Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiki kipande kimenigusa sana.SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,,
Daah haya majanga sasa, basi nikajikokota zangu kuelekea geto, ila shingo naiskia kama vile imefungiwa kamba alafu inavuta gari, Daah hawa jamaa si watu aisee, yan ukicheza unakufa hivi hivi,
Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,
Nikajikokota taratibu paka geto, shingo inauma balaa, Basi nikamsimulia Da J yaliyotokea akanipa pole sana, Akachemsha maji akanikanda shingoni angalau ikaachia kidogo,
Basi Da J akanipa elf 20 kesho nikatafute simu, Kesho yake nikiwa najiandaa kwenda kutafuta simu Mara Sity naye akaingia, Akauliza simu imepatwa na nini toka jana haipatikani, basi nikamsimulia pale akasikitika sana, basi tukatoka kwenda kutafuta simu, Pia tukafanya mpango wa ku renew line,
Maisha yakazidi kuwa magumu maana simu ndo nilikiwa nategemea kutafutia kazi mtandaoni, maana Pc nilisha iuza ili kulipa kodi ya chumba, Basi nikawa sasa ni kusambaza cv ofisi kwa ofisi,
Basi nikatafuta panga langu nalichomeka kiunoni alafu napita ile njia ili nikutane na wale vibaka lakini sikufanikiwa, Basi maisha yakaenda hivyo, Mda mwingi naenda kushinda pale beting jioni narudi geto kulala hivyo yani,
Siku moja nikaondoka geto niende kule beting, geto nikaacha kumetuliaa maana hakukuwa na mtu nyumbani, Basi jioni niliporudi nikamkuta Da J anafua nje, Akaniuliza we chizi vitu umepeleka wapi, au umeenda kuhonga huko kwa malaya zako, sa mi sikumwelewa, kuingia geto nakuta geto jeupe kimebaki kitanda tu na chaga, yaani hadi godoro hakuna,
Nikashtula sana, Da J akaja, Nikamwambia Da J nimeibiwa vitu, Da J hakuamini, Akasema, mi nimekuja nikakuta mlango upo wazi, nikajua upo ndani, sa nakuita naona kimya, kuingia nashangaa hakuna vitu nikajua umeamua kuhama,
Daah ukisikia majanga ndo haya sasa, basi nikatoka nikaulizia kwa majirani nao wanaishia kushangaa tu, Daah haya maisha acheni tu, Nikampigia Sity akaja, akanikuta pale nimekaa kama bwege, yaan sijui hata nafanya nini, Sity akaniambia hivi wewe utakuwa umemkosea nini Mungu, yaani juzi tu hapa umekabwa ukaibiwa simu, hata mwezi haujaisha unavunjiwa unaibiwa vitu, hapana bwana ebu jichunguze umemkosea nini Mungu,
Sa mi nikifikiria sioni nlipokosea, au sababu siendi kanisani, lakini ni muda tu siendagi kanisani, tangu nianze chuo paka namaliza sijawahi kwenda kanisani, sasa iweje sasa hivi ndo yatokee haya, Basi tukakaa pale paka giza likaingia,
Sity akaomdoka, Mimi ikabidi nifungue tu kile kitanda nitafute mabox nitandike chini, maana nisingeweza kulala juu ya chaga bila godoro, Da J akanipa mashuka ndo nikatandika chini na mabox nikalala, Cha kushukuru ni kuwa nyuma ya mlango nlikuwa nimetundika begi langu ambapo kuna material tuliokuwa tunasoma na vyeti vyangu vipo huko, sa sijui hawakuliona, au waliona ni makaratasi tu na mavitabu hayana ishu, mi sijui ila Mungu saidia lilikwepo,
Basi usiku sikulala nikawa nawaza sana haya yote yanatokana na nini, nikakumbuka yale maneno ya Sity kwamba nijichunguze huenda kuna sehemu nimemkosea Mungu, Basi nikaamka nikapiga magoti nikasali ili kama kuna nilipokosea Mungu anisamehe,
Nikiwa bado nawaza nikaona kabisa kuwa siwezi kuendelea kukaa dar, Huu mji umenikataa nisilazimishe, swali sasa niondoke niende wapi, Kurudi nyumbani hapana yani akili ndo haitaki kabisa kusikia hicho kitu, Sasa nitaenda wapi,
Basi wazo likanijia kule Arusha naskia kuna kiwanda cha nguo, alafu kuna jamaa zangu kama watatu tumemaliza nao chuo naskia wamepata kazi huko,Namba zao nlikuwa nazo sema ndo zikasepa na ile simu iliyoibiwa, ila sio case,Ni bora niende huko huko ntawatafuta tu huko, Ni bora niende tu na mimi nikajaribu maisha, Ila sasa nikifika ntafikia kwa nani, Daah maswali yakawa mengi ila majibu machache, ila moyo ukawa umeshakufa ganzi lazima lazima niondoke huu mji,
Basi kesho yake Sity akaja, nikamshirikisha wazo langu, akakubali kishingo upande ila na yeye maswali yakawa yaleyale niliyojiuliza usiku, Ila nikamtoa hofu kwamba mimi ni mwanaume lazima nipigane nisikae kizembe tu, na maisha ni popote, Basi akakubali ,shida ikaja ni nauli napata wapi, Basi nikasema nitafute mteja wa kile kitanda ndo nipate nauli,
Kweli nikatangaza kwa wadau mbalimbali mmoja tu ndo akasema atanipa elf 50, nikasema fine, Basi nikaanza maamdalizi ya kuamsha zangu Arusha, Da J alipokuja jioni nikamwelezea, akasema bana usiende , nikamwambia sa nikibaki hapa ntakaaje , sina chochote, lazima niondoke, akasema usiende huko utakufa, nikamwambia mwanaume haogopi kufa,
Basi yule jamaa akaja akachukua kile kitanda akanipa hela, Mda huo Sity alikuwa kaondoka akasema atakuja badae alale huku ili kesho anisindikize stand, Basi kweli badae badae hivi Sity akaja, Tukaongea pale, Akanipa elf 30 akasema ameenda kutafuta ndo kapata hiyo, Basi nikawa na elf 80 tayari, Usiku ukaingia tukatandika mabox tukalala, Nikala zangu mzigo wa mwisho mwisho huku nnasikitika huu mzigo ndo nauacha hivyo daah,
Basi saa 11 Sity akanishtua nijiandae, nikaoga pale fresh, nikawa najiandaa andaa pale, wakati najiandaa nikimwangalia Sity usoni machozi yanatiririka tu, Basi nikakaa nianze kum bembeleza, nikamwambia we ndo mke wangu, ngoja nikatafute ntakuja kukuchukua niamini mimi, basi akatulia,
Basi Sity akabeba begi tukatoka, Nikamgongea Da J , nikamuaga pale, Daah alihuzunika sana, Basi akanipa elf 10 akasema utakula njiani, Basi nikampa ufunguo wa geto aje ampe mwenye nyumba, ingawa kitasa kilikuwa kimevunjwa na wezi, Basi tukaaga pale tukasepa,
Tukafika ubungo, nikapata gari la saibaba, lilikuwa bado halija jaa basi tuka kaa na Sity siti moja tukaongea mengi tu, ila Sity alikuwa anajizuia lakini machozi bado yanatoka, Ilipofika saa moja gari ikataka kuanza kuondoka, Sity akashuka tukawa tunapungiana kwa chini, Basi chuma ikaamsha taratibu, Sity akawa analikimbiza gari paka likatoka nje ya kituo, Basi gari ikakamata morogoro road, Sity tukamuacha kasimama tu pale kaduwaa gari inaondoka, Basi chuma ikaamsha Arusha moja hiyo
Itaendelea
Mabomu yalianza ya goms kwenye miaka ya 2003 kwa mara ya pili ndo hayo anayasimulia OP mwaka 2011 kisha yakafuata ya mbagala(sikumbuki mwaka). Naishi Gongo la Mboto ndomana nimekumbuka miaka.Basi utakuwa mdogo Sana .Yalianza mabomu ya Mbagala ndo yakafuata ya Gongo la mboto wakati huo Hussein Mwinyi alikuwa waziri wa ulinzi(2009-2010)
Ha ha ha......... Sity akawa analikimbiza gari paka likatoka nje ya kituo, Basi gari ikakamata morogoro road, Sity tukamuacha kasimama tu pale kaduwaa ...
Subir mkuu mleta mada anapata kimoja Cha mkwez toka kwa shemeji yetu SITY asbh hii s unajua ndyo mke wake huyoTupiamo ka episodi kengine ka kufungulia wiki
Paspoti size mkuu mbn dk 3 tu.Hapa tu ndio umekosea. Passport hauwezi kuipata siku hiyi hiyo...
umeona eeh.yule mpwaungusijui anakaa kujibu mwisho anafyum anazira. dawa ni kutojibuShusha nondo, halafu nakusifu hata huwajibu wanoko wa chai kabisaaa. Endelea hivyo hivyo
Wale wajinga , hawaishii kumtaka mtu tu ila mpaka elimu huziitaji piaDaah..mawanang..umenikumbushaa mbaal..na mie nlishawah ona tangazo Kama uliloliona aww..cemaa m wahusikaa walikua sinzaa..@nlienda nmechomekeaa kinomaa cku iyo..kufikaa palee..nlichokaa. washenz wale et.nitembezeee mabakuli@daah..kugonga nyumba za watu kwa kwel hapanaa !boraa kuchomaa mahind!thanks God now nko pazur Kia's!it was 2014
Hakika huyu ni engineer maana sio kwa kutuinjinia vizuri wanajfNasubiri "SEHEMU YA KUMI NA TATU" kwa hamu sana.
Endelea kushusha vitu hvyo.
Hakika huyu ni injinia.Hakika huyu ni engineer maana sio kwa kutuinjinia vizuri wanajf
Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Sio usiombe yakukute, wewe ulikuwa ni lofa. Na nina mashaka mpaka now bado ni lofa!SEHEMU YA TATU
Ilipoishia,,,,,,,,,,,
Basi kwa vile jamaa yangu Frank yeye ana account na ndio mtu nnaemuamini na ni mtumishi mzuri basi nikamkabidhi kibunda aniwekee kwenye account yake mpaka nitakapopata account, Kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye
Endelea
Basi nikahama pale kwa Frank nikahamia chuo campus, Nikafanikiwa kufungua account CRDB maana wao tuliambiwa boom linawahi CRDB kabla ya benki nyingine, Akilini napangia bajeti kile kibunda, nikasema nijibane nitumie nusu, halafu nusu niweke nikipata boom lingine niongezee ninunue PC (Laptop), maana story zilikuwa kwamba engineering bila PC hutoboi.
Basi baada ya kupata account nikasema nimcheki Frank ili anipe kibunda yangu niweke kwenye account, mzee pale ndo niliamini hela haina pastor wala mchungaji, nikaanza kupigwa sound, mara nipo mbali nikitoka nitaenda benki, Mara leo nimeenda benk ATM hazina hela, sound nyingi, siku nyingine namwambia sina hela hata ya kula basi ananipa elfu10 halafu anasema kesho nikija chuo tunaenda kwenye ATM, kesho ukimtafuta anakupiga chenga, mara hapokei simu, nikasema mzee hii balaa sasa.
Basi bana, akanizungusha wee, mwishoni ikabidi anichane ukweli, daah nilihuzunika sana, akaniambia kuwa alichukua hela yangu akachanganya na yake na mshikaji mwingine wakanunua pikipiki, wamempa mtu kila siku analeta elfu saba, Sasa nikamuuliza mi nitaishije, akasema usijali mi ntakuwa nakupa hela ya kula, pia ntakulipa kidogokidogo mpaka iishe, Nikasema daah hii mbona balaa tena.
Kiukwelii maisha yangu pale chuoni yakawa magumu sana, ikafika steji sina hela hata kumi, njaa inauma, Frank hapatikani kwenye simu, kwenda geto kwao kumefungwa hawapo, yaani hapo ndo maji unaita mma,
Pale hall two kuna matank ya maji ya kufulia na kuoga, huwezi amini yale yakageuka maji yangu ya kunywa, home naogopa hata kuomba hela maana hali halisi naijua, tena ingetakiwa mimi ndo niwatumie hela. Basi maisha yakaenda hivyo, siku nyingine Frank ananiipa elf 20, mara elf 10 mara asinipe, hivyo yaani.
Shule ikaanza, masomo kibao, mchana kutwa naranda randa kule Coet na drawing board langu, maana room ni mbali balaa , floor ya 11 na lift haifanyi kazi hivyo ni bora usubiri vipindi hukuhuku Coet.
Basi bana ikafika karibu na UE, PC nagongea kwa washkaji tu, siku moja nipo na PC ya mshikaji room napiga msuli mezani, Sasa inabidi nisome nimalize chapter zote kabla mwenyewe hajaja kuchkua PC yake, kwahiyo hata nikichoka vipi nasoma tu maana kesho yake kuna paper, Ilipofika saa tisa usiku nikawa nimetepeta balaa ,nimechoka balaa, usingizi huu hapa, nikasema cha kujifia ni nini nikaacha PC pale mezani nikasema nilale saa 11 nishtuke nimalizie, nikalala.
Kuja kushtuka saa 12, kucheki mezani PC hamna, umebaki waya wa adapter tu unaelea maana niliupitisha chini ya shuka kuelekea mezani nikawa nimeulalia, Basi nikajua jamaa watakuwa waliamka wakaizima maana niliacha inapiga mziki laini kwa mbalii, nikawashutua jamaa niwaulize aliyechukua PC mezani, wote wakasema hawajachukua, Duuh nikapata wazo au mwenyewe alikuja akaichukua, nikapanda floor ya juu nikamuulize, nikakuta bado kalala nikamwamsha nikamuuliza akajibu kwa kushtuka, hapana sjachkua, vipi imeibiwa??
Nikamwambia subiri, nikarudi room nikakuta jamaa bado wanadiscus kila mmoja anatoa mawazo yake, mwingine anasema alishtuka saa 11 akaikuta mezani, Daah sasa nani kachukua, mara mwenye PC akaja aliposikia jamaa wanavo discuss akajua PC yake imeibiwa, acha aanze kulia, tena kwa nguvu, PC yake Toshiba kanunua laki saba anaskia imeibiwa.
Basi bana, jioni ikafika, usiku ukaingia asubuhi kukakucha ndo hivyo tena PC imeenda, jamaa anataka hela au PC yake daah nikajiona sijui nna gundu, Basi ikabidi hela ya field ilipoingia takribani laki sita nimpe yote jamaa, Alafu mimi ntajua ntaishije, nitaendaje huko field na pia ntarudi vipi nyumbani, mzee usiombe yakukute.
Itaendelea