Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

SEHEMU YA NNE

Ilipoishia,

Basi ikabidi hela ya field ilipoingia takribani laki sita nimpe yote jamaa, Alafu mimi ntajua ntaishije, nitaendaje huko field na pia ntarudi vipi nyumbani,,,,,, mzee usiombe yakukute

Endelea,

Tukamaliza UE, chuo kikafungwa watu wakasepa zao makwao, wengine kwenye mikoa waliyoomba field, mzee mzima nipo bado sina muelekeo, Mfukoni sina hata coin, Daah ntafanyaje sasa, ila uzuri ni kuwa niliomba field makampuni mbali mbali ya hapo hapo Dar, Mungu saidia nikapata kampuni mmoja maeneo ya Temeke, Fine ila sasa nauli ya kwenda huko napataje, ntaishi wapi nitakula nini, ukisikia mtihani ndo huo sasa.

Nakumbuka siku hiyo nipo maeneo ya chuoni kule uwanjani nimekaa chini ya mti nna mzigo wa mawazo, mara nikapata wazo, pale Pugu madogo wa advance si bado wapo, kwanini nisiwe naenda kuwapigia pindi usiku? Sitakosa hela ya kuishi, nikaona ni wazo zuri, ila mziki unakuja nauli sasa natoa wapi, nikapata wazo hivi Frank alishamaliza hela yangu kweli? Hela zake ndogo ndogo mpaka niiikashindwa kujua kama kanimaliza au laa, banaee nikanyanyua simu nikamuendea hewani, nikamchana live kuwa hela yote nimempa jamaa wa pc (uzuri na yeye alikuwa anajua nimeiibiwa PC ya watu), basi nikamwambia anitumie hela maana sina hata ya kula, kweli mara nikasikia triiiiii, tigo imedhibitisha umepokea elf kumi kutoka kwa Frank, nikasema poa.

Ilikuwa kwenye saa nne hivi asubuhi nikapanda room (ufunguo nilikuwa nao), nikachkua begi nikaweka nguo zangu kadhaa nikasepa huyoo mpaka Ubungo, nikadandia gari ya Goms, niikafika Goms kama saa saba hivi, nikazuga pale mpaka kama saa kumi hivi nikadandia gari mpaka shule.

Nikapita nikaanza kuwatangazia madogo wa advance kuwa jioni kutakuwa na pindi la hesabu na physics, topic elfu 3 , kwa vile baadhi ya madogo walikuwa wananijua bado hivyo sikupata shida, wakajioganize nikawaambia nitarudi saa moja tuanze.

Basi saa moja nikarudi, nikakuta darasa lina madogo kama kumi hivi wa physics, nikaanza wakata pindi pale, ila nikaanza na intro maana nilikuwa sijajiandaa, basi nikamaliza wakaingia wa hesabu, kidogo walikuwa wengi, basi nikakata pindi hadi kama saa nne hivi, nikajivuta mapinduzi 3 nikatia mbonji pale mpaka asubuhi, kulipo kucha nikagonga uji na mandazi ya mama Mahinda pale nikasepa nikadandia gari huyoo mpaka Temeke nikaenda kuripoti field.

Basi ndo ikawa ratiba yangu hiyo, usiku nagonga pindi asubuhi nasepa kazini, uzuri kule field msosi wa mchana unagonga huko huko, mambo kidogo yakawa byeee, Mungu saidia nikamaliza field vizuri, matokeo yakatoka sina sap nikasema alhamdulilahi rabila lamini.

Basi chuo kikafunguliwa kuanza mwaka wa pili, ila ikaibuka kipembembe nyingine, kwamba mpaka ulipe ada uende na risiti ndo uruhusiwe kusain boom (maana mimi niilikuwa napata bumu 80%, kwaiyo kuna pasenti natakiwa nilipie ada), Daah sasa itakuwaje na sisi tunategemea tupate boom ndo litusaidie kulipia ada, huu nao ukawa mtiti mwingine.

Basi tukaenda pale block O ndo zinapatkana zile karatasi za risiti, ukishaipata unaenda na risiti basi wanakugongea muhuri ile karatasi halafu unaenda kwenye office ya loan unawaonesha ndo wanakuruhusu kusain boom, Sasa nilikuwa na mshikaji wangu kidosho, tukachukua zile karatasi, tukachukua na karatasi yenye muhuri basi tukaenda mpaka Riverside kwa wachonga mihuri, tukamuonesha ule muhuri akasema buku kumi kuutengeneza , tukabagain nae mpaka akakubalii buku tano, chap akatutengenezea, tukajaza zile karatasi tukaziigonga muhuri tukasepa haaoo hadi chuo, tukaunga mstari pale ofisi ya mikopo ila kiroho kinadunda, nikaacha kidosho atangulie kwanza, mara kidosho akazama, akakaa weee mara akatoka akaninyooshea dole, yaani safi, ikafika zamu yangu nikazama ndichi, basi nikawaonesha pale namimi nikasaini nikasema imetoka hiyo ikirudi pancha

Nikapanda paka room, kufika nikakuta kuna mabegi tu kwamba kuna watu wameshafika lakini hawapo pale, basi wazo likaniijia ukijumliisha na machungu ya kuibiwa pc, nikafungua begi moja la mgongoni nikakuta Dell mpya, nikaichukua nikafunga begi ile nataka kutoka nikaskia jamaa wanakuja, Daah hii balaa sasa, nikabaki na pc mkononi huku natetemeka, nahisi haja kubwa na ndogo zinakuja kwa mpigo, jamaa wamesha karibia mlango

Itaendelea
 
SEHEMU YA TANO

Ilipoishia,

Nikabaki na pc mkononi huku natetemeka, nahisi haja kubwa na ndogo zinakuja kwa mpigo, jamaa wamesha karibia mlango

(Kabla ya kuendelea niweke sawa kitu hapa, ni kuwa kabla hatujafunga chuo tulienda kuongea na waden, tulikuwa kama wa nne hivi wanaroom, tukaongea na wadeni ili tukirudi mwaka wa pili tuendelee kukaa room yetu pale pale, basi wadeni akasema atatupa vitanda viwili yaan double kwaiyo kila kitanda anataka laki mbili, basi tukakubaliana pale jamaa watoe alafu boom likija toka tunarudishiana, kwaiyo room yetu mwaka uliofuata ilibaki ileile ila wakachanganywa badae madogo wa first year)

Endelea,

Nikiwa bado nimesimama nawaza cha kufanya wazo likanijia, nikapita mlango wa kibarazani (baadhi ya room kwenye yale mahall zina vibaraza), nikatokea kibarazani, wazo jingine likanijia, nikashika zile kingo za kibaraza nikabembea nikarukia kibaraza cha room nyingine, Yaani hata sijui ule ujasiri nlitoa wapi maana inatisha sana, fikiri floor ya 11, ukiangalia chini unaona watu wadogo, mzeee wacha!!!!

Basi nikafungua mlango wa baraza wa ile room, Mungu saidia nikakuta hakuna mtu kwenye ile room, nikapanda juu ya meza nikaiweka ile pc juu ya kabati, nikashuka kucheki mlango upo wazi, nikatoka nje nikaona mlango wa room yetu maana ni majirani nikapiga hesabu, nikaona ngoja niingie room, nikafungua mlango nikaingia, nikakuta kumbe ni mshikaji mmoja kaja na demu wake kumuonesha room, basi nikawasalimia pale, nikamtaniatania shemu pale, Jamaa akaniuliza ndo umeingia nikamwambia ndio, huku najifanya napanga panga vitu vyangu basi nikawaaga pale nikamwacha jamaa na demu wake, kilichoendelea mimi sijui.

Basi nikashuka paka Kariakoo (kuna sehemu pale chini kunauzwa vitu panaitwa kariakoo) nikanunua juice na keki nikatafuta sehemu kwenye kivuli nikakaa nikala huku nawaza kwanza jamaa akigundua pc yake haipo itakuwaje, pili jinsi ya kwenda kuichukua kwenue ile room maana sina mazoea sana ya kuingia ile room.

Basi niikamaliza pale nikatoka nikashuka Coet kwenda kucheki cheki ratiba ya vipindi na matangazo, nikapata wazo niende kutembea Mabibo basi nikapiga zangu shatle pori (kutembea kwa miguu) kuelekea Mabibo yote ni kupoteza muda ili baadae nirudi room.

Basi nikazuga zuga Mabibo kule, jioni nikageuza zangu campas, kufika room nakuta jamaa wananisubiri kama kuku aliepigwa na jua sasa kashikwa na kiu balaa, Basi ile naingia tu nakumbana na swali toka kwa jamaa mmoja, Oya Akili sina umechukua PC yangu kwenye begi? Basi kwanza nikarilax halafu nikajibu kwa utani "imeshaenda hiyoo" , Jamaa akanisihi niache utani niwe serious, basi nikamwambia sijachkua kwa kweli, maana nilikuja mchana nikamkuta flani na demu wake basi nikasepa sahivi ndio narudi.

Basi nikamwona jamaa machozi yanamlenga, anatafuta PC hadi chini ya mto kana kwamba kaiweka huko, Basi bana gumzo likawa ndo hilo pc imeibiwa pc imeibiwa, tukakaa sana pale room tukijadili jinsi ya kuipata, jamaa akaahidi kama hataiona mpaka kesho asubuhi basi ataenda kwa mganga Bagamoyo, kweli tukampa support tena mimi ndo nakazia nikijifanya nna machungu ya kuibiwa PC na mimi, basi tukatawanyika pale kwenda cafteriia kutafuta menyu.

Kwenye saa tatu hivi nikaenda kwenye ile room niliyoweka PC, nikagonga nikaingia nikakuta kuna mshikaji kalala, nikajifanya namuulizia mshkaji flani hivi, jamaa akasema hajarudi kula bado, basi nikasema ngoja nimsubiri huku najifanya nasikiliza bongo fleva za zamanii zilizokuwa zinapiga kwenye PC pale mezani, jamaa akaendelea kulala tena kageukia ukutani sijui alikuwa kapiga mtungi, basi nikazuga pale nikapata chance nikapanda juu nikaivuta ile pc alafu nikarud nikakaa, nikatoa begi mgongoni nikaiweka halafu nikatulia

Basi nikamuaga jamaa nikamwambia ntarudi badae, basi nikatoka nikaenda kushukia ngazi za mwisho kabisa wa jengo ili kupunguza chance ya kukutana na wanaroom.

Basi nikashuka chini nikakamata shortcut ya kwenda Msewe, maana jamaangu kidosho alikuwa ameamua kupanga mtaanii, basi nikafika kwa kidosho pale nikakuta kapika ugali tukala, nikamwambia kesho kuna sehemu naenda sasa naacha begi langu pale nitalipitia nikienda, akasema poa.

Nikarudi zangu chuo, tukalala kukakucha asubuhi PC haijapatikana, Kweli jamaa akajiandaa huyoo Bagamoyo kwa bibi, mi nikajua ni biti tu ili kutia woga kumbe mshikaji kaenda kweli, Mida ya mchana akarudi akasema bibi kasema amesha mwona aliyechukua, ni wa humuhumu ndani kwahiyo kasema kesho wote tuende kwake, tukasema poa

Kesho kweli wote tukajiandaa haoo mpaka kwa bibi, tukafika tukakuta bibi ana mtu mwingine anamuhudumia hivyo tukaambiwa tusubirii nje kwenye jamvi, tukakaa pale wee, ila mimi moyoni Amani sina kabisa, sema najilazimisha tu nionekane nipo sawa, yaani ningepimwa presure pale nadhani ingekuwa juu karibu na kufa, mwisho tukaitwa tukaingiia, kwa vile chumba ni kidogo halafu tupo kama nane hivi basi tukajipanga chini kwa msitari,

Bibi kavaa kaniki yake, kajifunga na mavitambaa mekundu, kuna katoto ka kike ndo kinatafsiri yale Bibi anayosema maana sisi hatuelewii, Basi bibi akaanza na bonge la biti, halafu kila akiongea ananiangalia mimi machoni, basi macho yakigongana mi naangalia chini, basi daah yaan najiskia huku chini nimetota kabisa kwa hofu na woga, Bibi akaanza kuchoma ubani, mara akapandisha mashetani, akaanza kusema sasa, kwamba wazee wameshamwona aliechukua mali ya watu, lakini wazee wameona huruma wameamua kumpa huyo mtu nafasi, airudishe hiyo mali kwa mwenyewe, wazee wao wanajua kufunga tu, kufungua hawajuii kwaiyo asiije akalaumu mtu, wazee wametoa siku tatu hiyo Mali ipatikane (yeye anaita mali sijui hawezi kusema laptop).

Basi bibi akamaliza kutoa maneno yake pale huku yakiitafsiriiwa na kale katoto, basi akachukua kibuyu chake ambacho muda wote kilikuwa kinafuka moshi, akaanza kumpitishia kila mtu, anamzungushia kichwani huku anasema maneno yake, alipofika kwangu akanata kwanza, akatia pozi, watu wote kimya, mwili nikahisi kuparalize, nikasema enheee ukisikia kimbembe ndo leo, Basi nikajikaza mtoto wa kiume, bibi bado kapozi kwangu, watu wote wananikodolea mimi kuona ni nini kitatokea

Itaendelea
 
SEHEMU YA TANO

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,

Nikabaki na pc mkononi huku natetemeka, nahisi haja kubwa na ndogo zinakuja kwa mpigo, jamaa wamesha karibia mlango

(Kabla ya kuendelea niweke sawa kitu hapa, ni kuwa kabla hatujafunga chuo tulienda kuongea na waden, tulikuwa kama wa nne hivi wanaroom, tukaongea na wadeni ili tukirudi mwaka wa pili tuendelee kukaa room yetu pale pale, basi wadeni akasema atatupa vitanda viwili yaan double kwaiyo kila kitanda anataka laki mbili, basi tukakubaliana pale jamaa watoe alafu boom likija toka tunarudishiana, kwaiyo room yetu mwaka uliofuata ilibaki ileile ila wakachanganywa badae madogo wa first year)

Endelea,,,,,,,,,,,,

Nikiwa bado nimesimama nawaza cha kufanya wazo likanijia, nikapita mlango wa kibarazani ( baadhi ya room kwenye yale mahall zina vibaraza), nikatokea kibarazani, wazo jingine likanijia, nikashika zile kingo za kibaraza nikabembea nikarukia kibaraza cha room nyingine, Yaani hata sijui ule ujasiri nlitoa wapi maana inatisha sana, fikiri floor ya 11, ukiangalia chini unaona watu wadogo, mzeee wacha!!!!

Basi nikafungua mlango wa baraza wa ile room, Mungu saidia nikakuta hakuna mtu kwenye ile room, nikapanda juu ya meza nikaiweka ile pc juu ya kabati, nikashuka kucheki mlango upo wazi, nikatoka nje nikaona mlango wa room yetu maana ni majirani nikapiga hesabu, nikaona ngoja niingie room, nikafungua mlango nikaingia, nikakuta kumbe ni mshikaji mmoja kaja na demu wake kumuonesha room, basi nikawasalimia pale, nikamtaniatania shemu pale, Jamaa akaniuliza ndo umeingia nikamwambia ndio, huku najifanya napanga panga vitu vyangu basi nikawaaga pale nikamwacha jamaa na demu wake,kilichoendelea mi sijui

Basi nikashuka paka kariakoo ( kuna sehemu pale chini kunauzwa vitu panaitwa kariakoo) nikanunua juice na keki nikatafuta sehemu kwenye kivuli nikakaa nikala huku nawaza kwanza jamaa akigundua pc yake haipo itakuwaje, pili jinsi ya kwenda kuichukua kwenue ile room maana sina mazoea sana ya kuingia ile room

Basi niikamaliza pale nikatoka nikashuka Coet kwenda kucheki cheki ratiba ya vipindi na matangazo, nikapata wazo niende kutembea mabibo basi nikapiga zangu shatle pori ( kutembea kwa miguu) kuelekea mabibo yote ni kupoteza muda ili baadae nirudi room

Basi nikazuga zuga mabibo kule, jioni nikageuza zangu campas, kufika room nakuta jamaa wananisubiri kama kuku aliepigwa na jua sasa kashikwa na kiu balaa, Basi ile naingia tu nakumbana na swali toka kwa jamaa mmoja, Oya Akili sina umechukua PC yangu kwenye begi? Basi kwanza nikarilax alafu nikajibu kwa utani "imeshaenda hiyoo" , Jamaa akanisihi niache utani niwe serious, basi nikamwambia sjachkua kwa kweli, maana nlikuja mchana nikamkuta flani na demu wake basi nikasepa saivi ndo narudi

Basi nikamwona jamaa machozi yanamlenga, anatafuta PC hadi chini ya mto kana kwamba kaiweka huko, Basi bana gumzo likawa ndo hilo pc imeibiwa pc imeibiwa, tukakaa sana pale room tukijadili jinsi ya kuipata, jamaa akaahidi kama hataiona paka kesho asubuhi basi ataenda kwa mganga bagamoyo, kweli tukampa saport tena mi ndo nakazia nikijifanya nna machungu ya kuibiwa pc na mimi, basi tukatawanyika pale kwenda cafteriia kutafuta menyu

Kwenye saa tatu hivi nikaenda kwenye ile room niliyoweka PC, nikagonga nikaingia nikakuta kuna mshikaji kalala, nikajifanya namuulizia mshkaji flani hivi, jamaa akasema hajarudi kula bado, basi nikasema ngoja nimsubiri huku najifanya nasikiliza bongo fleva za zamanii zilzokuwa zinapiga kwenye pc pale mezani, jamaa akaendelea kulala tena kageukia ukutani sjui alikuwa kapiga mtungi, basi nikazuga pale nikapata chance nikapanda juu nikaivuta ile pc alafu nikarud nikakaa, nikatoa begi mgongoni nikaiweka alafu nikatulia

Basi nikamuaga jamaa nikamwambia ntarudi badae, basi nikatoka nikaenda kushukia ngazi za mwisho kabisa wa jengo ili kupunguza chance ya kukutana na wanaroom

Basi nikashuka chini nikakamata shortcut ya kwenda msewe, maana jamaangu kidosho alikuwa ameamua kupanga mtaanii, basi nikafika kwa kidosho pale nikakuta kapika ugali tukala, nikamwambia kesho kuna sehemu naenda sasa naacha begi langu pale ntalipitia nikienda, akasema poa
Nikarudi zangu chuo, tukalala kukakucha asubuhi PC haijapati kana, Kweli jamaa akajiandaa huyoo bagamoyo kwa bibi, mi nikajua ni biti tu ili kutia woga kumbe mshikaji kaenda kweli, Mida ya mchana akarudi akasema bibi kasema amesha mwona aliyechukua, ni wa humuhumu ndani kwaiyo kasema kesho wote tuende kwake, tukasema poa

Kesho kweli wote tukajiandaa haoo paka kwa bibi, tukafika tukakuta bibi ana mtu mwingine anamuhudumia hivyo tukaambiwa tusubirii nje kwenye jamvi, tukakaa pale wee, ila mimi moyoni Amani sina kabisa, sema najilazimisha tu nionekane nipo sawa, yaani ningepimwa presure pale nadhani ingekuwa juu karibu na kufa, mwisho tukaitwa tukaingiia, kwa vile chumba ni kidogo alafu tupo kama nane hivi basi tukajipanga chini kwa msitari,

Bibi kavaa kaniki yake, kajifunga na mavitambaa mekundu, kuna katoto ka kike ndo kinatafsiri yale Bibi anayosema maana sisi hatuelewii, Basi bibi akaanza na bonge la biti, alafu kila akiongea ananiangalia mimi machoni, basi macho yakigongana mi naangalia chini, basi daah yaan najiskia huku chini nimetota kabisa kwa hofu na woga, Bibi akaanza kuchoma ubani, mara akapandisha mashetani, akaanza kusema sasa, kwamba wazee wameshamwona alie chukua mali ya watu, lakini wazee wameona huruma wameamua kumpa huyo mtu nafasi, airudishe hiyo mali kwa mwenyewe, wazee wao wanajua kufunga tu,kufungua hawajuii kwaiyo asiije akalaumu mtu, wazee wametoa siku tatu hiyo Mali ipatikane ( yeye anaita mali sijui hawezi kusema laptop),

Basi bibi akamaliza kutoa maneno yake pale huku yakiitafsiriiwa na kale katoto, basi akachukua kibuyu chake ambacho mda wote kilikuwa kinafuka moshi, akaanza kumpitishia kila mtu, anamzungushia kichwani huku anasema maneno yake, alipo fika kwangu akanata kwanza, akatia pozi, watu wote kimya, mwili nikahisi kuparalize, nikasema enheee ukisikia kimbembe ndo leo, Basi nikajikaza mtoto wa kiume, bibi bado kapozi kwangu, watu wote wananikodolea mimi kuona ni nini kitatokea

Itaendelea
Dondosha nyingine sehemu ya sita, kabla ya wajuaji na wauliza maswali hawajaamka
 
SEHEMU YA PILI

Ilipoishia,
Basi nikazama ndani kwenye lile gari, lakini wakati napanda kuna mama alikuwa mbele yangu nikamvuta nikazama ndani, kumbe ni mke wa dereva wa lile gari,,,,,,,,,,

Endelea,

Basi yule Mama akapiga kelele, mme wangu wanatuvuta tusiingie, yule dereva akasema, asa we ulitaka wapande nini, ebu panda huko twenende, basi kimoyo nikajisemea yes dereva si ndo huyu, basi chuma ikawaka, tukaendaaa weee, hapo sasa ndo nikaanza kuskia maumivu ya mguu na vidole, nlikuwa sjayaskia, kujishishika naona majimaji nikajua hii damu, banaee tutajua kesho maadam nimepata usafiri haina noma, nikiwa kwenye lindi la mawazo ya kilichotokea, nawaza bwenini nimetoka hata tranka langu la maji sjafunga, maana pale shule kitu cha thamani kuliko vyote ni maji, basi bana nikiwa kwenye mawazo mazito mara naskia mtu ananigusa, oya umepona, kucheki ni mshkaji wangu Abdul Kisoda tunaishi nae mapinduzi 3, daah sikuamini nkamwita Kisoda ni wewe, daah we umefikaje huku akaniambia yeye alipata lori la mchanga likamleta paka kisarawe, sa nikamuuliza kwani ni nini kimetokea akasema yeye pia hajui, basi tukaendelea ila angalau sasa nna amani kidogo baada ya kumwona abdul kisoda

Basi tukafika sehemu tukakuta migambo wakasimamisha gari, wakamfata dereva wakamwambia huku mnakoenda ni mbali sana, hapa yenyewe mlipo ni mbali sana, ni bora muishie hapa, basii dereva akapaki pembeni tukashuka tukakuta watu wengine wengi pale, tukajisogeza pembeni kulikuwa na gari dogo imefungua milango yote alafu imewasha redio kwa sauti kubwa, basi pale ndo tukasikia habari kwamba mabomu yaliyokuwa yamehifadhiwa kambi ya jeshi gongo la mboto yamelipuka, watu wamekimbia kila mahali, juhudi zinafanyika kuyazima,

Daah basi tukakaa pale angalau sasa tunajua nini kimetokea, cha kushangaza tukajikuta wana bweni kama wanne hivi tumekutana pamoja, Na mshikaji wangu Hassan yeye ana mtoto mdogo kama miaka mitatu hivi wakike, tukamuuliza vipi tena na mtoto akasema kuna dada walikuwa wanakimbia nae sasa mtoto akamlemea ndo akamsaidia, Ila kamwachia namba za simu atamplelekea, daah nikaona mshikaji ana roho nzuri kweli, mi nimemkacha mlemavu kule shule, nafsi ilinisuta sana ila nikajipa moyo imeandikwa kila mtu na aiponye nafsi yake

Basi tukajikusanya wanafunzi wa Pugu tukachanganyika na wa Minaki tukawasha moto mkubwa, tukachuma majani tukalala, Basi kukapambazuka tukaanza safari ya kurudi shuleni, Sasa kumekuwa kweupe nikijiangalia sina tofauti chizi, suruali imepasuka, sina ndala, madamu yamegandiana kwenye miguu na vidole nikasema daah akili sina mimi nna tofauti gani na kichaa

Basi ile barabara ina hawa jamaa wanabeba magunia ya mkaa kwenye baskeli, nikamwona mmoja anapatashida kukokota kupandisha kilima nikaenda kumsaidia nikawa namsukuma hapo nyuma, kidogo ikanipunguzia aibu kwani nikawa kama na mimi ni mbeba mkaa sababu tunafanana ikapunguza hata watu kunishangaa, basi nikamsukuma yule jamaa paka tukatokea kisarawe, daah ni umbali mrefu sana, basi pale kisarawe tukakuta daladala za kwenda goms zipo, Hassan alikuwa na hela kidogo basi akatulipia wote tukapanda ( kumbuka nauli ni mia kwa wanafunzi)

Basi tukaondoka huko njiani tunakutana na mabomu ambayo hayakulipuka, ebwana ni makubwa, bomu kubwa hata mtu hubebi, pia tukapiita baadhi ya nyumba zina misiba, watu wao wamekufa na mabomu, Basi bana tukafika shule tukaanza kupeana story jinsi kila mmoja alivyookoka, Maji yangu kwenye tranka kama kawaiida nikakuta hola nikasema poa nikashuka pondi nikaoga freshi nikabadili nguo, Hasan akampigia yule dada mwenye mtoto akamwambia anakaa goms basi akaenda huko

Basi bana mitihani ikaisha shule ikaisha nikarudi zangu home kupigisha madogo mapindi, tena ukizingatia nimemaliza form six basi bonge la heshima pale kijijini
Siku zikaenda matokeo yakatoka sikufanya vibaya, nikachaguliwa kujiunga na degree yangu ya kwanza pale UDSM kitivo cha engineering, pale kijijini ilikuwa balaa walivyosikia naenda kusomea uinjinia, basi yaani hata ningesema nleteeni mabikira wote nichague wa kumuoa basi wazazi wangeleta mabinti zao ili wajaribu bahati zao, yaani nlikuwa kama mfalme pale kijijini

Basi mda ukafika, nikatimba Udsm Coet pale, Nlikuwa nmepewa hela kidogo hom nikafanya registration pale, uzuri nilishukia kwa jamaangu ambaye tulikutana pugu yeye alikuwa udsm , walikuja pugu kwenye semina ya kidini, basi akawa jamaangu ananipa ushauri mbalimbali , hata kabla sjamaliza pugu nilikuwa naenda udsm kumsalimia alikuwa anakaa hall 5, basi akawa ananipitisha maeneo ya chuo ili kunitia tamaa, na kweli nlikuwa nikirudi shule huo msuli ntakaopiga si wa dunia hii

Basi bana kwaiyo kabla sjapangiwa room pale chuo nikawa nakaa kwa jamaangu huyu Ambaye anaitwa Frank, kipindi hicho yeye na jamaa zake kadhaa walikuwa wamepanga mtaani maana walikuwa mwaka wa tatu, Basi nikawa naona jamaa wanapiga msulii balaa nikauliza mbona mnapiga msuli halafu hamuendi chuo, wakasema wanajiandaa na Sap, saa hiyo sijui hata sap ni nn, Basi naskia tu huyu ana Sap sita, mwingine nne, Jamaangu yeye alikuwa na sap tano, sasa nikajiuliza huyu jamaa mbona alikuwa vizuri hizi sap (maana waliniambia sap maana yake umefeli mtihani unatakiwa urudie) zote amepataje, maana hapo mwanzo aliwahi kunionesha vyeti vyake jamaa alipasua balaa, form four ana one ya saba, form six ana one ya nne tena PCM, sasa saivi nikiangalia hata past paper zake za chuo nakata tamaa kabisa, unakuta ana tatu ya kumi, 20 ya 60 nikasema khaaa shule ndo hivi

Basi bana chuo wakatupangia rooms, mimi nikapangiwa hall two, floor ya 11 side room, tunakaa nane room moja, basi sasa kimbembe kikaanza tukaitwa tukapewe boom, maana hatuna account hivyo tunapewa mkononi kule kwenye ofisi za auxiliary police, basi tukapanga foleen nikafika dirishani Kwa madam mmoja jina lake Rhoda, akanihesabia kibunda nikasepa, sasa hizi hela zote naweka wapi na ndo mara ya kwanza kushika hela nyingi hivyo kwa mkupuo (kama laki sita hivi)

Basi kwa vile jamaa ngu frank yeye Ana account na ndo mtu nnae mwamini na ni mtumishi mzuri basi nikamkabizi kibunda aniwekee kwenye account yake paka ntakapopata account, Kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye na ndo hapo kichapo kilipoanzia, na ndo msingi wa stori yangu unapoanzia


Itaendelea

Duuh Mabomu ya Gongolamboto hiyo 2011 nakumbuka tulikuwa tunajiandaa kulala mimi, mama na mamdogo mzee hapo hajarudi mdogo wangu hapo yeye kalala hata hajielewi. Mamamdogo akapigiwa simu na rafiki yake akasema kifo kimbieni akakata simu. Duuh tulimwamsha dogo hata hajielewi nakumbuka tulikimbia hadi Mbagala Chamanzi huko.
 
Back
Top Bottom