Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Zama za mfumo wa chama kimoja nchini Malawi chini ya chama cha Malawi Congress Party (MCP) kilichokuwa kinaongozwa na Hastings Kamuzu Banda, siasa za nchi hiyo zilikuwa za kuogofya sana na zilijaa kila aina ya ukatili na uovu.
Katikati ya vurumai hiyo, kulikuwa na jumuiya ya vijana ya chama tawala iliyokuwa inaitwa Malawi Young Pioneers (MYP).
Jumuiya hiyo ambayo kwenye miaka ya tisini ilikuwa inaongozwa na watu kama John Tembo, Gerisham Jere na Zimani Banda, ilikuwa inaogopwa na kila mmalawi kuliko ilivyokuwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo
Vijana wa MYP walikuwa wanamiliki mashamba, majumba ,ofisi na silaha wakati mwingine bora zaidi kuliko za vyombo vya ulinzi na usalama.
Kiufupi MYP ilikuwa kama ndiyo jeshi binafsi la Kamuzu Banda na lilikuwa halihojiki Wala kuingiliwa na chombo chochote kile nchini Malawi. MYP walitesa, waliteka, walipora,waliua watu na hakuna aliyeweza kuwahoji.
Kutokana na kudekezwa na Kamuzu Banda, MYP walifikia mahali kujigamba kuwa Iko siku wao ndiyo watakuwa jeshi la Malawi. Na wakazua tabia nyingine ya kuwapiga wanajeshi wa nchi hiyo hasa wakiwakuta Bar.
Miaka ya tisini hasa mwaka 1993 wakati huo Kamuzu Banda akiwa na miaka zaidi ya 95, jeshi la Malawi likafikia ukomo wa kuvumilia manyanyaso toka Kwa MYP.
Siku moja bila ya kujua kuwa vitendo vyao vimeshachokwa na jeshi, vijana wa MYP waliwapiga wanajeshi jijini Lilongwe na kwenye mji wa Zomba. Na baadae kibabe wakawapeleka wanajeshi hao Hospitalini baada ya kuwapiga.
Wakati hayo yakitokea Mkuu wa majeshi wa wakati huo alikuwa ni Jenerali Isaac Yohane, mtu mtiifu kwa Kamuzu Banda na mfumo wa chama kimoja chini ya Malawi Congress Party.
Wanajeshi wa chini yake wakaanzisha Operesheni iliyokuja kujulikana kwa jina la "Bwezani" ikimaanisha "Rudisha ulichoiba"
Siku ya Disemba 9 mwaka 1993, jeshi chini ya Jenerali Manken Chigawa, likavamia Makao Makuu ya MYP, wakaenda kwenye Kambi ya Mpyupyu iliyokuwa kwenye mji wa Zomba, wakafika Mvera karibu na Salima, Kasungu na Kaskazini mwa mji wa Mzuzu.
Kufika Asubuhi ya tarehe 10 Disemba, Jenerali Chigawa akaenda kwenye redio ya Taifa bila ya ruhusa ya Banda na kutangaza kuwa MYP imesambaratishwa na kuvunjiliwa mbali.
Kwenye Operesheni Bwezani, silaha kadhaa kama makombora, bunduki Machine Gun zikiwemo, risasi lukuki pamoja na magari ya MYP vilikamatwa.
Ndani ya masaa 12 jeshi la Malawi lilifanikiwa kukisambaraitsha kikundi cha kihuni cha chama tawala wakati huo kilichokuwa kinaogopeka na kilichokuwa kinajiona chenyewe Kiko juu ya kila mtu ndani ya Malawi isipokuwa kwa Kamuzu Banda na watu wanaomtii yeye.
Kwenye Operesheni hiyo ambapo vijana wa MYP zaidi ya 5,000 walikamatwa au kujisalimisha na wengine kukimbilia msumbiji, Mkuu wa majeshi wa wakati huo, Jenerali Isaac Yohane alikuwa yupo kizuizini nyumbani kwake.