Usiishi na Mwanamke Mzuri kisasa. Mzalishe chapuchapu angalau watoto wawili, watatu. Huna hasara hata mkiachana

Usiishi na Mwanamke Mzuri kisasa. Mzalishe chapuchapu angalau watoto wawili, watatu. Huna hasara hata mkiachana

Babu Clifford (R I P)alikushauri kama vile sio binadamu mwenye conscience.

Imagine kuzaa watoto bila mpangilio ili eti kumfunga mama yao kwa mnyororo mfupi.

Pengine alishapata Safari lager zake mbili tatu au wewe ndio hukumuelewa.

Kutumia resources na fursa inaweza kuwa na tafsri nyingine kabisa ukiongelea jinsia ya ke.

R I P babu Clifford. Alikuwa rake moja hatari sana.

Huwezi kuwaelewa Watibeli mpaka matatizo yawakutage.

Alichoshauri Mzee Clifford ndicho nilichokiwasilisha tena kwa ufafanuzi tukuka
 
My dear utaangukia pua… maisha yanakutaka unadilike kulingana namuda unavyoenda… Maisha ya sasa sio kama zamani baba anakaa balazani analetewa kahawa na mkewe. Nowadays wanawake wanapambana kutokaa ndani.. uyo wa kumzalisha hvyo bila future atakua jinga na uzazi wa mpango umejaa bure 😆😆😆

Wanawake wa zamani nao walikuwa wanapambana. Siku hizi ndio wavivu.
Tofauti ni Kuwa zamani walikuwa hawana haki ya kumiliki Mali sasa hivi wanahaki.

Nilichoandika ni muhimu kwa ambao wanataka uwezekano na faida za mapema na uhakikisho.

Ni hasara uwe na mwanamke mzuri kisha muachana na haukumtumia vizuri. Mojawapo ya matumizi sahihi ya mwanamke ni kuzaa watoto.

Sasa unaishi na mwanamke kama mdoli Siku amekuacha utalia kama lijinga. Uliwahi kuona wapi MTU kamzalisha mwanamke watoto wengi alafu akalialia Siku wakiachana?
 
Umejibu vizur sana
Jau sana hawa jamaa.

Shida ya watu dizaini ya Robert Heriel Mtibeli ni kua wanakutana na watu walewale kila siku, sio mtu wa vyombo, hali kaya, hakai vijiweni, hana biashara inayomkutanisha na watu tofauti tofauti na kutoa idea zake vitabuni na youtube videos.

Hizo pisi anazionea wapi??

Oya vitoto vya bukubee vikali ni vingi na haviishi, ushindwe wewe tu, mtibeli atavizalisha hata buku maana ni rahisi kuvipata na kuvimudu.
 
Jau sana hawa jamaa.

Shida ya watu dizaini ya Robert Heriel Mtibeli ni kua wanakutana na watu walewale kila siku, sio mtu wa vyombo, hali kaya, hakai vijiweni, hana biashara inayomkutanisha na watu tofauti tofauti na kutoa idea zake vitabuni na youtube videos.

Hizo pisi anazionea wapi??

Oya vitoto vya bukubee vikali ni vingi na haviishi, ushindwe wewe tu, mtibeli atavizalisha hata buku maana ni rahisi kuvipata na kuvimudu.

Sasa mtoto wa 2000 Mimi niwapeleke wapi?
Michezo ya ujana mara ya mwisho nimeifanya mwaka 2016 ambapo hao watoto wa 2000 walikuwa na miaka 16(wadogo).

Hao nimewaachia ninyi na kina min -me.

Kazi zangu niza kimataifa. Vitoto vya Kiswahili ambavyo hata buku ya vocha havina Kwa kweli hata vingekuwa vizuri kama Malaika huwaga sivutiwi kabisa
 
Sasa mtoto wa 2000 Mimi niwapeleke wapi?
Michezo ya ujana mara ya mwisho nimeifanya mwaka 2016 ambapo hao watoto wa 2000 walikuwa na miaka 16(wadogo).

Hao nimewaachia ninyi na kina min -me.

Kazi zangu niza kimataifa. Vitoto vya Kiswahili ambavyo hata buku ya vocha havina Kwa kweli hata vingekuwa vizuri kama Malaika huwaga sivutiwi kabisa
Kaka wewe kwa mwanamke unataka nini??
Unataka akutumie vocha?

Mtibeli unaniangusha ujue..
Mkeo anajua hii Id yako hapa jf?

Mliooa mna mtazamo tofaut juu ya pisi.
 
Kaka wewe kwa mwanamke unataka nini??
Unataka akutumie vocha?

Mtibeli unaniangusha ujue..
Mkeo anajua hii Id yako hapa jf?

Mliooa mna mtazamo tofaut juu ya pisi.

Mimi mwanamke kwangu ni msaidizi sio mzigo.
Sifa ya mwanamke wangu ipo kwenye mithali 31 sura yote.

Watibeli hatunaga kuficha tupo wazi Sana. Mke na ndugu wote waliopo mtandaoni wanaijua ID hii na wanaisoma.

Bahati nzuri ni mambo ambayo hawayashangai kutoka kwangu coz wanajua falsafa zangu.
 
Sasa mtoto wa 2000 Mimi niwapeleke wapi?
Michezo ya ujana mara ya mwisho nimeifanya mwaka 2016 ambapo hao watoto wa 2000 walikuwa na miaka 16(wadogo).

Hao nimewaachia ninyi na kina min -me.

Kazi zangu niza kimataifa. Vitoto vya Kiswahili ambavyo hata buku ya vocha havina Kwa kweli hata vingekuwa vizuri kama Malaika huwaga sivutiwi kabisa
Dogo wa kihurio tulia tu utazeeka kama mimi , wala usiwe na haraka
 
Mimi mwanamke kwangu ni msaidizi sio mzigo.
Sifa ya mwanamke wangu ipo kwenye mithali 31 sura yote.

Watibeli hatunaga kuficha tupo wazi Sana. Mke na ndugu wote waliopo mtandaoni wanaijua ID hii na wanaisoma.

Bahati nzuri ni mambo ambayo hawayashangai kutoka kwangu coz wanajua falsafa zangu.
Mkuu kunywa pepsi asee, wale watoto hawana future kabisa.. mi nikishaona mtu kanitext hv namkataa … ety ‘’xaxa unajua xio xawa m xtak’’ 😅😅😅
 
Kikubwa nawashaur watu, zaa kwa mpango, panga na mkeo sio kila tendo ni mimba mtakosa starehe😅😅.
Jipeni muda wa kufurahia tendo jmn ndyo ndoa yenyewe hioo😆

Cha pili usisaau hata mzazi wewe una ndoto zako, so zaa watoto unaoweza kuwamudu na kuendelea kujimudu wewe pia.
 
Babyface, tako kubwa, mguu wa bia, chuchu konzi, rangi ya mtumee🫠
Sidhani km kuna mwenye vyote😃😃😃
Lzm kuna kimoja atakosa ila ukichunguza sn

Bahati mbaya wengi utaona anampendea mtu kitu kimoja tu , the rest hana mpango navyo...

Kuna mtu ye tako tu , hajali sura wala kitu kingine...meingine sura tu , mwingine rangi, mwingine miguu, mwingine wembamba ...😃😃😃
 
Nyie vijana wadogo GEN Z hamjui Maisha mna less life experience.

Mwanamke wa kumzalisha haraka haraka ni yule mwenye akili kubwa kichwani .

Kwakuwa atakuwa na uwezo wa ku-secure future ya watoto wenu .

Kigezo cha uzuri sio kigezo pekee cha kuzaa na MTU

Au kumpa mbegu yako ni hatari
Jamaa yangu manyaunyau niambie bhana! Ulipotea wapi?
 
Sidhani km kuna mwenye vyote😃😃😃
Lzm kuna kimoja atakosa ila ukichunguza sn

Bahati mbaya wengi utaona anampendea mtu kitu kimoja tu , the rest hana mpango navyo...

Kuna mtu ye tako tu , hajali sura wala kitu kingine...meingine sura tu , mwingine rangi, mwingine miguu, mwingine wembamba ...😃😃😃
Hivi huwa vinasaidia nini katika mahusiano?
 
1. Sitachoka kuwafundisha ninyi vijana. Maana wengi wenu hamkuishi na Wazee nazungumzia wazee waliozaliwa kabla ya mwaka 1940. Hao ndio Wababu.

2. Mtibeli nilibahatika kuishi na Wazee waliozaliwa miaka ya 1920-1945. Nikajifunza baadhi ya issues kutoka kwao. Na bahati nzuri walikuwa rafiki zangu. So nje ya kupenda kusoma pia nimejua baadhi ya ishu kwa kukaa na wazee.

3. Ninaheshimu Wazee kwa uzoefu wao wa maisha. Haimaanishi nilikubali Kila walichoeleza.

4. Moja ya Falsafa nilizojifunza kutoka kwao. Mzee wangu Mmoja aitwaye Clifford Tenga ambaye sasa ni Marehemu, tukiwa kwenye matembezi katika kijiji cha Kisiwani, Wilaya ya Same. Katika Stori akaniambia;

5. Ukioa mwanamke mzuri usimkawize, mzalishe watoto angalau wawili watatu chapuchapu. Nikamuuliza kwa nini?

6. Akaniambia, akijibu kama Mwanasiasa, kwani alikuwa Diwani wa kata ya Kisiwani kupitia CCM. Akasema, Resources lazima uzitumie vilivyo. Na fursa usiyo na uhakika nayo lazima uhakikishe unaitumia kikamilifu.

7. Bado Namsikiliza. Hapo nilikuwa kidato cha tano Likizo. Nimeenda Kumsalimia Babu Clifford.

8. Akaendelea, Mwanamke Mzuri ni kama rasilimali nyeti ambayo wanaume wengi hupambana kuipata. Unapomiliki mwanamke Mzuri usimkawize. Usiishi naye kwa akili ya kuwa atakuwa wako Milele. Kwa namna hiyo use her effectively.

9. Mzee tulipiga stori nyingi Sana lakini hiyo Leo nimeikumbuka. Na nimeamua kushiriki nanyi kwa ambao wataona waitumie hewala.

10. Kanuni hii sisi Watibeli tunaitumia. Watibeli hatunaga Hasara kwa sababu tunajua wakati na jinsi ya kutumia rasilimali.

11. Mapenzi kwetu ni kama kunywa Uji wa vuguvugu. Yaani shwaaa! Kwa sababu hatuishi kwa hisia bali tunaishi kwa Kanuni.

12. Ndio Maana Leo mimi Mtibeli, nakuambia kijana wangu. Utakapopata mwanamke Mzuri. Mwenye hadhi, cheo, au msomi. Akaingia kwenye 18 zako.

13. Jua, it's your turn, ni zamu yako. Na muda wa kudumu naye itagemea how you play your balls. Nitakurahisishia kazi hapa.

14. Elewa mwanamke hisia zake zinaenda kwa kubadilika. Hivyo usizitegemee hisia zake kama nguzo kuu ya mapenzi na uhusiano wenu. Anavyokupenda Leo na kukuona Leo sivyo atakavyokuwa hivyo miaka mitatu au mitano ijayo.

15. Kwa kujua hilo, unatakiwa kuongeza ziada ya hisia zake. Ziada hiyo ni utegemezi usiovunjika kirahisi.

16. Utegemezi na connection isiyovunjika kirahisi. Hapo ndipo kumzalisha watoto inapokuwa mbadala wa hisia zake.

17. Mwanamke kadiri unapompa mzigo wa watoto ndivyo anavyopoteza ramani ya kujua akuache vipi.
Hisia hata zikiisha, sasa atawaza watoto wangu (wenu) itakuwaje? Mtoto mmoja kwa mwanamke sio tatizo anaweza kukuacha mapema tuu ingawaje pia atafikiri mara mbilimbili.

18. Mwanamke Mzuri unapomzalisha watoto wawili watatu. Kiukweli hauna hasara. Kama ni biashara imelipa. Umejua kutumia resources vizuri.

19. Muda sahihi wa kumzalisha mwanamke watoto. Ni kipindi hisia zake zipo juu Sana kwako na kipindi ambacho hajapata uhalisia wa maisha.

20. Iko hivi wanawake wengi wanapenda kuzaa watoto wengi, yaani kuanzia wanne. Hilo weka kichwani. Wanawake hupenda kuzaa na mwanaume mmoja tuu.

21. Katika umri chini ya miaka 25 wanawake wengi bado hawajakomaa kujua uhalisia wa maisha. Hivyo suala la kuzaa watoto hulichukulia kirahisi.

22. Usiishi kisasa na Mwanamke mrembo. Utaumia Mzee. Leta uzungu kwa mwanamke mzuri alafu huyo mwanamke akutane na Sisi watibeli. Tunambomoa utashangaa mimba zinaingia na kuzaa kama sungura.

23. Mwanamke ukishaishi naye. Miaka Ile mitatu kwenda minne ya mwanzo hakikisha tayari unawatoto wawili.
Hiyo ni kutengeneza uwezekano na uhakilka kwa sehemu kubwa.

24. Hapo yeye ndiye atawaza familia said hasa kuwahusu wewe mumewe, watoto wenu na yeye. Wakati wewe kwa kusogeza kete hiyo utakuwa unawaza kutafuta pesa na kutunza familia.

25. Pressure kubwa itakuwa kwake kwamba akifanya ujinga akavunja ndoa tayari anawatoto wawili watatu. Ninakuhakikishia sio rahisi mwanamke kuvunja nyumba akiwa na watoto wawili watatu. Yaani mpaka uwe umefanya Jambo kubwa Sana tena kwa muda mrefu.

Na sio Ile ya ati amedanganywa na wanaume wa mjini. Nani alikuambia mwanamke anadanganywa? Hawadanganywi Bali wanawake hufanya mambo Yao wakiws tayari wamesha calculate faida na hasara. Na wapo tayari kwa matokeo.

26. Ukishaona mwanamke mzuri anakuambia anahofu ya kuzaa na upo naye. My friend kuna sehemu umefeli pakubwa. Tayari akili zake zimerejea. Kikawaida mwanamke akikupenda na akiwa na hisia na lile wenge la Kwanza kwako haoni shida kuzaa watoto wengi.

Na Sisi wanaume ndio tunakuwa na hofu ya watoto kutokana na kuangalia hali ya maisha. Kwamba utawaleaje watoto wakati uchumi haujakaa vizuri.

27. Hiyo kwako ni fursa ambayo hutakiwi kuiacha ipite. Hata kama unamaisha magumu kiasi gani. Ukiwa na mwanamke mzuri unayempenda Sana akawa na kiu ya kuzaa watoto wengi. Usiogope zaa. Wakifika wawili au watatu hapo stop kidogo ndio unaweza kufikiria ugumu.

28. Hiyo ni fursa kwako isiyojitokeza mara mbili. Usiwe wale wanaume wa ngoja mambo yakae Sawa ukiwa mbele ya mwanamke mrembo. Hakuna cha mambo kukaa sawa. Mpe anachotaka. Utamuelewa baadaye. Wanawake warembo hawapendi wanaume waoga wa maisha na majukumu. Yaani uogope kuwatunza watoto wawili au watatu?

29. Oooh! Tayari tunamtoto mmoja. Acha nijiendeleze kielemu. My friend kama mwanamke wako ukimtazama hivi unamuona ni Kifaa, kisu, pisikali iliyonyooka. Achana na mambo ya kisasa kwa muda ila tumia akili Sana.

30. Bahati nzuri ada utatoa wewe. So unamuambia atasoma mwaka huu. Ikifika tarehe za kulipia vyuoni hata kama unahela Fanya mambo yanaingiliana.

Mpe moyo kuwa lazima atasoma huku ukimpenda na kumfanyia mind games. Mtie mimbia ya pili. Akishajifungua mtoto wa pili. Mshukuru, mpe na pesa kabisa kama zawadi.

31. Kisha wakati wa chuo. Mpe hela ya usajili na ada kabisa aparangane mwenyewe.

32. Mwanamke mzuri aliyekuzalia watoto kuanzia watoto wawili - watatu. Huyo hauna hasara. Lakini kama ndio mtoto mmoja au hauna kabisa, lazima roho ikutoke.

33. Mapenzi kwa vijana wa miaka 20-30 ni mchezo wa kuviziana kama Draft tuu. Mwanamke anamvizia mwanaume vivyohivyo kwa mwanaume kumvia mwanamke. Ni umri wa kutokuwa na uhakika na uwezekano. Hivyo unatakiwa kucheza kete zinazokupa uhakika na uwezekano mkubwa. Hata kama deal likifa bado unafaida kwenye mchezo.

34. Kwa kijana ukishakuwa na watoto wawili watatu kwa mwanamke mmoja. Asilimia kubwa matatizo ya mwanamke hayatakuwa kwenye mambo ya kuangalia wanaume wengine huko. Kwani ushamuwekea Msalaba. Kiburi cha mwanamke kinaenda chini.

35. Malalamiko yandoa kwa wanawake wenye watoto wawili watatu husababishwa na wanaume kutokuwa waaminifu huku mwanamke akiwa analinda zaidi familia yake kwa maslahi ya watoto

36. Wanawake wakishakuwa na watoto wawili kuendelea plan zao hubadilika. Mbinu za kivita zinabadilika. Wanajipanga kwa vita ya baadaye.

37. Wengi husema nasubiri watoto wangu wakue alafu huyu mwanaume nitamnyoosha. Hapa ni kama mwanaumee alikuwa mkandamizaji na anayemdhulumu mkewe.

38. So ukiwa umemzalisha mtoto wawatu watoto wawili watatu kuendelea. Sio sababu ya kumkosea na kumdhulumu haki yake. Unafanya hivyo kwaajili ya kulinda himaya na maslahi yako Kwa future kama unampango wa kuishi mpaka uzee na mkeo mzuri.

39. Kama unamtesa mkeo jiandae kwa vita ya pili muda usiotarajiwa hasa baada ya watoto kukua.

40. Kwa Watibeli hatuwezagi kutesa Wanawake zetu. Ingawaje tunajua njia za kujihami endapo itatokea ukaoa mwanamke atakayeanzisha vita vya uzeeni dakika za jioni.

Kufikia hapo sina la ziada.

TaikonMaster
Kwa Sasa Dar es Salaam
Wewe umeoa? una ngonjera sana mdau
 
Back
Top Bottom