Usijaribu kukaa na ndugu zako kwenye familia yako, utajuta!

Usijaribu kukaa na ndugu zako kwenye familia yako, utajuta!

Ni kweli undugu ni kazi lakini tunatakiwa tuwe na dhana ya kutenda wema uende zako. Ulichokifanya kwa kujitoa kusaidia hao watoto halafu wao wakabweteka kuliko hata wanao na kupelekea kufeli masomo sio haki yako kulaumiwa hata kidogo.

Kinacholeta shida ni watu kudhani kwamba wanapewa misaada na ndugu ni haki kumbe ni hisani kama zilivyo hisani nyingine. Mimi nina wadogo zangu na wajomba lakini huwa sipepesi macho, napiga vikao kila napojisikia na huwa nawapa zoezi la kuandaa agenda na mimi kuziboresha.
Na kupitia vikao hivyo nimekuwa nikiwaambia kabisa kwamba wao hawana haki ya kuishi kwangu isipokuwa nimewaonea huruma kwa hiyo ataezembea kukazania kile kilichomleta kwangu muda wake ukiisha, anasepa with nothing akasimlie vizuri utalii aliouona, halafu umri wa maisha halisi ukimfika atakumbuka na kujiambia mwenyewe huko, jinga kabisa!!.

Nashukuru Mungu madogo wanatusua kila level na wamekuwa kama waongoza njia kwa watoto wangu nao wanatamani kuwa kama wao.
 
Sikatai mkuu
Nakumbuka sana kaka yangu nilipopigwa alikuja kunisaidia, aliwahi nitengenezea manati nijilinde shuleni
Nakumbuka sana,
Shida hapa ni waligeuza wema kama msumari To stab in my back

Mbaya zaidi wanaona kama ni haki yao wewe kuwasaidia, msaada ni hiyari unaweza kutolewa ama usitolewe
 
Ntaishi na mtoto wa mtu pale inapobidi mzazi kafariki hakuna wa kumtunza na lazima afuate masharti yangu vinginevyo ntatoa msaada akiwa kwa mzazi wake huko huko na kama nna uwezo wa kufanya hivyo.
 
Kiukweli familia nyingi za kiafrika zimebebana.Wewe ulieanzisha mada hii inawezekana unatoka kwenye spoon family. Wajomba,mashangazi,baba mdogo nk wamefanya kazi kubwa kuinua familia nyingi. Wakina dada wengi watoto wao wamelelewa ujombani baada ya kukataliwa na baba zao. Wengine Wana madaraka makubwaka na vyeo .
 
Back
Top Bottom