Usiichukulie poa Tanzania katika medani za kivita, walioijaribu walifutika

Tunahitaji kujipanga sana ,hiyo ni wake up call kwetu ,waziri wa ulinzi anatakiwa awe mwanajeshi na si mwanasiasa anayevaa sale za jeshi kama fashion
 
Hii Vita mmarekani ataingilia kati
 
Sasa hivi tukivamiwa mfano na Kenya, au Rwanda kwa uongozi huu wa kisiasa tunaweza kweli kupambana?
Wapambanaji ni walewale,vikosi ni vile vile,mbinu mpya,vijana wapya,damu mpya
JWTZ ukiichokonoa kidogo,inakufuata siyo chumbani tu,itainua hadi kitanda na kusaka hata mende na kunguni
Atakaegusa Tanzania,atafanywa kitu ambacho hadi vitukuu hawatosahau
 
Mission ilikuwa ya kulinda amani wao wakajipa mamlaka ya kuteka na kuwaua M23.
 
Na ndo hicho mlichofanya dhidi ya M23. Mliwaua lakini sasa wamerejea kwa kupata vijana wengine.
Nendeni mkaue na hao pia
 
Mkuu kwa Africa Tanzania ina rank ya ngapi kijeshi?
 
Na ndo hicho mlichofanya dhidi ya M23. Mliwaua lakini sasa wamerejea kwa kupata vijana wengine.
Nendeni mkaue na hao pia
M23 waasi hawa ni wa kizazi kipya walioasi jeshini baada ya wenzao wengine,ila wanatamba kwa sababu hawajapata mtu wa kuwafinya na kuwapa dozi kidogo,mbona watavua magwanda wakimbie,wakifinywa kidogo tu,watapotea
 
Vinyongo vya Banyamulenge havitomalizwa kwa risasi na mabomu. Sana sana mkifanya hivyo mtaendeleza uasi vizazi hadi vizazi kama kule ukanda wa Gaza!
Migogoro ya kijamii inamalizwa kijamii.
 
Vinyongo vya Banyamulenge havitomalizwa kwa risasi na mabomu. Sana sana mkifanya hivyo mtaendeleza uasi vizazi hadi vizazi kama kule ukanda wa Gaza!
Migogoro ya kijamii inamalizwa kijamii.
Inamalizwa kwa social science
 
Siyo kwa hawa wanajeshi wanywa gongo na wenye vitambi.
Mkuu usichukulie poa hili geshi letu.
Kuna mjeda mmoja maeneo flani alinipa maelezo namna walivyowatandika wale wa MKIRU hadi niliogopa.
 
Tupo vizuri sana...Embu tuingie Pale GOMA iwe kama kupiga Tizi ili Tutest ubora wetu
 
Sasa hivi tukivamiwa mfano na Kenya, au Rwanda kwa uongozi huu wa kisiasa tunaweza kweli kupambana?
Kwani si ni zama hizi hizi za uongozi unaouita wa kisiasa huuhuu kule
Mtwara kwenye border yetu na msumbiji Jeshi letu limefanya kazi iliyotukuka??
 
Vita inatusaidia nini?

Sisi tunataka maji
Katiba mpya
Watu wasitekwe
Rasilimali zetu zitumike vizuri
Kura zetu ziheshimiwe
Vijana wapate ajira
Elimu iwe bora
Afya na huduma njema

Hayo ndo tunayoyahitaji zaidi.
Hayo mambo ya vita siyo muhimu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…