Kila mtu anasema tujiajiri, hakuna anaefundisha namna ya kujiajiri
Kwakweli siwapendi nyie motivation speakers
Hakuna model ya uchumi wa kileo inayoruhusu kila mtu kujiajiri. Au hata majority ya watu kuwa wamejiajiri.
Watu wanachukulia mambo simple.
Ukweli ndio huo.
Wote tukijiajiri mahakama zitaendeshwa na nani? Ofisi za Polisi zitaendeshwa na nani? Hospitali za umma zitaendeshwa na nani? Shule za serikali zitaendeshwa na nani? Kazi za bandari zitaendeshwa na nani? Ofisi zote za serikali zitaendeshwa na nani?
Haya, tuseme watu wanaofanya kazi ofisi ya serikali ya kutoa vibali vya kuanzisha biashara wote wasikilize ushauri huu, waache kazi na kuanzisha biashara zao, na watu wengine wasi apply kazi hizo za serikali, kwa sababu wamesikia ushauri huu na wao wanataka kuanzisha biashara zao.
Nani atatoa vibali vya serikali vya kuanzisha biashara mpya ikiwa hao wafanyakazi wa serikali wa kutoa vibali vya kuanzisha biashara wote wameacha kazi na kwenda kuanzisha biashara zao?
Ushauri huu ukifuatwa na watu wengi utaangusha uchumi.
Hii model basically ina abolish government and all government services. How do you run a modern country without a government?
That will give us absolute chaos.
Maisha si mshahara au mafanikio ya pesa tu, kuna walimu wanapata satisfaction kubwa sana kwa kujua kwamba wanafundisha kizazi kijacho, wanaheshimiwa na jamii, at least wanatakiwa kuheshimiwa na jamii, hata kama mshahara wao si mkubwa sana.
Kuna madaktari wanafanya kazi serikali ya Tanzania kwenye mshahara mdogo licha ya kuweza kwenda nchi nyingine kwenye mshahara mkubwa, au kuweza kuanzisha practices zao, kwa sababu wanaona ratio ya madaktari kwa population nyumbani kwao Tanzania ni ndogo sana. Na wengine wanaamua kutokuanzisha oractices zao na kwenda vijijini huko ambako hakuna privilege wala services nzuri, ili waweze kuhudumia watu wa vijijini zaidi.
Hiyo model mnayohubiri ya majority self employed population inaonesha hata nyie wenyewe hamna akili ya kuelewa uchumi huo hautakuwa sustainable.
Hakuna nchi yoyote duniani iliyoweza kufanya mfumo huo.
Yani mnahubiri kitu ambacho kitaiumiza jamii nzima na kuwaumiza hata nyie wenyewe.
Inaonekana mnahubiri vitu ambavyo hamjavifikiria kwa kina.