Watanzania wengi ni mabingwa wa kutoa ushauri ambao hawajaombwa, kwa watu wasiowajua, kuhusu mambo wasiyoyafahamu.
 
Nimesema nimezunguka duniani...sijasema Dunia nzima😂😂😂

Kuhusu kuzamia, tafuta kwanza pesa ukizipata ndio uzamie...kwenda kudhalilika ugenini sio poua kabisa...

Rejea andiko langu hili...Kwa mnaopenda kwenda ughaibuni kutafuta Maisha

Utajiri unaanzia ndani ya nafsi ifundishe nafasi Yako kuridhika...!

Nipo Dubai ndio...
 
Kutafuta pesa ughaibuni ni rahisi Mkuu kwa sababu ya mazingira.

Nitakucheki siku sio nyingi natokea huko.
 
Wewe ndio ipo siku utaelewa kua bado unaishi maisha ya fikra za kijamaa,Dunia ni kubwa,toka hapo kijijini,

Acha kukatisha tamaa vijana wetu.
Huyu jamaa katimba nchi moja tu anaanza kutuyeyusha sisi watafuta fursa.

Inatakiwa aongee kwa taarifa na ushahidi kwamba huko nje kuko vp na sio kuja kusema kuwa kutoboa Tanzania ni rahisi kuliko ughaibuni.
 
Sio rahisi kama unavyo dhani...! Ila kwasababu umeshaamua karibu Mimi nitakuwa mpenzi mtizamaji...!

Upinzani uliopo UGHAIBUNI ni mkubwa mno...!
Nchi nyingi hata za Afrika ikiwemo Tanzania kuna fursa za kutosha na sio Ulaya wala Amerika pekee. Hivyo, mtu yeyote akijipanga anaweza kutoboa mahala popote.

Wenzetu wa nchi zingine kama Kenya, Uganda, Nigeria wanatoboa kirahisi sana pande nyingi za dunia.

Tukijipanga tunaweza kufanya vizuri ndani na nje ya mipaka yetu.

Nategemea uzi ujao utatuwekea hapa fursa mbalimbali zinazopatikana nchi ulizozunguka humo duniani.
 
Hili sasa ndio neno...tukiwaza hivi kama ulivyo andika tutatoboa na tutaacha kuhangaikia AJIRA...Bali tutasaka fursa fursa inazalisha AJIRA kwa wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…