Usiende ughaibuni kutafuta maisha
Katika mapambano ya maisha muda mwingine watu tunakata tamaa, kukata tamaa huanzia ngazi ya mtu binafsi hapo utasikia nafsi inakwambia jiue😭😭😭, mtu huyo huyo anaweza kuikatia tamaa familia yake kwasababu haimsaidii wengi wao hujitenga na familia zao, Kisha anaikatia tamaa nchi yake kua haimsaidii hapo ndipo ndoto za kwenda ughaibuni zinapo zaliwa...!
View attachment 3209750
Katika mapambano ya maisha huwezi kutumia njia alio itumia mtu mwingine kufanikiwa na wewe ukafanikiwa, Kila mtu Kuna namna anajiona kuwa mbeleni huko atakuwaje...! Picha ya nani unataka kuwa unayo wewe mwenyewe kichwani mwako...usijilinganishe na yeyote na Wala usitamani kuwa yeyote kwa kudhani ukipita njia aliyo pita yeye utafanikiwa kama yeye...!

Vijana wengi wakifikia hatua ya kukata tamaa huwaza kukimbia nchi zao na kwenda kutafuta MAISHA ughaibuni wakidhani kule watapata mafanikio ya haraka, haraka...! Huku wakiwa wanasahau kuwa tafsiri sahihi ya mafanikio ni kuridhika na kukitunza kile kidogo ulicho nacho...kama kidogo huwezi kukitunza ujue hata kikubwa hutoweza kukimiliki...!
View attachment 3209760
Mafanikio ni uwezo wa KUMILIKI, siku utakayo weza kuwa walau na Laki 1 tu harafu usipate kimuhe muhe Cha kuitumia ukAihifadhi walau kwa muda wa mwezi tu... ujue umekomaa na muda sio Mrefu unaenda kufanikiwa...ila ukiwa mtu ambae ukishika PESA akili Zina kutoka Hadi hiyo pesa iishe ndio akili zinarudi...MY FRIEND USIENDE UGHAIBUNI 😂😂

Mimi ni miongoni mwa vijana ambao nilihangaika sana kuyatafuta maisha nikasahau kuwa maisha hayaitaji hasira, yanahitaji umakini na ukichaa kidogo😂😂😂

Vijana wengi tunafeli mno kwakuwa wengi wetu akili zetu zimefungwa na JERA hatari la AJIRA, tunasahau kuwa AJIRA haiwezi kufanya uwe tajiri ila zipo fursa kadha wa kadha ambazo ukizifanya kwa ufasaha unafanikiwa maishani...!

Vijana wengi tunapoteza muda mwingi kutafuta AJIRA, na wengi wa vijana wanao taka kwenda ughaibuni lengo lao ni kusaka AJIRA...!

Ndani ya nchi yetu Kuna fursa ambazo wakenya, wachina, Warundi, Wakongo wanazitumia na Zina watoa ki maisha...pindi ambapo unawaza kwenda kutafuta MAISHA nchi za ugenini Kuna watu hapa hapa nyumbani ni MATAJIRI na wametajilikia hapa hapa na hawajawahi kwenda hata Kenya Wala passport ya kusafiria hawana...!
View attachment 3209765
Swala la AJIRA ni ugonjwa wa Dunia nzima Tanzania sio nchi ya kwanza ambayo inashindwa kutoa AJIRA... Marekani yenyewe Ina wamarekani ambao ni masikini wakutupwa Awana hata sehemu ya kulala...!

Nimezunguka duniani nimegundua kuwa nchi yetu imejaaliwa sana, Ina Kila kitu Cha kumfanya mtu atajilike bila kutegemea AJIRA...! Karibia nchi yote ya Tanzania ardhi yake Ina rutuba, tofauti na nchi jirani au nchi nyingine...!

Leo hii wakenya ni vinara wa kuuza mazao ulimwenguni huku mazao hayo wanayatoa Tanzania...😭😭😭

Ni kushauri tu kijana mwenzangu USIENDE UGHAIBUNI KUTAFUTA badala yake tafuta pesa kwa kufanya biashara Kisha kupitia biashara zako vuka mipaka ukafanye biashara...! Toa bidhaa Tanzania peleka nchi zenye uhitaji...! Toa bidhaa huko lete Tanzania...!

UGHAIBUNI ukienda na pesa zako fursa nyingi utaziona, ila ukienda UGHAIBUNI kubahatisha maisha wewe ni sawa na mkimbizi...!

Watanzania wengi ni mabingwa wa kutoa ushauri ambao hawajaombwa, kwa watu wasiowajua, kuhusu mambo wasiyoyafahamu.
 
Binafsi naungana na wewe kwa upande uliozingatia kuuelezea kwamba nchi yetu ina fursa na rasilimali za kutosha.

Umesahau kuhusu mazingira wezeshi au usawa wa kuzifikia na kutumia rasilimali hizo mpaka kuwa na maendeleo zikiwemo sera, vitendea kazi na soko. Hivi vitu bado sana.

Umesema umezunguka dunia nzima, sina uhakika na hilo. Nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea kwao rasilimali ni chache lakini mifumo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii maisha iko imara kwa wananchi wake tofauti na pale kwetu.

Kimsingi nina mipango ya kuzamia nje kwenda kutafuta maisha na ninaamini nikijipata huko ndipo nitaweza kuwa tajiri Tanzania kwa maana ukiwa na pesa ni rahisi kutoboa Tanzania ila kuzipata ukiwa ndani ni shughuli.

Bado upo Dubai Mkuu?
Nimesema nimezunguka duniani...sijasema Dunia nzima😂😂😂

Kuhusu kuzamia, tafuta kwanza pesa ukizipata ndio uzamie...kwenda kudhalilika ugenini sio poua kabisa...

Rejea andiko langu hili...Kwa mnaopenda kwenda ughaibuni kutafuta Maisha

Utajiri unaanzia ndani ya nafsi ifundishe nafasi Yako kuridhika...!

Nipo Dubai ndio...
 
Nimesema nimezunguka duniani...sijasema Dunia nzima😂😂😂

Kuhusu kuzamia, tafuta kwanza pesa ukizipata ndio uzamie...kwenda kudhalilika ugenini sio poua kabisa...

Rejea andiko langu hili...Kwa mnaopenda kwenda ughaibuni kutafuta Maisha

Utajiri unaanzia ndani ya nafsi ifundishe nafasi Yako kuridhika...!

Nipo Dubai ndio...
Kutafuta pesa ughaibuni ni rahisi Mkuu kwa sababu ya mazingira.

Nitakucheki siku sio nyingi natokea huko.
 
Wewe ndio ipo siku utaelewa kua bado unaishi maisha ya fikra za kijamaa,Dunia ni kubwa,toka hapo kijijini,

Acha kukatisha tamaa vijana wetu.
Huyu jamaa katimba nchi moja tu anaanza kutuyeyusha sisi watafuta fursa.

Inatakiwa aongee kwa taarifa na ushahidi kwamba huko nje kuko vp na sio kuja kusema kuwa kutoboa Tanzania ni rahisi kuliko ughaibuni.
 
Sio rahisi kama unavyo dhani...! Ila kwasababu umeshaamua karibu Mimi nitakuwa mpenzi mtizamaji...!

Upinzani uliopo UGHAIBUNI ni mkubwa mno...!
Nchi nyingi hata za Afrika ikiwemo Tanzania kuna fursa za kutosha na sio Ulaya wala Amerika pekee. Hivyo, mtu yeyote akijipanga anaweza kutoboa mahala popote.

Wenzetu wa nchi zingine kama Kenya, Uganda, Nigeria wanatoboa kirahisi sana pande nyingi za dunia.

Tukijipanga tunaweza kufanya vizuri ndani na nje ya mipaka yetu.

Nategemea uzi ujao utatuwekea hapa fursa mbalimbali zinazopatikana nchi ulizozunguka humo duniani.
 
Nchi nyingi hata za Afrika ikiwemo Tanzania kuna fursa za kutosha na sio Ulaya wala Amerika pekee. Hivyo, mtu yeyote akijipanga anaweza kutoboa mahala popote.

Wenzetu wa nchi zingine kama Kenya, Uganda, Nigeria wanatoboa kirahisi sana pande nyingi za dunia.

Tukijipanga tunaweza kufanya vizuri ndani na nje ya mipaka yetu.

Nategemea uzi ujao utatuwekea hapa fursa mbalimbali zinazopatikana nchi ulizozunguka humo duniani.
Hili sasa ndio neno...tukiwaza hivi kama ulivyo andika tutatoboa na tutaacha kuhangaikia AJIRA...Bali tutasaka fursa fursa inazalisha AJIRA kwa wengine
 
Back
Top Bottom