Usijivune: Kassim Majaliwa, Prof Mark Mwandosya na marehemu Prof Idris Mtulia, Wakiwa ndani ya Mtumbwi

Usijivune: Kassim Majaliwa, Prof Mark Mwandosya na marehemu Prof Idris Mtulia, Wakiwa ndani ya Mtumbwi

Hii michezo ya kuigiza kwenye mitumbwi ni hatari sana,mto rufiji sio kufanyia maigizo kabisa.
Huo mto una mamba wengi sana niliwahi kuzama ziwani sina hamu na hiyo mitumbwi
Ukiongea habari ya kuzama majini hadi mwili unasisima, nimewahi kunusurika wakati nina miaka 12, nusura nisepe.
 
Picha hii ni ya mwaka 2010, yaani miaka nane iliyopita. Wa tatu kwa waliokaa kutoka nyuma ni Kassim Majaliwa ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji. Majaliwa hakuwa hata mbunge wakati huo.

Nyuma ya Majaliwa ni Prof Mark Mwandosya ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, asiye na Wizara Maalum. Na nyuma ya Mwandosya ni aliyekuwa Mbunge wa Rufiji, Prof Idris Mtulia (marehemu).

Katika Uchaguzi Mkuu mwaka huo, Majaliwa alichaguliwa kuwa mbunge na baada ya hapo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, akishughulika zaidi na upande wa elimu.

Miaka mitano iliyofuata Majaliwa akawa Waziri Mkuu. Ukiangalia picha hii unapata jawabu kuwa hakuna ambaye alikuwa anawaza kama Majaliwa ni Waziri Mkuu baada ya Mizengo Pinda.

Hapo Majaliwa alikuwa akionekana mwenye cheo kidogo tu, Mkuu wa Wilaya. Pichani anaonekana ni mtu mnyonge tu, mnyeneyekevu mbele ya wezake.

Majaliwa wa leo huwezi kumpandisha kwenye mtumbwi hivyo, maana ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika ofisi yake kuna kila aina ya usafiri bora ambao unaweza kumfikisha popote, tofauti na mtumbwi huo ambao unaona kuupanda ni kama vile kuhatarisha maisha.

Majaliwa ana ndege yake kama Waziri Mkuu, ana helikopta na magari. Majaliwa wa leo hawezi kuvuka Mto Rufiji kwa mtumbwi hivyo, helikopta itamvusha.

POKEA ELIMU HII

Mwenye kibali cha kuyafahamu maisha yanayofuata kwa kila binadamu ni Mungu tu. Mungu alijua Majaliwa ni Waziri Mkuu baada ya Pinda, ila watu wengine wote kwenye mtumbwi huo akiwemo nahodha na Majaliwa mwenyewe hakuna aliyeifahamu siri hiyo.

Picha hii inafundisha watu kuwa wanyenyekevu katika maisha yao. Unaweza kumdharau mmachinga anayekubembeleza kununua bidhaa zake lakini miaka inayofuata ndiyo akawa Rais.

Ukijiona umebarikiwa kwa maisha fulani usiongeze tambo, bali mshukuru Mungu na uwe mnyenyekevu. Unaweza kumdharau housegirl nyumbani kwako, baadaye akawa Rais mwanamke au mke wa Rais, na mkamwita First Lady kisha barabarani mkapanga foleni kwa kuzuiwa na traffic, maana First Lady anapita.

Si mnasema kupanga ni kuchagua? Basi mpangaji ni Mungu na yeye ndiye humchagua amtakaye. Anaweza kumchagua kumwinua mtu ambaye wewe unamchukia kupita kiasi, acha chuki. Anaweza kumchagua unayemdharau, hebu acha dharau. Anaweza kumchagua unayemwonea na kumnyanyasa kwa unyonge wake, tafadhali usionee wenzako.

Ishi maisha ambayo yatakufanya uwe huru leo na kesho. Tenda wema na kama huwezi basi usitende ubaya. Usipomtendea mtu ubaya utakuwa huru kila siku. Na utatabasamu kwa mafanikio ya kila mmoja. Ukiwa mwovu, kuna watu wakifanikiwa utaona wanaifanya dunia yako iwe chungu.

FB_IMG_1538374925105.jpeg
 
Huyu ni Samwel Doe aliyekuwa Rais wa Liberia. Huyu alikuwa Dikteta na mbabe kwa raia wake na kuwadharau viongozi wenzake na wale waliokuwa wakipinga mawazo yake.
Huyu hakuwa na mawazo ya mtoa mada kuwa Mungu ndiye apangaye maisha ya baadae. Jee wangapi wakipata madaraka nao wanakuwa kama Doe? wanajua nini kinaweza kuwapata kwa tabia za aina hiyo. Kama wapo basi wajifunze,
Doe.jpg
 
Afavyo mbwa ndivyo Afavyo binadamu!
Ni ubatili na kujilisha upepo.

Ukiwa Rais haimaanishi huta kufa! Utakufa tu!

Jiheshimu ungali hai uheshimiwe kabla na baada ya kufa.

Watu hawa hata wakisema uongo dhahiri, ukiwanukuu unakuwa mtuhumiwa ghafla!

Hakuna wanachoweza kujivunia zaidi ya sura zao (mmoja mmbayaaaa swaiba beautiful)
 
Huyu ni Samwel Doe aliyekuwa Rais wa Liberia. Huyu alikuwa Dikteta na mbabe kwa raia wake na kuwadharau viongozi wenzake na wale waliokuwa wakipinga mawazo yake.
Huyu hakuwa na mawazo ya mtoa mada kuwa Mungu ndiye apangaye maisha ya baadae. Jee wangapi wakipata madaraka nao wanakuwa kama Doe? wanajua nini kinaweza kuwapata kwa tabia za aina hiyo. Kama wapo basi wajifunze,
View attachment 882986


Kuna watu wakipata madaraka wanaona ndio maisha yao yatakua hivyo mpaka mauti kwahiyo wanatesa watu tu. hawajui kama kuna siku na wao watateswa
 
Ajuae kesho ya mtu ni Mungu mwenyewe. Usimdharau yoyote.. hata kama una pesa zaid yao
 
Huyu ni Samwel Doe aliyekuwa Rais wa Liberia. Huyu alikuwa Dikteta na mbabe kwa raia wake na kuwadharau viongozi wenzake na wale waliokuwa wakipinga mawazo yake.
Huyu hakuwa na mawazo ya mtoa mada kuwa Mungu ndiye apangaye maisha ya baadae. Jee wangapi wakipata madaraka nao wanakuwa kama Doe? wanajua nini kinaweza kuwapata kwa tabia za aina hiyo. Kama wapo basi wajifunze,
View attachment 882986
Ujumbe ufike pale kwa ndugu jiwe
 
Kuna watu wakipata madaraka wanaona ndio maisha yao yatakua hivyo mpaka mauti kwahiyo wanatesa watu tu. hawajui kama kuna siku na wao watateswa
Hakika ndivyo ilivyo hata hapa kwetu kwa sasa. Mtu mwenye familia yake anapotezwa mazima na serikali (viongozi) hawajali bali wanakebehi as if hiyo familia yake inakuwa kama imepoteza paka wao.
Mchana peupe kiongozi mahiri anapigwa risasi ambazo hata jambazi hapigwi na serikali (viongozi) wanaona sawa na hawajishughulishi kuchunguza zaidi ya wao kuzuia malipo ya matibabu yasifanywe ili afa kwa kukosa huduma. Kama sio wananchi kuchangia hakika matibabu yangeshindikana na Lissu angekufa. Jee siku viongozi wa sasa yakiwatokea ya Doe wananchi watalia au kuchekelea? Wajifunze unyenyekevu na kutenda haki
 
Back
Top Bottom