Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Achana na msemo kuwa "anakujaribu". Kama umejitahidi lakini yeye haoneshi kujali mahusiano, ujue unapoteza muda wako. Unatumika tu kupoteza muda. Pengine ana bwana wake anayempenda zaidi yako na anamjali kuliko wewe. Wapo wanawake ambao hawakukubali hata kama wewe ndiwe ungekuwa mwanaume pekee duniani.
Unapojitoa kwa mtu bila yeye kujitoa kwako, unajiumiza. Utaonekana hujiheshimu na hujakuwa. Pia unamzoesha huyo mtu kwamba, yeye hana haja ya kuhangaikia uwepo wako, anajua utakuja tu kwake au utajipendekeza tu.
Hatoona shida kukuendesha. Anajua kabisa huwezi kujiongoza, acha akupeleke anavyotaka. Mwisho wa siku, ukisema amekuumiza, unakua umekosea. Sababu kiukweli hakukuomba ujipendekeze kwake, ni wewe mwenyewe ulishindwa kujizuia.
Cha kufanya
Kuwa na mipaka na we mwenyewe.
Ujue ni wapi ukifikia unakua umejipendekeza.
Ujue ni wapi ukifikia unakua umeweka nguvu inavyostahili. Ili usijikute unaendeshwa. Sababu huna mipaka yako mwenyewe.
Kuna muda hautakiwi kukata tamaa.
Lakini juhudi zako lazima uone zina mwelekeo. Kama hazina matumaini/ mwelekeo ni heri uache na utafute kwingine.
Weka nguvu kwa wale wanaokukubali
Wapo wanaokukubali.
Wapo wanaotaka kuwa na wewe. Hao ndo uwaweke wa muhimu.
Ni rahisi kuelewana nao. Mahusiano yanakua rahisi.
Pia we mwenyewe badilika na ujiweke tayari kuwa na mtu mnaye-elewana.
Sababu unaweza mpata mtu rahisi kwako lakini ulishazoea vita huko nyuma. Hamtadumu.
Hivyo, jiheshimu na usikubali kuendeshwa/ kuburuzwa na mtu asiyekuelewa/ anayekunyonya.
Hakikisha mahusiano uliyopo mnaweka nguvu pamoja.