AHADI ISIYOTEKELEZWA,NI MZIGO WA LAWAMA
1.Tuliambiwa,tatizo la umeme ni upungufu wa maji kwenye mabwawa,Mungu akaleta mvua ya kutosha,bado ikatafutwa sababu nyingine.
2.Tuliambiwa,tatizo litaisha tukiwasha mtambo katika mradi mpya wa bwawa la Nyerere,siku zikifika,wanasogeza tarehe mbele,utasikia sababu zingine,Mwezi Machi ndio shida itaisha kabisa..
Katika aibu,Serikali ione aibu ya kushindwa kujisimamia kwa kukosekana kwa umeme wa uhakika,huku Viongozi wakijitoa ufahamu kama vile ni suala dogo tu.,huku wakujua ukuaji wa uchumi unategemea umeme.
Wanànchi wanawangalia tu,mnatoa sababu zinazobadilika badilika kila siku bila hata aibu.
Mbona kama mnashindwa kudhibiti mambo yanayowaumiza wananchi;mnaacha bei zinapanda kiholela,hata hatua za udhibiti wa bei za bidhaa.
Hili la upungufu wa umeme tunawasubiri.