kwanini anasumbua wanadamu? Kwanini Mungu hapendi tumfate shetani na mambo yake?
 
Kwahiyo:-
Shetani alitoka wapi? Kwanini anasumbua wanadamu? Kwanini Mungu hapendi tumfate shetani na mambo yake?
Shetan ni cheo kikubwa sana, hasumbui watu, sisi ndio tunamsumbua, miaka yote amekuwa akisingiziwa kuwa ana ubaya ili asipate wafuasi, habari zote za ubaya zilizoandikwa kuhusu yeye ni uongo mtupu.
 
Hata wewe hapo ni raia. Ukifungwa jela maisha jina linabadilika...unakuwa mfungwa
 
Hata wewe hapo ni raia. Ukifungwa jela maisha jina linabadilika...unakuwa mfungwa
Mkuu, mbona unaikwepa mada? Jikite kwenye hoja ya msingi. i.e. Kiumbe aitwaye Malaika na kama uasi wake ulimfutia/Ulimwondolea kuwa ni malaika. Habari ya vyeo isubirishe kwanza ili hoja hii ipate majibu kwanza.

Kwa kutumia mantiki yako hapo juu, yaani Mtu hatoacha kuwa ni mtu eti kwa sababu amefungwa jela au mathalani ataacha kuwa mtu Raia wa Tz kwa sababu amefungwa jela.

Kwa hoja yangu ni kwamba Malaika ataendelea kuwa ni Malaika iwe ni Mbaya au ni Mzuri hiyo sasa itakuwa ni sifa yake kama inavokuwa kwa Mtu e.g. ni mfungwa, ni tapeli, ni mkatili, ni mweupe au ni mjinga n.k.
Nikuombe sasa uijibu hoja yangu.
 
Wale askari walitumwa na wapinga Kristo, kwa hiyo wapinga Kristo walishinda
Dah! aisee; Hivi unajisemea kwa nafsi yako(ie. kama unavyoona na kufikiri wewe binafsi) au kuna mahali maandiko(Reference) yanakuelekeza au ku-support hoja yako? Kama hakuna mahali unafanya Rejea(reference) hoja yako ni BUTU na HAINA mashiko. - Tupa kule.
 
Aisee!!
 
Hoja inaeleweka, ni kweli Ayubu alichapwa pamoja na Yesu, Adam na Hawa wakasomeshwa sasa kwanini nisiseme Shetan alishinda?
 
Mkuu; Ujue hoja au majibu yako yanasomwa na wengi sio mm tu. Chukua tahadhari
Hoja yangu ni hivi, kwakua Yesu alisulubishwa vibaya alipokuwa akijaribu kumpinga Shetani basi Shetani sio wa kuingia nae vitani, Ikiwa Yesu pamoja na nguvu zake zote alipata adhabu yote ile basi sisi binadamu ni akina nani hata tuthubutu kuanzisha vita na Shetani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…