Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
story yako kama haina chawa si story hiiSEHEMU YA KUMI
Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,
Tukiwa tumekaa nje kwenye benchi tunapiga stori mara tukaitwa kule ndani, Basi nesi akatuambia majibu yenu tayari, ila kwa kuwa ninyi ni wapenzi na mna aminiana basi kila mmoja atasoma majibu ya mwenzake, tukasema sawa, basi mi nikapewa ya Sity na Sity akapewa yangu, Basi sity alipofungua majibu asome mara ghafla akashtuka kwa nguvu,
Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Moyo ukapasuka paaa!! Nikamuuliza Sity Vipi? Akatabasamu, Akasema, Nakutania bana, majibu yako mazuri, Yaani sema nilijizuia tu ila nilitaka nimkate bonge la bao, nikajisemea kimoyomoyo huyu analetaje utani kwenye mambo ya msingi, kwa kweli niliogopa sana tena ukizingatia zile mishe zangu za buguruni,
Basi nikacheki na majibu yake yapo poa, Yule nesi akatuhusia sana, kwamba tuwe waaminifu kila mmoja kwa mwenzake kama tunataka tuishi vizur, pia akasema yale majibu si ya mwisho, inabidi tukae miezi mitatu halafu turudi tena tupime hapo ndo tutakuwa na uhakika wa afya zetu,
Moyoni nikajisemea huyu nesi vipi, hajui kuwa hii mashine sjaiburuza bado, kwaiyo niisubirie tena miez mitatu, aaaah itakuwa ngumu aisee, Basi tukaitika pale sawa sawa, akatupa vipeperushi vyake tukaondoka, Tukasema tuelekee geto msewe poa,
Basi hakuna siku niliona msewe ni mbali kama siku ile, yaani tunatembea naona hatufiki, yaani natamani tufike nimrukie lakini daah ndo hivyo hatufiki aisee, Njiani huko masela wanamkodolea macho manzi balaa, maana huko nyuma kafungasha si kitoto, Wanaona nafaidi, kumbe mimi kama wao tu, wote tunakula kwa macho,
Kweli bana tukafika msewe, uzuri tukakuta kidosho hayupo, tulipofika tu ndani nikamtupia kitandani, nikaanza kula mambo yetu yale, mtoto akaonesha ushirikiano, tukagaragarazana kitandani, mara nikafanikiwa kumchojooa nguo zote akabaki na chupi, nayo nikaitoa, nikaanza kupima oil, mzee ni balaa najua wote mnajua yaliyoendelea, ila mtoto si kwamba kapewa tu mzigo ila anajua kuutumia, maana mzigo unazungukia pale kwenye kiuno ni hatari aisee
Basi nikafanikiwa kula tunda pale, tena nikajipimia tani yangu, tukamaliza mtoto akapika pale tukala, akaenda kuoga akavaa nikamsindikiza, hapo ndo ikawa mwanzo wa mapenzi mimi na Sity, mtoto alinikubali sana, kuna story nlikuwa naskiaga kwamba mabonge yanapenda kizembe kumbe kweli bana, Sity alinipenda balaa,
Basi shule ikaendelea, semista ikaisha, ikaanza nyingine nayo ikakata, Tukawa tumehitimisha safari ndefu ya miaka minne pale chuoni, Shule ndo imeisha hivyo,
Basi tukabaki mimi na kidosho pale geto, mziki ukaanza sasa kutafuta kazi, kwa vile matokeo ya mwisho bado, kwaiyo tukaenda chuo tukapewa transcript ya miaka mitatu ndo tukaanza nayo kutafuta kazi, Banaeeh hapo ndo nikaanza kujua kumbe kutafuta kazi ni kazi kuliko kazi yenyewe,
Tafuta kazi weee , ingia kwenye mitandao tafuta kazi wapi, paka matokeo yakatooka watu wakafanya graduation pale mlimani city , sisi hatukwenda maana hata hela ya joho hatukuwa nayo, Maisha yakaanza kuwa magumu maana tulizoea bumu, sasa hakuna cha bumu wala nini,
Basi tukaenda chuo kuchukua vyeti vyetu tukiamini vitasaidia kutafuta kazi ila wapi, Kipindi hicho ndo serikali ilikuwa imesitisha hajira, sijui mambo ya vyeti feki mi sijui mambo ya wana siasa,
Basi mwaka ukapinduka vidume mambo bado yamekaza, ilipofika mwez wa sita kidosho maji yakamfika shingoni, akasema yeye anarudi zake mkoani akacheki ishu nyingine, nikasema poa, mi sirudishi majeshi nyumbani, Ukizingatia kijijini dogo kashanipiga gap kubwa, yeye ana mji wake na familia mimi sina chochote zaidi ya laptop, na ntaenda kijijini kufanya nini, kama ni kulima si bora ningeanza kulima toka nilipo maliza shule ya msingi, nimekuja huku kufanyaje sasa, si ntakuwa nimepoteza muda bure, alafu hata elimu yangu itakuwa haina maana sasa kama ntarudi kuanza kutegemea wazazi, ntakomaa paka kieleweke,
Basi mzee nikabaki mwenyewe geto, Fikiri natakiwa nilipe kodi elf 50 kwa mwezi, bado umeme na maji, sjui kulipia taka taka, na kazi sina, Hapo ndo utajua kwanini mafua yanazibaga pua moja tu,
Basi mzee sikukata tamaa, bado napambana kutafuta kazi ila kila siku ni bora ya jana, Yaani aliekuwa ananiweka mjini ni Sity sasa, maana yeye ndo alikuwa anantumia elfu tano, nakula, mara analipa umeme paka kodi akawa analipa,
Akawa ananipa moyo sana kwamba nisijali ntapata kazi tu na mambo yatakaa poa, mwingine aliyekuwa ananisaidia ni dada mmoja wa chumba cha jirani, Alikuwa anaitwa Jamila, tukazoea kumuita Da J, Yeye akitoka mishe zake huko basi anapika msosi pale ananipa, siku nyingine nakwama umeme anantolea hivyo yaani,
Sasa baada ya kusota sana bila mafanikio nikaanza kwenda kushinda kwenye beting center, Pale riverside kwa ndani kuna sehemu kulikiwa na beting ya primier pale nikawa naenda kushinda pale, Sity akinipa buku tano nabania paka inabaki jero naenda kubeti pale, kulikuwa na mpira, michezo ya namba, michezo ya mmbwa, farasi na mingine, ikawa ndo hivyo ili mradi muda uende nirudi geto nilale,
Itaendelea
Sawa mamaa usijali. Nitakufikisha kibo na Mawenzi kadri ya matakwa yako na uta enjoy sana[emoji23][emoji23]Mtoa mada,
Sahii na wewe ukituacha solemba kama zile maandazi zingine niamini Mimi, tunafanya maombi ya kufunga kwa ajili yako.!!
Hamuwezi kutuacha kila siku na utamu wakati ndiyo tunakaribia kileleni..!!
Mzee kwani hapa kaweka details zote? Kuna vitu kibao kaviacha nina uhakikaKatika hali ya kawaida unawezaje kukumbuka vitu vya miaka zaidi ya 5 au zaidi iliyopita kwa 'detail' hivyo? Naona kama ni ngumu sana....
Vyovyote vile hadithi ni nzuri iwe ya utunzi au ya kweli. Nahisi wewe ni mtunzi maana unaishia sehem zenye 'suspense' ili msomaji ifuatilie kiliendelea nini kwneye muendelezo.
mkuu Vita ya Ukraine iishe tutaona mengi SanaHuu mwezi zinapigwa stori za kikamanda tu .
[emoji1][emoji1][emoji1]Stori ina basi 3,457 na Basi bana 25,798
USICHOKIJUA mpwayungu village na Akili Sina ni MTU mmoja.mpwayungu village uliringa sana na stories
Yako haya sasa dude lingine hili