Usikubali kusaini nyaraka hii unapopekuliwa na Polisi

Wakili MSOMI,nashukuru kwa ufafanuzi wako hapo hiyo form unaletewa katika mazingira gani?Hati uwe na uwezo wa kutosaini!?
 
Wewe wakili kichwa cha habari UMEANDIKA CHA HOVYO na nina doubt kubwa kama wewe unaweza kuendilea na sifa ya kuwa afisa wa mahakama pamoja na msimamizi wa viapo

Kwenye statutory interpretation heding ni muhimu kabisa katika kubeba maana y document na mtu anayefanya tafsiri ya andiko fulani ili kujua muandishi alimaanisha nini anaweza kutumia kichwa cha habari kama nyenzo muhimu ya kujua lengo la maandishi yale

Mtu akisoma kichwa cha habari atajua kuwa Wakili uneharamisha CERTIFICATE OF SEIZURE kwamba haipo kiusheria na watu hata wanapopekuliwa kwa kufuata tatatibu zote za sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai pamoja na sheria y ushhidi na sheria nyinginezo basi wasikubali kusaini

Hiii ni hatari kubwa kwa wanasheria mnapotoa elimu ya sheria kwa njia ya KIUANAHARAKATI halafu taaluma mnaweka pembeni hapa mnatengeneza taifa la ma RADICAL S na italeta mgongano mkubwa kati y wananchi wanapokutana na wasimamizi.wa sheria.

Content ni nzuri.sana lakini heading ni Mbovu kabisa kuandikwa.na mwanasheria heading ingereflect illegal search na sio search zote.
 
kumbe Ni inawezekana mkuu!
Na vipi kuhusu ile sign ya kuweka na dolegumba ambalo limechovywa kwenye wino!
 
Ingekua ni ukikataa tu kusaini ushahidi unaharibika Basi waliokutwa na madawa ya kulevya majumbani kwao wangekua wanakataa na sahiv wasingekua jela.

Wakija kukipekua wanakuja na kiongoz wako wa mtaa hata ukikataa kusaini ila kama umekutwa nacho bado mziki ni mzito tu
 
Kwenye iyo fomu si pia vinaorodheshwa na vitu ambavyo vimekutwa kwenye iyo office au nyumba, na pia kunakuwa na sehemu ya kusaini mjumbe au balozi,,, au iyo ni tofauti na search warrant!?
 
Huyu ni Wakili kweli?? na mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini..
Huyu ni Wakili kweli?? na mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini..
Amesema unakataa kusaini kama kunakitu unaona hakipo sawa. Ametoa mfano hata kama nikitu kidogo kama sindano wakijaza fomu kwamba wameondoka nacho wakati wewe kwako hakikuepo,usisaini fomu hiyo. Bilashaka wakili yupo sahihi
 
Bahati mbaya hao jamaa kuna wakati mwingine hutumia nguvu badala ya ustaarabu kukusainisha! Virungu nje nje!! Biti kali!! nk.

Sasa kama hujafikia viwango vya ununda, itakulazimu tu kusaini.
Bora nguvu itumike kuliko kusaini kitu nisichokubaliana nacho. After all, kwanini kuweka mazingira ya kumfunga mtu kwa kutumia uongo?
 
Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.

Hicho kinachoitwa utaratibu wa kisheria, ndicho wakati mwingine kinatumika vibaya kwa kubambikia watu vifurushi!
 
wewe ni mwanasheria mchanga, bado una safari ndefu. kwa taarifa yako, hata usiposaini, lakini wamesaini independent witnesses, haimaanishi certificate of seizure haitapokelewa mahakamani, na haimaanishi haitakuwa na mashiko. usipoteze wenzako maboya. halafu, hivi kwa akili yako huwa kuna mtu anayesaini kwa kupenda au ameshavurugwa kwa kichapo na vitisho? ati usikubali,wanasheria huwa mnapotosha sana watu kwa vitu vya wazi. chukulia mfano hao kina song lei, wanakutwa na pembe za ndovu sijui faru live kwenye gari yao au kwenye begi, au mtu anakutwa na kichwa cha mtu kwenye mfuko, auu mtu anakutwa na unga tumboni au kwenye begi, unaanzaje kukataa kwa mfano, hata wakikuzaba kibao watakuwa wamekuonea kweli? na hakuna ushahidi kama ulichapwa wala nini....hujawahi kamatwa ndio maana unaongea hivyo, ukija kufanya kosa la maana ukakamatwa ukawa peke yako chumbani kule polisi utajua kama mtu anaweza kusaini au akawa na uhuru kukataa. unaweza kukataa kama wanakubambika, n a wao ni binadamu wanaweza kukuacha wasikuchape, ila umekutwa navyo na unakataa utajikuta wewe mwenyewe unaomba peni usaini. pia, uwepo wa independent witnesses huwa una cure hiyo hoja yako and still certificate of seizure can be admissible in court without the signature of the accused on it.
 
Wakili msomi naomba tafsiri ya hichi kipande .[emoji116]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…