sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Mkuu, kama cheti hicho kinaweza kuwa admissible na kuwa na mashiko bila hata ya saini ya mtuhumiwa kuna umuhimu gani wa kumlazimisha asaini?? Maana unasema kabisa watu huwa hawasaini kwa kupenda bali kwa lazima.wewe ni mwanasheria mchanga, bado una safari ndefu. kwa taarifa yako, hata usiposaini, lakini wamesaini independent witnesses, haimaanishi certificate of seizure haitapokelewa mahakamani, na haimaanishi haitakuwa na mashiko. usipoteze wenzako maboya. halafu, hivi kwa akili yako huwa kuna mtu anayesaini kwa kupenda au ameshavurugwa kwa kichapo na vitisho? ati usikubali,wanasheria huwa mnapotosha sana watu kwa vitu vya wazi. chukulia mfano hao kina song lei, wanakutwa na pembe za ndovu sijui faru live kwenye gari yao au kwenye begi, au mtu anakutwa na kichwa cha mtu kwenye mfuko, auu mtu anakutwa na unga tumboni au kwenye begi, unaanzaje kukataa kwa mfano, hata wakikuzaba kibao watakuwa wamekuonea kweli? na hakuna ushahidi kama ulichapwa wala nini....hujawahi kamatwa ndio maana unaongea hivyo, ukija kufanya kosa la maana ukakamatwa ukawa peke yako chumbani kule polisi utajua kama mtu anaweza kusaini au akawa na uhuru kukataa. unaweza kukataa kama wanakubambika, n a wao ni binadamu wanaweza kukuacha wasikuchape, ila umekutwa navyo na unakataa utajikuta wewe mwenyewe unaomba peni usaini. pia, uwepo wa independent witnesses huwa una cure hiyo hoja yako and still certificate of seizure can be admissible in court without the signature of the accused on it.
Na unaona ni sawa kwa mtuhumiwa kuzabwa vibao sababu amekutwa redhanded ilhali yeye hakubali kuwa amekutwa redhanded? Unaona ni sawa kwa sababu tu hakutakuwa na ushahidi wa kuonesha kuwa alipigwa? Hao independent witness wanakuwa wapo kwa ajili ya kushuhudia kila kinachotokea au wapo kwa ajili ya kuhakikisha mtuhumiwa anasaini?
Sio vyema kabisa kufurahia matumizi ya nguvu kwenye upekuzi au ukamataji. Hapa bado tunahitaji sana maaskari wetu wapewe body cams ili kuepusha mambo kama haya. Kesi inajengwa kwa ushahidi imara na sio wa kulazimishana