Usiginwaji wa Katiba Bungeni: Watetezi wa Haki za Binadamu nchini walaani. Wawakumbushia umuhimu wa kila raia kuilinda Katiba ya Nchi

Usiginwaji wa Katiba Bungeni: Watetezi wa Haki za Binadamu nchini walaani. Wawakumbushia umuhimu wa kila raia kuilinda Katiba ya Nchi

Kumbuka Mwanasheria wa serikali pia anashiriki Bunge
Inawezekana Spika hana katiba katika desk lake maana kabla ya uamuzi wake huu angeweza kuisoma ibara hii ya katiba kwanza....!!

Ama kama sivyo, kuna uwezekana idara ya sheria na katiba ya taasisi ya Bunge ina vilaza watupu wa sheria...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama amekiuka Katiba si mchukue hatua kuliko kulalamika tu huku mtandaoni. Jamani inakera. Mahakama si zipo.

Hata kama upo kijijini patandi meru kusikufanye ushindwe kuelewa kwamba tayari CILAO wanakusudia kulipeleka hilo suala mahakamani ati. Walichofanya ni press release.
 
mnalaumu Spika bure tu....

fuatilia uone Nani kashika microphone
 
Kama amekiuka Katiba si mchukue hatua kuliko kulalamika tu huku mtandaoni. Jamani inakera. Mahakama si zipo.
Mahakama hizi zinazotoa hukumu kwa kupokea maelekezo kutoka juu
 
Mi binafsi niwapongeze hao CILAO Kwa kuweza kufuatilia kwa ukaribu na kutuelimidha juu ya haki za kiraia.

Mmewaaeleza waaandishi wavhabari kuwa pamoja na Cecil Mwambe kutangaza kupitia vyombo vya habari Ni wazi atakuwa ameshapoteza uanachama wa chama chake na kupoteza sifa ya kuwa mbunge...
Hakukuwa na mkutano wa kuidhinisha Mwambe kujivua uanachama kwa kuwa hakuomba ktk chama ili ahame. Kwenye video ya YouTube anasema kwa hiari yake ameamua kujivua uanachama na kuacha nadhifa zake zote ikiwa ni pamoja na UBUNGE. What else does Job want?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Roving Journalist,
CILAO wametimiza wajibu wao lakini hiyo mihimili mingine haina mizizi iliyojichimbia kwenda ardhini imebaki inaelea elea hewani, naamini mhimili wenye mizizi iliyojichimbia kwenda chini ndiyo utaibuka mshindi kwenye hiyo kesi tu.
 
Wananchi nao mazuzu....subiri 2020 election utaniambia
 
Wanaoshangilia haya sasa ni vipofu wasioona hatari nchi inalopelekwa. Chombo cha kutunga sheria kinafurahia uvunjifu siyo wa sheria tu bali Katiba ambayo wameapa kuihifadhi! Nafikiri ni ulevi usioelezeka wa madaraka.

Wanadhani wana uwezo wa kutenda watakavyo, lakini yatakapobadilika wengi wao watajuta. Kuna msemo wa kiswahili: ukionja asali utachonga mzinga au bandu bandu umaliza gogo. Just wait.
 
Spika alidai kuwa barua iliyotoka kwa katibu mkuu, kuwa mbunge amejivua uanachama, haikua na viambatanisho vya ushahidi!

Kama mbunge alijivua kwenye media, inafaa kuwa ni ushahidi?

Je, Katibu mkuu wa chama alikua na uhakika gani kama spika alishinda kwenye mitandao na kuona mbunge aliyejivua?
 
Wamezidi kutudharau sijui kwakua wao walishajitwalia umungu wa chato IPO siku .
 
Roving Journalist,
Wajulisheni kuwa Bunge haliendeshwi kwa kusikiliza vyombo vya habari vimetangaza nini kama Chadema hawakumjulisha Spika kuwa huyo mbunge uanachama wake wa Chadema umekoma basi Spika hawezi chukua maamuzi yoyote.

Chadema inaupungufu sana kwenye mambo ya administrative. Hii ni sawa na issue ya Lissu eti utetezi wao ulikuwa eti Spika anajua kwa sababu vyombo vya habari vinatangaza alipo. Hawa nao sheria hawaijui au wanataka wawaonyeshe wafadhiri wao kuwa wanafanyakazi.
 
Inawezekana Spika hana katiba katika desk lake maana kabla ya uamuzi wake huu angeweza kuisoma ibara hii ya katiba kwanza....!!

Ama kama sivyo, kuna uwezekana idara ya sheria na katiba ya taasisi ya Bunge ina vilaza watupu wa sheria...

..Katibu Mkuu wa cdm alimuandikia Spika barua akimweleza kuwa Cecil Mwambe siyo mwanachama wao tena.

..Spika ameikataa barua hiyo akidai haionyeshi kikao walichokaa CDM na kuamua kumfukuza / kumvua uanachama.

..Katibu Mkuu wa cdm amejibu kuwa hakukuwa na haja ya kuitisha kikao au kumuita Cecil Mwambe ktk kikao kwasababu aliamua kwa hiyari yake kuachana na CDM na kujiunga na CCM.

..Cecil Mwambe baada ya kusikia kuwa ameitwa na Spika, amesisitiza kuwa yeye ni mwana-CCM, lakini ameeleza kuwa ataitikia wito wa kwenda bungeni.
 
Ni kesi muhimu sana, tatizo Je , Tuna Makakama? Kuna Makahama Kuu yenye ubavu was kukataa "amri kutoka juu"?
Concern yangu ni hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bunge haliendeshwi kwa kufuata habari iliyotolewa kwenye vyombo vya habari. Kama Chadema hawakupeleka taarifa za kukoma kwa uanachama wake kwa Spika na Mkurugenzi wa Uchaguzi ili nafasi ya Ubunge itangazwe kuwa iko wapi mmeliwa. Chadema wengi ni mbumbumbu kweli wa kila kitu wamebaki na mapovu tuuu!!!
 
Back
Top Bottom