Usikubali heshima kubwa kanisani mtizame Mungu, isipokuwa tu kama unaheshimika na huna Fedha wala madaraka

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Kesho ni siku ya kuabudu na kumtukuza Mungu. Simaanishi kwamba siku nyingine sifanyi hivyo Ila ninaposali Mimi jumapili ni siku maalumu ya ibada.

Nimewiwa kuwaomba wanaoingia kanisani kuanzia kesho wajitafakari kuhusu heshima wanayopewa, je heshima inatokana na wao wanavyomytumikia Mungu au heshima inatokana na pesa na Mali walizonazo? Je, heshima haitokana na nyadhifa zao?

Ukibaini unapewa heshima na viongozi wa Dini na unaamini heshima hiyo inatokana na Mali au wadhifa wako pls Mwombe Mungu akusaidie upate ujasiri wakumwambia huyo kiongozi wa Dini asikuabudu wewe na Mali zako amwabudu Mungu. Mwombee kiongozi wako wa Dini asikufanye wewe ukajiona ni Bora KULIKO wengine kwa sababu utaendelea kwenda kanisani kupokea sifa za wanadamu huku ukijikusanyia Kuni za kuzimu.

Naamini viongozi wengi wa Dini wamewafanya watu wasio na uwezo kiuchumi wasipewe Nafasi kanisani hata kama Wana upeo mkubwa kiasi gani. Tuliojaaliwa uwezo na nyadhifa tunalojukumu la kuzosaidia nyoyo za viongozi wa Dini zisituabudu Sisi Bali zimwabudu Mungu.

Huu ni wito wangu kwenu wanadamu, nimezungumzia Kanisa Kwa sababu naabudu huko. Endapo ujumbe huu utamfaa asiyeabudu kanisani inshaalah ila mwisho wa siku lazima tukubali kwamba viongozi wa Dini wameacha kutumia dini kumwabidu Mungu Bali wanatumia dini kama ajira na njia yakuwakuza wenye Fedha huku wakibagua wasio na Fedha.
 
Lengo lako la kwenda Kanisani ni nini hasa? Ukilatambua Hilo basi mengine ni ya ziada .
 
Kusema ukweli umenena VEMA hivyo ndivyo hali ilivyo kwa sasa katika makanisa karibia yote
 
Back
Top Bottom