Usihangaike na mwanamke ambaye havutiwi nawe

Usihangaike na mwanamke ambaye havutiwi nawe

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Wanaume wengi huumia kwa kutokuzingatia vitu vya msingi linapokuja suala la mahusiano. Sababu hawajui wanachokitaka, wanachokifanya, hawana uzoefu. Na kuishia kuumia, kuwachukia, na kuwalaumu wanawake kwa mambo mengi.
Lakini ili kuepuka hayo, na wakati unatengeneza uzoefu kwenye suala la mahusiano, ni muhimu kuzingatia haya.
.
Usihangaike na mwanamke ambaye havutiwi nawe.
Wanaume wengi huangaukia hapa. Na kujikuta wanaishia kuchunwa au kuumizwa au kusalitiwa, sababu mwanamke hakua na mpango naye lakini amelazimisha sana.

Wanaume tumeumbwa kulazimisha vitu, kupambania vitu na kutafuta majibu ya vitu tusivyojua. Lakini linapokuja suala la mahusiano na mwanamke inabidi kuvaa vitu vingine tofauti na vya upambanaji wa maisha.

Sio kwa sababu umevutiwa na mwanamke fulani basi ni lazima naye avutiwe nawe, au ipo siku lazima umpate. Wapo wanaofanikiwa lakini kwa kuyalazimisha mapenzi.
Ndio maana tunaona ndoa nyingi zipo kimasilahi zaidi ya upendo.

Mwanamke unayempenda na unamfukuzia ni rahisi kukuacha.
.
Mpe nafasi mwanamke akufukuzie.
Ukishaachana na wasio kupenda.
Alafu ukakutana na ambaye anakukubali.
Sio sababu ya gari lako, hela zako, au mali tu bali sababu anakuhitaji wewe kwenye maisha yake basi usimrahisishie kazi kabisa ya kuwa naye. Usitake umuweke ndani mapema, acha upendo ukue taratibu.
Mpe nafasi na yeye akuthibitishie kuwa anastahili kuwa na wewe.
Mpe nafasi akufanyie vitu vizuri bila kumlazimisha.
Mpe nafasi akihitaji muda wake binafsi, sio lazima muda wote muwe pamoja. Pia hapa utajua ni wa aina gani.
Mpe nafasi upendo wake kwako ukue taratibu, sio kila siku umuambie akupende.
Mpe nafasi akuwaze mkiwa mbali, sio kila muda unamtafuta ili ujifariji kuwa upo naye.
Mpe nafasi akutafute kwa kuwa amekumisi, sio kumuuliza kila muda umenimisi baby?

Usimnyang’anye mwanamke zawadi ya kukufukuzia kwa kumrahisishia kila kitu. Wanataka changamoto na kuona kuwa wamelipambania pendo lako.

Mwanamke anayekupenda na kukufukuzia hawezi kukuacha.

Mvuto hauchagui, hivyo usiwe na wasiwasi kama kuna mwanamke atavutiwa na wewe. Wewe cha msingi hakikisha unajiweka katika hali ambayo hata wewe inakuvutia. Kisha weka nguvu zako kwenye malengo yako, mwanamke awe sehemu ya maisha yako na sio ndo maisha yako.
 
Hakuna mkate mgumu mbele ya chai, pesa ndio kiboko ya Wanawake.

Tutafute tu pesa jamani.
 
Back
Top Bottom