Usijivune: Kassim Majaliwa, Prof Mark Mwandosya na marehemu Prof Idris Mtulia, Wakiwa ndani ya Mtumbwi


Ujumbe kuntu kwa mazombie ya Lumumba
 
Unaposema MUNGU lazima utufafanulie ni yupi unayemsema wewe.
 
hawakupanda huo mtumbwi kwa kupenda, hiyo ilikuwa kick au inaitwa nitoke vipi
 
Kuna mazingatio mengi sana. Hii naijibubili iwe kama rejea. Ni bandiko lenye kufikirisha sana.
 
Kuna mbunge mmoja wa mkoa wa Dsm alikuwa house girl kipindi cha nyuma na mama mwny nyumba alimtendea ukatili had leo yule mama choka mbaya afu dada ndo mbunge, sidhani km anaweza kugongea msaada kwa aliyomtendea in the past.
 
Viongozi wetu wawe wanapitia historia kama hizi, naamini zitawafanya wawe wanatafakari sana kabla ya kuongea na kuamua, huwa naangalia video za viongozi ambao huyu jamaa (Doe) aliagiza wafungwe kwenye nguzo halafu wapigwe risasi mbele ya kadmnasi nikawa najiuliza hivi alidhani yeye hapa duniani ndio amehamia jumla!
 
Jiwe ndio anaona Ulimwengu wote ni wake na wala hakumbuki alikotoka.
 
Mnyenyekevu hapo ni Mwandosya! Kwa sababu kwa cheo chake angekataa kupanda hauko ka-dau, na hao wengine wote wasingepanda.
 
You will lose nothing if God is not there and you beleive in Him.

"You will lose Nothing"???

Really?

All effects ya matendo yenu encompassing "belief" hayana shida?

How do we account for that?
 
Big up
 
Mwandosya pamoja na Uwaziri wake alipanda mtumbwi huo?
 
Picha hii ilipigwa mwaka 2009. Wa kwanza kulia (waliokaa) ni Prof.Idris Mtulia, aliyekua Mbunge wa Rufiji. Anayefuatia ni Prof.Mark Mwandosya wakati huo akiwa Waziri wa maji na umwagiliaji. Anayefuatia ni aliyekua mkuu wa wilaya hiyo Bw.Kassim Majaliwa.

Prof.Mwandosya akiwa Waziri alitembelea Rufiji katika ziara ya kikazi. Majaliwa akiwa mkuu wa wilaya akampokea, na Prof.Mtulia kama Mbunge mwenyeji akashiriki ziara hiyo. Hapa wanavuka kwa Mtumbwi mto Rufiji eneo la Mtanza.

Mwaka 2010 Majaliwa aligombea Ubunge Ruangwa baada ya kifo cha aliyekua Mbunge wa jimbo hilo Sigifrid Ng'itu. Alishinda na kuteuliwa Naibu Waziri TAMISEMI (Elimu). Miaka mitano baadae akawa Waziri Mkuu.

FUNZO:
Hakuna ajuaye hatma ya maisha yetu ila Mungu pekee. Ukiwa na cheo au madaraka makubwa leo usiwadharau walio chini yako, huenda kesho wakawa maboss zako.

Potifa alikua mkuu wa gereza kule Misri, akamuona Yusufu kama kijakazi aliyejaribu kumbaka mke wake, akamtupa gerezani. Lakini baadae Yusufu akawa Waziri Mkuu na Potifa akawa anatii na kutekeleza maagizo ya Yusufu.

Wakati Majaliwa akiwa DC Rufiji, alikua anaripoti kwa RC Pwani Bi.Amina Mrisho Said na Waziri wa TAMISEMI Stephen Wassira. Leo wote wawili hawapo tena serikalini.

Majaliwa alipoteuliwa Naibu Waziri TAMISEMI alikua anaripoti kwa Kepteni George Mkuchika. Leo mzee Mkuchika ndiye anayeripoti kwa Majaliwa.

Maisha ni mzunguko. Ukifanikiwa usijae kiburi ukadhani ndio mwisho wa safari. Al-Bashir alikua na madaraka makubwa na pesa nyingi. Lakini leo ni mfungwa. Anakula, kulala na kuamka kwa amri. Hana tena hiyari ya maisha yake.

Na pia ukikosa leo usikate tamaa ukadhani Mungu amekuacha. Bado lipo tumaini. Anayekudharau kwa sababu ni 'Housegirl' kesho unaweza kuolewa na Rais ukawa First Lady na akakuheshimu.

Wana wa Israel walipowekwa mateka kule Babeli, Esta na mjomba wake Mordekai walikua watumwa. Esta akachukuliwa na Hegai kuwa kijakazi kwenye nyumba ya Mfalme.

Hegai alikua kama 'Afisa Utumishi' kwenye kasri la mfalme Ahasuero. Vijakazi wote wa mfalme waliripoti kwake akiwemo Esta. Lakini baadae Esta akawa Malkia, na Hegai akawa anaripoti kwa Esta. Life is circle.

Hakuna aliyejua kiongozi mwenye ulinzi mkubwa na fedha nyingi kama Gadafi siku moja angeweza kujificha kwenye mtaro wa maji taka kama mwizi wa kuku.

Usijivune kwa kufanikiwa leo, na usivunjike moyo kwa kufeli leo. Winston Churchill aliwahi kusema "Success is not final, and failure is not fatal. It is the courage to continue that counts"

Mungu atujalie hatma njema.
 
Nzuri hiyo malipo ni hapa hapa duniani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…