Usiku ambao malkia wa Cocaine alitaka kumuua Rais wa Colombia

Usiku ambao malkia wa Cocaine alitaka kumuua Rais wa Colombia

Miaka ya 1980 na 1990 iligubikwa na vita vya umwagaji damu kati ya serikali na makundi makubwa ya kihalifu. Wote tunaijua hadithi ya Pablo Escobar, lakini kulikuwa na mwanamke mmoja katili zaidi aliyetawala jiji la Miami na Colombia kwa mkono wa chuma:aliitwa Griselda Blanco, aliyefahamika pia kama "La Madrina" au "Malkia wa Cocaine".

Hii ni simulizi ya kweli ya usiku mmoja wa hatari sana, mwaka 1989 mjini Medellín, ambapo mkondo wa kundi lake la kihalifu ulipishana kwa sekunde chache na maisha ya Rais wa nchi hiyo, Virgilio Barco Vargas, kwenye mtego wa siri uliopangwa kufanywa juu kwenye ghorofa ya kifahari… ipo hivi

Ili kuelewa uzito wa usiku huu, ni lazima uwajue wahusika wakuu watatu waliokuwa kwenye ramani moja ya kifo:

• Rais Virgilio Barco: Kiongozi hatari wa Colombia ambaye mwaka 1989 alitangaza vita vya wazi dhidi ya makundi ya madawa ya kulevya (cartels), akiruhusu mkataba wa kuwapeleka wafungwa wa madawa nchini Marekani (extradition). Hii ilimfanya awe adui namba moja wa wahalifu wote.
View attachment 3633540
• Griselda Blanco: Malkia wa Cocaine ambaye alitoroka Marekani na kurudi Colombia kuendesha genge lake kwa siri. Alijulikana kwa mtindo wa kutumia wauaji wa pikipiki (motocicarios) na hakuwa na hofu ya kuua maafisa wa serikali.View attachment 3633541
View attachment 3633539
• Jorge "Rivi" Ayala: Muuaji mkuu wa kukodiwa na mtiifu kwa Griselda Blanco. Rivi alikuwa mtaalamu wa kutega mabomu na kuvamia majengo bila kuacha alama.

Sasa basi Novemba 1989, Rais Virgilio Barco alikuwa asafiri kwa siri kubwa kwenda mji wa Medellín kukutana na wamiliki wa viwanda ili kujadili usalama wa mji huo uliokuwa unateketea kwa mabomu. Kwa sababu za kiusalama, ikulu haikutangaza hoteli ambayo Rais angefikia wala muda wa msafara wake.

Hata hivyo, kundi la siri la Griselda Blanco lilikuwa limesha wahonga maafisa wa ngazi ya juu wa polisi wa jiji hilo. Masaa machache kabla ya Rais kutua, Griselda alipokea ujumbe mfupi: "Ndege ya Rais inatua saa nne usiku. Atakaa kwenye ghorofa ya 22 (Presidential Suite) ya Hoteli ya InterContinental."

Griselda alimuita Rivi Ayala na kumpa amri fupi: "Hii ndio nafasi yetu ya kuonyesha nani anamiliki nchi hii. Sitaki Rais huyo aone jua la kesho asubuhi."

Rivi Ayala alikusanya kikosi cha makomando wa kihalifu 12. Walivaa suti nyeusi zinazofanana na zile za walinzi binafsi wa Rais (Secret Service) na kubeba bunduki za kisasa za kijeshi zilizofichwa kwenye mabegi ya gofu.

Majira ya saa tano usiku, kikosi hicho kiliingia hotelini hapo kupitia mlango wa nyuma wa jikoni baada ya kumfunga kamba na kumziba mdomo meneja wa zamu. Walitumia lifti ya mizigo kupanda hadi ghorofa ya 21, walipanga kupanda ngazi za dharura hadi ghorofa ya 22 ambapo Rais alikuwa amepumzika baada ya safari.

Wakiwa kwenye ngazi hizo, Rivi alitoa bastola yake yenye kizuia sauti (silencer), tayari kuwazima walinzi wawili waliokuwa wamesimama nje ya mlango wa Rais. Kwenye zile sekunde za taharuki, ambapo mkono wa muuaji ulikuwa mita chache tu kutoka kwenye chumba cha Rais wa nchi, kitu kimoja kidogo kilibadili historia yote.. ni nini hicho?

Mkuu wa walinzi wa Rais, Kanali Martínez, alikuwa na tabia ya wasiwasi uliopitiliza (paranoia). Dakika 15 kabla ya wauaji hawajafika, alimshauri Rais Barco kuwa hoteli hiyo ilikuwa na madirisha mengi makubwa yanayoweza kuruhusu wadunguzi (snipers) kumpiga kutoka maghorofa ya jirani. Bila kumwambia mtu yeyote hoteli humo, alimhamisha Rais usiku huo huo kwa siri kupitia lifti ya dharura kwenda kwenye ngome ya kijeshi iliyoko karibu ya Batallón Bomboná.

Wakati Rivi na watu wake walipovunja mlango wa chumba cha ghorofa ya 22, walikuta chumba kiko tupu kabisa, huku kikombe cha kahawa cha Rais kikiwa bado cha moto juu ya meza. Wakajua kuwa wameshagundulika, wauaji hao walitoroka haraka kabla jeshi halijazingira hoteli hiyo.

Huu ukawa mwanzo wa mwisho wa kundi la Griselda Blanco nchini Colombia. Rais Barco, akiwa amekasirishwa na dharau ya kundi hilo kutaka kumuua ndani ya chumba chake, aliamuru operesheni kubwa ya kijeshi iliyopewa jina la Search Bloc. Ndani ya miezi michache, washirika wengi wa Griselda walikamatwa, Rivi Ayala alikamatwa nchini Marekani na kufungwa jela maisha, na Griselda Blanco mwenyewe alikuja kuuawa miaka mingi baadae (2012) mjini Medellín kwa kupigwa risasi mbili za kichwa akiwa anatoka sokoni kununua nyama. Ikawa the end of Godmother...
Anyway lakini kama umebahatika kusoma riwaya ya The godfather ya Mario puzzo , kabla ya kuanza kusoma chapter one ,utakutana na nukuu moja ya kibabe sana inasema unasema in every great fortune, there is crime @Balzac🫵🫵😎
Cc.connecttz
In every Great fortune there is crime
 
Back
Top Bottom