Usikubali kusaini nyaraka hii unapopekuliwa na Polisi

Usikubali kusaini nyaraka hii unapopekuliwa na Polisi

USIKUBALI KUSAINI NYARAKA HII UNAPOPEKULIWA NA POLISI

Na Bashir Yakub. WAKILI
+255 714 047 241

Polisi wanapokufanyia upekuzi, iwe wewe mwenyewe binafsi, nyumbani kwako, kazini kwako, gari lako au penginepo ipo fomu maalum ambayo wao wenyewe huijaza na kumtaka mtu aliyefanyiwa upekuzi naye kuijaza.

Fomu hii huitwa Certificate of Seizure. Fomu hii hujazwa hasa pale ambapo katika upekuzi kuna chochote kinatakiwa kuchukuliwa kama ushahidi(exhibit).

Ni fomu ambayo huoredhesha mali ama vitu ambavyo umekutwa navyo. Chochote ambacho umekutwa nacho ambacho wao wanatakiwa kukichukua/kuondoka nacho kama ushahidi basi huorodheshwa.

Hata kama kidogo kama pipi ama sindano madhali wanatakiwa kukichukua kwa ajili ya upelelezi basi hutakiwa kuorodheshwa kwenye hiyo fomu/hati.

Aidha, ni muhimu kujua kuwa ikiwa unapinga kuhusu kile kinachochukuliwa kuwa hukukutwa nacho ama hakikukutwa kwako basi usikubali kusaini fomu hiyo.

Hii ni kwasababu kukubali kwako kusaini fomu hiyo tafsiri yake kisherria ni kuwa umekubali kuwa umekutwa na hicho kitu.

Na endapo utafikishwa mahakamani basi fomu hiyo itawasilishwa kama ushahidi na kwasababu ulisaini basi ulikubali kuwa ulikutwa na kitu hicho.

Vinginevyo uwe unakubali kuwa ni kweli hicho kitu umekutwa nacho, basi hapo waweza kusaini. Lakini kama hukubali basi usisaini.

Msimamo huu ni wa Mahakama ya rufaa kupitia kesi ya SONG LEI VS THE DPP, AND THE DPP VS XIAO SHAODAN and Two Others, Consolidated Criminal Appeal Nos. I6'A' of 2016 & 16 of 2017, ambapo mahakama ilisema kuwa kusaini hati/fomu ya upekuzi ya mali zilizochukuliwa ni kukubali kuwa umekutwa na huo ushahidi.

Katika hii kesi raia wa China walisaini Pembe za Wanyama kukutwa ndani ya gari lao na ndo ukawa ushahidi dhidi yao.

Maamuzi mengine mengi yameeleza msimamo huu kuwa ukikubali kusaini umekubali kukutwa na huo ushahidi.

Ni muhimu sana kulijua eneo hili la mtego ambalo linaweza likakupeleka jela na yafaa basi kuwa makini katika mazingira hayo.
Kama kweli huyu ni wakili basi ni bogas kabisa.. Upekuzi wowote unafanyika kwa kufuata utaratibu, utàratibu huo ni kuwa upekuzi lazma ufanyike mbele kiongozi Wa serikali ya mtaa, au hata mbele ya wakili wako au mashahidi wengne kama ndugu zako.

Pia anayepekuliwa lazma aelezwe kwamba ni kitu gani kinatakiwa katka upekuzi huo.. Sasa huyu kanjanja sijui anaongea nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naona ameelezea vizuri. Kuna upekuzi mwingine unafanyika ili kupandikiza ushahidi wa uongo. Fikiria askari ana kusearch na katika kufanya hivyo anaonesha ulikuwa na bangi ilhali sio kweli! Utakubali kusign?
Usisign upigwe virungu ufe uache familia
 
Kazi ya wakili ni kukataa kosa hata kama umetenda kweli
Kazi ya Wakili siyo kukataa kosa bali ni kumtetea mtuhumiwa au mteja wake mkuu. Kama una wakili wa hivyo basi hakufai kabisa.

Mfano kesi ya kuua mtu ambaye umemfumania mtu anafanya mapenzi na mke wako. Huwezi ukasema sikuua. Bali lazima Wakili akuongoze vyema ili uileze mahakama ni kwa namna gani au mazingira gani hicho kifo kilitokea.

Mfano
Wakiki: Shahidi/mtuhumiwa ieleze mahakama ni nini kilitokea tarehe 5/6/2020.

Shahidi/mtuhumiwa: manamo tarehe hiyo nilitoka kazini mida ya saa mbili usiku. Nilipofika nyumbani chumbani nilimkuta marehemu anafanya mapenzi na mke wangu.

Mfano mwingine ni kifo kilichotokea wakati wa kujitetea( self defense). Hapa Wakili inabidi wakati wa utetezi akuongoze wewe uoneshe mazingira ambayo hicho kifo kilitokea.
 
hapa kuna vitu viwili, iwe ni risiti au certificate of seizure,kama kuna ushahidi kwamba ulitakiwa kusaini ukagoma, na wapo mashahidi waliosaini kwenye certificate na wakaongea hivyo mahakamani, hiyo risiti itakubana tu hata ufanyeje. labda PP awe boya.

kama
Unaweza ukasaini au kutosaini na bado certificate of seizure ikawa haina maana so inategemea aina ya kesi ya jinai mfano unakutwa na mali zinatiliwa shaka kwamba ni za wizi. Polisi akasaini na wewe ukasaini pamoja na shahidi huru. Lakini kule mahakamani yule Shahidi(mtu aliyelalamika kuibiwa) akashindwa kufanya utambuzi/ kutambua hizo mali anazosema zimeibiwa pale mahakamani. Do you think mpaka hapo certificate of seizure itasaidia?
 
Search warrant= hati ya kufanya upekuzi. Hiki ndicho kibali kinachowapa nguvu ya kufanya upekuzi. Ingawa askari anaweza fanya upekuzi bila hata ya kuwa na hati ya upekuzi akihisi kwenye gari yako kuna madawa ya kulevya etc ila ni lazima shahidi huru awepo.

Certificate of seizure na search warrant ni nyaraka mbili tofauti ila hutumika katika tukio moja la upekuzi.

Certificate of seizure hutolewa baada ya kufanya upekuzi ndani ya nyumba na ofisi. Upekuzi unapofanyika lazima awepo shahidi huru(independent witnes) mara nyingi ni wajumbe wa mtaa au mtaa chairman.

Certificate of seizure huorodhesha mali zote ambazo zimekutwa katika ofisi yako au kwenye gari.

Certificate of seizure lazima isainiwe na mwenye ofisi, gari, au mtu yeyote ambaye amefanyiwa upekuzi, askari polisi na shahidi huru. Baada ya hapo polisi lazima akupe risiti ya upekuzi kwa mujibu wa sheria. Lengo la kusaini ni kwamba unakubali kwamba umefanyiwa upekuzi kwa mujibu wa sheria na umekutwa na hizo mali au nyaraka.

Ukiona upekuzi unafanyika bila shahidi huru ujue huo ni illegal search.
asante
 
Kuna mashahidi kadhaa wanakuwepo wanaotakiwa kujiridhisha kinachofanyika kina uhalali labda nao hao washawishiwe kukuruka
Unatakiwa kuwa makini sasa wewe mwenye nyumba na inashauriwa hata kuingia ndani utangulie wewe, hata chumbani tangulia wewe wengine wafuate hiyo bastola wataweka saa ngapi?

Polisi hawawezi kuhadaa ujumbe mzima wa watu zaidi ya watano wakugeuke utakuwa ulichokwa tu na mtaa wako
Suala la kupandikiza ushahidi unaliangalia kwa wepesi mno!!

Evidence Planting sio lazima ifanywe na polisi!! Nimeshakupa njia mbili za namna gani ushahidi unaweza kupandikizwa! Polisi wanaweza kupandikiza ushahidi au wakati mwingine watu wake wale wale unaowaamini wanaweza kununuliwa na kupandikiza ushahidi!

Wakati wewe unaamini nyumba ipo safe, kumbe watu wameshafanya yao, na baada ya hapo architect wa mchezo anaihalifu polisi kwamba, kwa mfano nyumba x wanajihusisha na mihadarati!
 
USIKUBALI KUSAINI NYARAKA HII UNAPOPEKULIWA NA POLISI

Na Bashir Yakub. WAKILI
+255 714 047 241

Polisi wanapokufanyia upekuzi, iwe wewe mwenyewe binafsi, nyumbani kwako, kazini kwako, gari lako au penginepo ipo fomu maalum ambayo wao wenyewe huijaza na kumtaka mtu aliyefanyiwa upekuzi naye kuijaza.

Fomu hii huitwa Certificate of Seizure. Fomu hii hujazwa hasa pale ambapo katika upekuzi kuna chochote kinatakiwa kuchukuliwa kama ushahidi(exhibit).

Ni fomu ambayo huoredhesha mali ama vitu ambavyo umekutwa navyo. Chochote ambacho umekutwa nacho ambacho wao wanatakiwa kukichukua/kuondoka nacho kama ushahidi basi huorodheshwa.

Hata kama kidogo kama pipi ama sindano madhali wanatakiwa kukichukua kwa ajili ya upelelezi basi hutakiwa kuorodheshwa kwenye hiyo fomu/hati.

Aidha, ni muhimu kujua kuwa ikiwa unapinga kuhusu kile kinachochukuliwa kuwa hukukutwa nacho ama hakikukutwa kwako basi usikubali kusaini fomu hiyo.

Hii ni kwasababu kukubali kwako kusaini fomu hiyo tafsiri yake kisherria ni kuwa umekubali kuwa umekutwa na hicho kitu.

Na endapo utafikishwa mahakamani basi fomu hiyo itawasilishwa kama ushahidi na kwasababu ulisaini basi ulikubali kuwa ulikutwa na kitu hicho.

Vinginevyo uwe unakubali kuwa ni kweli hicho kitu umekutwa nacho, basi hapo waweza kusaini. Lakini kama hukubali basi usisaini.

Msimamo huu ni wa Mahakama ya rufaa kupitia kesi ya SONG LEI VS THE DPP, AND THE DPP VS XIAO SHAODAN and Two Others, Consolidated Criminal Appeal Nos. I6'A' of 2016 & 16 of 2017, ambapo mahakama ilisema kuwa kusaini hati/fomu ya upekuzi ya mali zilizochukuliwa ni kukubali kuwa umekutwa na huo ushahidi.

Katika hii kesi raia wa China walisaini Pembe za Wanyama kukutwa ndani ya gari lao na ndo ukawa ushahidi dhidi yao.

Maamuzi mengine mengi yameeleza msimamo huu kuwa ukikubali kusaini umekubali kukutwa na huo ushahidi.

Ni muhimu sana kulijua eneo hili la mtego ambalo linaweza likakupeleka jela na yafaa basi kuwa makini katika mazingira hayo.
Wakili:

Ukikataa kusaini inakuwaje?

Ni poa tu? Kwa nini watu husaini na vitu hawañutwa navyo kama ni poa kukataa kusaini? Changamoto huwa ni nini?

Usiposaini na kuna baadhi ni kweli wamechukua unavipata pataje mwisho wa kesi kama ulikataa kusaini na hakuna rekodi ?

Hiyo kesi ya Mahakama Kuu what was the case or controversy before the court ? Wachina walisema tumesaini gizani au tuliwekewa pisto utosini au hatuelewi maandishi ya Kiswahili au saini sio zetu, zimeghushiwa???

Na mahakama ikasema screw you all China men, ukisaini umesaini ?????

Umesema na umerudia rudia kwamba hati hii hujazwa endapo kuna chochote kinachotakiwa kuchukuliwa. Kinachotakiwa na nani ? Unashutumiwa kutumia matusi na uchochezi kwenye mkutano wa hadhara, ushahidi video. Wanakunyang'anya simu. Hiyo simu inatakiwa kuchukuliwa, inatakiwa na nani ??? Sheria ipi ? Au utuambie ni kitu ambacho wao wanataka kukichukua?

Na unasema hati hii hujazwa hasa pale ambapo kuna chochote kinachotakiwa kuchukuliwa kama ushahidi. Ni mazingira gani mengine ambapo hakuna kinachochukuliwa lakini bado wanakutaka ujaze ? Kama hakuna, kwa nini umetumia maelezo ya "hasa pale ambapo" ? Uliteleza, au ???????
 
Unaweza ukasaini au kutosaini na bado certificate of seizure ikawa haina maana so inategemea aina ya kesi ya jinai mfano unakutwa na mali zinatiliwa shaka kwamba ni za wizi. Polisi akasaini na wewe ukasaini pamoja na shahidi huru. Lakini kule mahakamani yule Shahidi(mtu aliyelalamika kuibiwa) akashindwa kufanya utambuzi/ kutambua hizo mali anazosema zimeibiwa pale mahakamani. Do you think mpaka hapo certificate of seizure itasaidia?
hiyo sio rahisi kutokea labda kama shahidi ameamua kuturn hostile. kwa kawaida, kabla ya kuja mahakamani shahidi huwa anaandaliwa na prosecutor, anaonyeshwa hadi exhibits zote za mahakamani au kama zipo tayari kule anafafanuliwa zilivyo, kiufupi ni kwamba anafundishwa.period. sasa huko kufika mahakamani na kushindwa kutambua itaanzia wapi?
 
Alichosema wakili ni kuwa usisaini kama hukubali kukutwa na hivyo vitu au hukubali kuwa ni vyako. Wewe ulichojibu ni kuwa hata bila kusaini bado cheti kina maana, lakini wakati huohuo ukalazimisha mtu asaini kwa sababu hata asiposaini bado haitamsaidia.

Sasa kama hata asiposaini haimsaidii, kwa nini alazimishwe kusaini?? Sio kwamba saini yake itarahisisha kazi kwa upande wa huyo PP kuliko ambavyo asiposaini. Hakuna kinachodangwanywa hapa, kutosaini kunamsaidia mtuhumiwa kuliko ambavyo angesaini, ndicho anachosema wakili
kama unakubaliana na mimi kuwa hata asiposaini haitamsaidia sasa huyu mwanasheria ametoa ushauri kuwa wasisaini kwa faida gani sasa? kama umemwelewa yeye lengo lake kuleta hapa hiyo hoja alikuwa anaamini usiposaini hiyo certificate itakuwa worthless/valueless, na anaamini mshitakiwa anaweza kutokea hapo, kitu ambacho sio always! alijielekeza vibaya na kwa watu waelewa, hata yeye mwenyewe tu, ninaamini ameshatambua mapungufu yake na amekubaliana nayo tayari. ninyi tu wengine ndio mnahangaika ila mtu mwelewa anayeamini siku zote tunaishi kwa kujifunza na kukosolewa huwa anakubali kurekebishwa.
 
Unaweza kusaini ktk listi unayoiona.... Bila tatizo.... Alafu jamaa wakaongeza pembe ya ndovu katika listi wakati wewe haupo... Mchakato ukaanzia hapa....

Inatia shaka....
kwa taarifa yako, hizo risiti/certificate nyingi zinakuwa sio tu na saini ya kawaida, bali na dole gumba. sasa kama watafoji na dole gumba lako basi utakuwa uliweka dolegumba la aina nyingine unayoijua wewe. ukiona certificate hauiamini, unaweza kuibishia na kuomba ichunguzwe dole gumba kama saini unaona imefojiwa. kwa kawaida kabla haijatolewa mahakamani si lazima upewe uichunguze na useme cha kusema?
 
Mkuu, kama cheti hicho kinaweza kuwa admissible na kuwa na mashiko bila hata ya saini ya mtuhumiwa kuna umuhimu gani wa kumlazimisha asaini?? Maana unasema kabisa watu huwa hawasaini kwa kupenda bali kwa lazima.

Na unaona ni sawa kwa mtuhumiwa kuzabwa vibao sababu amekutwa redhanded ilhali yeye hakubali kuwa amekutwa redhanded? Unaona ni sawa kwa sababu tu hakutakuwa na ushahidi wa kuonesha kuwa alipigwa? Hao independent witness wanakuwa wapo kwa ajili ya kushuhudia kila kinachotokea au wapo kwa ajili ya kuhakikisha mtuhumiwa anasaini?

Sio vyema kabisa kufurahia matumizi ya nguvu kwenye upekuzi au ukamataji. Hapa bado tunahitaji sana maaskari wetu wapewe body cams ili kuepusha mambo kama haya. Kesi inajengwa kwa ushahidi imara na sio wa kulazimishana
the sameway unaposema sio sawa kumzaba mtu, na mimi ningesema sio sawa kutoa mitego kwa wahalifu ili wakwepe mkono wa sheria wakati wanakuwa wameleta madhara aidha kwa watu binafsi au kwa serikali. unajua kabisa kuwa mtu amekutwa navyo na yeye anajua, halafu anakataa kusaini, utamwachaje kumzaba kwa mfano? na ninawashaurini, ukikutwa na kitu usilete ubishi utakuja upigwe na fimbo isiyo ya kawaida na hutaamini macho yako kwa kitu kidogo tu. we saini mengine mtapambana mahakamani. kuna maeneo utapigwa kwa mfano kwenye tigo huko na hautajulikana kama ulipigwa. huyo mwanasheria anawapotosha mtajuta. akili za mbayuwayu changanya na za kwako. nimekuwa PP kwa miaka mingi sana najua ninachoongea.
 
Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.
umemuelewa lakini??? kweli umepekuliwa.....na wewe wajua huna bangi kwako ...wakakuchezea cheusi chekundu banga ikkawepo ghafla..lakini katika ile fomu BANGE imeorodheshwa....utasaini??
 
kwa taarifa yako, hizo risiti/certificate nyingi zinakuwa sio tu na saini ya kawaida, bali na dole gumba. sasa kama watafoji na dole gumba lako basi utakuwa uliweka dolegumba la aina nyingine unayoijua wewe. ukiona certificate hauiamini, unaweza kuibishia na kuomba ichunguzwe dole gumba kama saini unaona imefojiwa. kwa kawaida kabla haijatolewa mahakamani si lazima upewe uichunguze na useme cha kusema?
Namaanisha Hivi..... Unaweza kusaini ukatia na dole gumba.... Jamaa wakaenda kuongeza item kwenye list ile uliyosaini awali....
 
Sawa hebu tuletee tena kihusu huyu aliyepigwa na akalazimishwa kusaini mahakama inasemaje hapa
 
Kumbuka tu kuna muda watachukua mali yako halali kwa kuishuku tu sasa ukikataa kusaini maana yake hawakuchukua.Hivyo Mkumbushe mwananchi kuwa siyo kila kilichochukuliwa wakati wa upekuzi siyo cha kukataa kusaini maana kuna muda unaikana Mali yako halali maana upelelezi ukikamilika na ikabainika hiyo mali haihusiki utarudishiwa.
 
Namaanisha Hivi..... Unaweza kusaini ukatia na dole gumba.... Jamaa wakaenda kuongeza item kwenye list ile uliyosaini awali....
wakiongeza item, siku inapokuja kutolewa mahakamani wewe utajua waliongeza item na itakuwa mojawapo ya sababu ya objection, pia kutakuwa na independent witness ambaye atakusapoti kwa hilo. cha msingi ni kwamba, hata ukigoma kusain iwe kwa dole gumba au pen inaweza kupokelewa tu, though kila kesi huamuliwa kulingana na mazingira yake.
 
Mkuu inawezekana hukumuelewa vizuri wakili. Hakumaanisha kuwa nyaraka haitapokelewa, alichomaanisha ni uzito wa hiyo nyaraka katika kesi, itakuwa imepokelewa lakini bila kuwa na uzito wa kumuweka hatiani mtuhumiwa tofauti na ingekuwa na saini yake. Hicho ndio msingi wa uzi. Msisitizo, amesema ikiwa unaona umebambikiwa vitu halisia au karatasi limeandikwa vitu visivyopo kihalisia
 
Back
Top Bottom