stabilityman
JF-Expert Member
- Jul 9, 2024
- 857
- 1,810
MAANA YA SETBACK KWA LUGHA RAHISI
Setback ni nafasi ya wazi ambayo lazima uache bila kujenga kati ya nyumba yako na mpaka wa kiwanja chako.
Mfano rahisi kama hauna elimu ya ujenzi:
Fikiria kiwanja chako ni karatasi. Halmashauri inakuchorea mstari ndani ya karatasi hiyo. Inakuambia: "Jenga ndani ya mstari huu tu. Nje ya mstari huu usijenge chochote".
Nafasi iliyoachwa kati ya mstari huo na ukingo wa karatasi ndio setback.
Kwa nini unatakiwa kuacha hiyo nafasi? Sababu 5 za msingi:
1. Moto usienee
Nyumba zikigongana, moto ukiwaka moja unaunguza zote. Nafasi hiyo inasaidia zimamoto kupita.
2. Hewa na mwanga
Nyumba yako ipate upepo na mwanga wa jua. Isiwe gizani mchana kutwa.
3. Faragha
Jirani asikuangalie chumbani kupitia dirishani. Wewe usimwone yeye anaoga.
4. Matengenezo
Ukuta ukipasuka, fundi apate pa kupita kuukarabati. Bomba likipasuka uweze kuchimba.
5. Barabara na huduma
Serikali ikitaka kupanua barabara au kupitisha bomba la maji lisibomoe nyumba yako.
Mfano wa namba:
Kiwanja chako kina upana wa mita 20.
Sheria inasema acha setback ya mita 1.5 kila upande.
Maana yake: 1.5m kushoto + 1.5m kulia = 3m imepotea.
Umebakiwa na mita 17 tu za kujenga nyumba.
Kwa kifupi: Setback = "Usiingilie jirani, usizibe njia, jiachiwe nafasi ya kupumua".
Ukienda kujenga, muulize fundi: "Nionyeshe mipaka ya setback kwenye ramani". Asipojua, tafuta mwingine.
SETBACKS ZA KUZINGATIA UNAJENGA NYUMBA
1. Setback mbele kuelekea barabara: 3m hadi 6m kwa nyumba ya kawaida. 6m hadi 9m kwa ghorofa.
2. Setback nyuma: 3m kwa nyumba ya kawaida. 4.5m kwa ghorofa.
3. Setback kando kushoto na kulia: 1.5m hadi 3m kwa nyumba ya kawaida. 3m hadi 4.5m kwa ghorofa.
4. Barabara kuu ya TANROADS: 15m hadi 45m kutoka katikati ya barabara.
5. Nyaya za umeme za high tension: 15m hadi 30m kutoka nguzo za TANESCO.
6. Mto/Korongo: 60m kutoka mto mkubwa, 30m kutoka mto mdogo.
7. Bahari: 60m kutoka ukingo wa bahari.
8. Reli: 30m kutoka katikati ya reli.
9. Kiwanja cha kona: Pande 2 zinazoelekea barabara zote acha 3m hadi 6m.
10. Fence/Ukuta: 1.5m kutoka mpaka wa barabara kuu.
11. Septic tank/choo cha shimo: 3m kutoka mpaka wa jirani na 1.5m kutoka jengo lako.
12. Kisima cha maji: 30m kutoka septic tank na choo.
13. Paa na balcony: Haziruhusiwi kupita mpaka wa kiwanja wala kudondosha maji kwa jirani.
14. Dirisha la kando: Kama umbali ni chini ya 3m kutoka mpakani, usiweke dirisha linaloangalia moja kwa moja kwa jirani.
15. Njia ya gari/garage: Acha 5m kutoka geti hadi barabara.
16. Njia ya dharura: Acha 3m kuzunguka jengo kwa ajili ya zimamoto na ambulance.
17. Miti mikubwa: Acha 3m kutoka jengo ili mizizi isiharibu msingi.
18. Buffer ya usalama: Ongeza cm 30 zaidi ya setback ya kisheria ili kuepuka kuvunjiwa ukikosea kipimo.
19. Hewa na mwanga: Acha nafasi ya kutosha kati yako na jirani ili vyumba vipate mwanga na hewa.
20. Matengenezo: Acha nafasi ya fundi kupita kufanya matengenezo ya ukuta wa nje.
Kumbuka: Nenda Halmashauri/Idara ya Mipango Miji kuchukua Site Development Conditions za kiwanja chako kabla hujajenga.
ENG JAMES 0743257669
KWA UJENZI NA RAMANI ZA NYUMBA NICHEK