Usijaribu kukaa na ndugu zako kwenye familia yako, utajuta!

Usijaribu kukaa na ndugu zako kwenye familia yako, utajuta!

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
16,911
Reaction score
28,469
Sio kwamba nina roho mbaya, hapana. Ila nimeona niwaambie tu.

Unapokuwa umeoa kaa na mkeo na watoto wako.

Hayo mambo ya kujazana ndani sijui mjomba sijui kaka ako sijui bamdogo, hayafai. Trust me, hata Dada zako (mawifi) tena hao ndo hawafai.

Nilipowaleta nyumbani watoto wa kaka zangu wawili nikawasomesha. Nami nina watoto wawili na mke. Jumla hapo wanne.

After that akaja sasa kaka yangu mmoja wa mwenye mtoto hapo akakaa alishaachana na mkewe na hajulikani yuko wapi.

Baada ya muda watoto wamemaliza la 7 wa kwake akafeli na wangu wakafaulu, shida ikaanzia hapa.

Ooh Mara umewasomesha watoto wako vizuri ndo maana wamefaulu sijui watoto wa ndugu zako huwasomeshi vizuri. Dah! wakati wote niliwapeleka shule moja.

Watoto wale wakaaanza nipakazia kwa baba zao (kaka zangu ) kuwa Mimi ndo nifae kulaumiwa kwa wao kufeli ..hii ishu ikafika kwa wazazi nyumbani wakanisema sana.

Nikaona ushenzi huu nikatimua ile mitoto na baba ake nikafurumusha nibaki na familia yangu pumbavu kabisa.

Mema yote hiyo ndo shukrani? Walishaanza kumsema na mama p mke wangu mambo ya kijinga.

Sitaki hata kuwasikia tena nitakuwa na wazazi tu huo undugu na hao wapuuzi ufe tu nitazikwa tu watu

Ujana wote huu nimekuwa na majukumu kama mzee? Kisa wao?
 
Hii ni kitu common sana. Na inasumbua mno. Pande zote huwa na shida. Kuna wengine wana treat watoto wa ndugu vibaya na kuna watoto wa ndugu na wazazi wao wasio na shukrani hata uwafanyie nini.
Kila mtu abebe mzigo wake, na kama ni msaada wasaidiwe hukohuko.
 
Mkuu nimeexperience hii kitu na kibaya zaidi hawana shukrani yani huwa hawakumbuki ulikowatoa. Binadamu anapanga yake asijue Mungu alishapanga yake best revenge nilijiapiza hawatokuja kunipita kimaisha kamwe najivunia nimewaacha mbali afu umri wao ni 40 na kuendelea hahaha mtegemea vya nduguze!?
 
Pole kiongozi, ni vyema umepata funzo mapema wamekuepusha na mengi na usirudie tena, kikubwa hakikisha unawategemeza watoto wako.

Afu huyo kakaako fala sana ni wajibu wake kuwasomesha watoto wake kwahio hata kama wakwako ungewapeleka shule ya maana halafu wakwake shule za serikali bado hapaswi kukulaumu.
 
Pole kiongozi, ni vyema umepata funzo mapema wamekuepusha na mengi...na usirudie tena, kikubwa hakikisha unawategemeza watoto wako. Afu huyo kakaako fal.a sana ni wajibu wake kuwasomesha watoto wake kwahio hata kama wakwako ungewapeleka shule ya maana halafu wakwake shule za serikali bado hapaswi kukulaumu
Cha ajabu wore walikuwa wanasoma shule moja hiyo hiyo
Kosa langu lilikuwa wapi?
 
Hii ni kitu common sana. Na inasumbua mno. Pande zote huwa na shida. Kuna wengine wana treat watoto wa ndugu vibaya na kuna watoto wa ndugu na wazazi wao wasio na shukrani hata uwafanyie nini.
Kila mtu abebe mzigo wake, na kama ni msaada wasaidiwe hukohuko.
Nakuunga mkono kabisa
Kabla hayajanitokea haya ningekupinga

Ila sasa nimeanza kuelewa vizuri
 
Dduuhh pole sn mkuu.

Inafika mahali tuishi tu maisha ya kizungu.

Km una ndugu au jamaa unataka kusaidia wasaidie huko huko mwakwao walipo..... waswahili badala ya kupata thawabu watakupatisha dhambi
Kwa sasa nimepanga kuwa na roho mbaya sanaa sijui mtoto wa kaka sijui nani piga chini kmk

Tunajinyima halafu bado wanatuona tuna roho ya korosho
Kila MTU alee shahawa zake
 
Kwahiyo mkuu unataka kutwambia shule za serikali siyo za maana? Au unatumiwa na mabeberu wewe[emoji2]

Back
Top Bottom