Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hallelujah!
Bado nakusanya ripoti. Bado najifunza na nitaendelea kuwafundisha.
Kuna msemo maarufu usemao, usiingilie ugomvi wa wazazi, msemo huo upo kwenye level ya kifamilia.
Watoto wengi wanaoingilia ugomvi wa Baba na Mama hujikuta katika maisha magumu hapo baadaye kwa namna waijuayo au wasioijua.
Mbaya zaidi wazazi wanapopatana tena ndipo mtoto aliyekuwa na kiherehere hujikuta kwenye hali ya mgogoro na mateso.
Kisiasa,
Wananchi wengi hupenda kujiingizwa na wakati mwingine huingizwa na wanasiasa kwenye magomvi ya wanasiasa.
Unakuta ugomvi kati ya CCM Vs Chadema. Mwanachama wa kawaida tena asiye na maslahi ya vyama hivyo moja kwa moja. Hasa maslahi ya kiuchumi maana huo ndio msingi wa siasa.
Mwanachama wa kawaida au mwananchi shabiki huingilia magomvi ya kisiasa ya chama pale ambapo viongozi wa vyama husika wakiparangana.
Jambo ambalo mara nyingi huwaletea matatizo.
Haya unakuta ndani ya chama, kuna ugomvi wa viongozi. Labda Lisu Vs Heche, au Mwigulu Vs Makonda.
Mwanachama wa kawaida anajiingiza kwenye vita vya wakubwa. Na mara nyingi nyasi ndio huumia.
Msemo wa Farasi zikipigana zinazoumia ni Nyasi. Haimaanishi Nyasi za Dunia nzima. Nope! NI NYASI zinazojifungamanisha na Farasi hao.
Kila siku nasema, usiingie kwenye jambo lolote kama haunufaiki hasa kiuchumi.
Yaani isifike hatua ukajitoa uhai au ukatolewa uhai kwa jambo ambalo kwanza hukulianzisha wewe,
Pili, sio mmiliki wake,
Tatu, hunufaiki kiuchumi.
Mfano kuna watu wanakuambia nitakufa kisa Uislamu au Ukristo. Wakati haunufaiki kiuchumi katika dini hizo.
Yaani ugombane na mtu mwingine, mpigane kisa uislam aliouanzisha Muhammad, au Ukristo ulioanzishwa na Paulo kupitia Kristo. Watu ambao huwajui ma hutokuja uwajue kamwe.
Wanaporushiana maneno Wachungaji Vs Masheikhe waache waparurane. Ni kazi yao hiyo. Wanafaidika nayo wao.
Oooh! Uteteeni Ukristo. Kwani unalipwa? Sadaka na zaka unazotoa kuwalipa watumishi wa dini, wanaozichukua ndio wakapiganie huko.
Oooh! Teteeni dini ya uislam. Wewe uislam ukiharibiwa unadhurika wapi, kipato chako kinaguswa?
Msiwe na akili ndogo.
Wewe mtu akichafua kazi yako unaweza kuwaambia watu wapigane kwaajili yako wakafanya hivyo? Kama sivyo why wewe upiganie kazi za watu wengine?
Wewe tetea HAKI.
Ugomvi wa wakubwa watoto wasiuingilie.
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam