Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Bonge moja la stori
 
Pugu ilijulikana kwa sifa hii kwa miaka mingi sana. Nashangaa serikali ya JMT inashindwaje kuweka mashine ya kuvuta maji na tanki kwenye shule kama Pugu. Akili ya JMT, wanaijua wenyewe tu.
 
Mimi nilikimbia kutoka viwege kwa muda mrefu sana. Nilipofika sehemu niliyokuta watu nilimuona dada mmoja anakaanga samaki nikamuuliza dada hapa ni wapi? Akanijibu hapa ni kilwa masoko nikazimia.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mmmh ila acha niende tu

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA TATU

Ilipoishia,,,,,,,,,,,

Basi kwa vile jamaa yangu Frank yeye ana account na ndio mtu nnaemuamini na ni mtumishi mzuri basi nikamkabidhi kibunda aniwekee kwenye account yake mpaka nitakapopata account, Kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye

Endelea

Basi nikahama pale kwa Frank nikahamia chuo campus, Nikafanikiwa kufungua account CRDB maana wao tuliambiwa boom linawahi CRDB kabla ya benki nyingine, Akilini napangia bajeti kile kibunda, nikasema nijibane nitumie nusu, halafu nusu niweke nikipata boom lingine niongezee ninunue PC (Laptop), maana story zilikuwa kwamba engineering bila PC hutoboi.

Basi baada ya kupata account nikasema nimcheki Frank ili anipe kibunda yangu niweke kwenye account, mzee pale ndo niliamini hela haina pastor wala mchungaji, nikaanza kupigwa sound, mara nipo mbali nikitoka nitaenda benki, Mara leo nimeenda benk ATM hazina hela, sound nyingi, siku nyingine namwambia sina hela hata ya kula basi ananipa elfu10 halafu anasema kesho nikija chuo tunaenda kwenye ATM, kesho ukimtafuta anakupiga chenga, mara hapokei simu, nikasema mzee hii balaa sasa.

Basi bana, akanizungusha wee, mwishoni ikabidi anichane ukweli, daah nilihuzunika sana, akaniambia kuwa alichukua hela yangu akachanganya na yake na mshikaji mwingine wakanunua pikipiki, wamempa mtu kila siku analeta elfu saba, Sasa nikamuuliza mi nitaishije, akasema usijali mi ntakuwa nakupa hela ya kula, pia ntakulipa kidogokidogo mpaka iishe, Nikasema daah hii mbona balaa tena.

Kiukwelii maisha yangu pale chuoni yakawa magumu sana, ikafika steji sina hela hata kumi, njaa inauma, Frank hapatikani kwenye simu, kwenda geto kwao kumefungwa hawapo, yaani hapo ndo maji unaita mma,

Pale hall two kuna matank ya maji ya kufulia na kuoga, huwezi amini yale yakageuka maji yangu ya kunywa, home naogopa hata kuomba hela maana hali halisi naijua, tena ingetakiwa mimi ndo niwatumie hela. Basi maisha yakaenda hivyo, siku nyingine Frank ananiipa elf 20, mara elf 10 mara asinipe, hivyo yaani.

Shule ikaanza, masomo kibao, mchana kutwa naranda randa kule Coet na drawing board langu, maana room ni mbali balaa , floor ya 11 na lift haifanyi kazi hivyo ni bora usubiri vipindi hukuhuku Coet.

Basi bana ikafika karibu na UE, PC nagongea kwa washkaji tu, siku moja nipo na PC ya mshikaji room napiga msuli mezani, Sasa inabidi nisome nimalize chapter zote kabla mwenyewe hajaja kuchkua PC yake, kwahiyo hata nikichoka vipi nasoma tu maana kesho yake kuna paper, Ilipofika saa tisa usiku nikawa nimetepeta balaa ,nimechoka balaa, usingizi huu hapa, nikasema cha kujifia ni nini nikaacha PC pale mezani nikasema nilale saa 11 nishtuke nimalizie, nikalala.

Kuja kushtuka saa 12, kucheki mezani PC hamna, umebaki waya wa adapter tu unaelea maana niliupitisha chini ya shuka kuelekea mezani nikawa nimeulalia, Basi nikajua jamaa watakuwa waliamka wakaizima maana niliacha inapiga mziki laini kwa mbalii, nikawashutua jamaa niwaulize aliyechukua PC mezani, wote wakasema hawajachukua, Duuh nikapata wazo au mwenyewe alikuja akaichukua, nikapanda floor ya juu nikamuulize, nikakuta bado kalala nikamwamsha nikamuuliza akajibu kwa kushtuka, hapana sjachkua, vipi imeibiwa??

Nikamwambia subiri, nikarudi room nikakuta jamaa bado wanadiscus kila mmoja anatoa mawazo yake, mwingine anasema alishtuka saa 11 akaikuta mezani, Daah sasa nani kachukua, mara mwenye PC akaja aliposikia jamaa wanavo discuss akajua PC yake imeibiwa, acha aanze kulia, tena kwa nguvu, PC yake Toshiba kanunua laki saba anaskia imeibiwa.

Basi bana, jioni ikafika, usiku ukaingia asubuhi kukakucha ndo hivyo tena PC imeenda, jamaa anataka hela au PC yake daah nikajiona sijui nna gundu, Basi ikabidi hela ya field ilipoingia takribani laki sita nimpe yote jamaa, Alafu mimi ntajua ntaishije, nitaendaje huko field na pia ntarudi vipi nyumbani, mzee usiombe yakukute.


Itaendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…